Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-07-22 19:01:40    
Nchi za Afrika zafuata mkondo wa uwekezaji wa kimataifa

cri

    Uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nchi za ng'ambo ni nguvu muhimu ya kusukuma maendeleo ya kiuchumi. Katika miaka miwili iliyopita, kiasi cha uwekezaji wa moja kwa moja wa kimataifa duniani kilipungua sana kuliko kile cha mwaka wa 2000 na 2001. Lakini kutokana na kuhimizwa na hali nzuri ya uchumi duniani, kiasi cha uwekezaji mwaka huu kinatarajia kuongezeka. Mkutano wa biashara na maendeleo wa Umoja wa Mataifa uliofanyika mwezi Juni ulitoa ripoti ikieleza kuwa, uwekezaji wa moja kwa moja wa kimataifa utatokea duniani hivi karibuni.

     Japokuwa nchi za Afrika zinazochukua asilimia 12 ya idadi ya watu duniani zinavuta asilimia 2 tu ya kiasi cha jumla cha uwekezaji wa moja kwa moja wa kimataifa, lakini kwa nchi za Afrika zinazojaribu kuondokana na mgogoro wa kivita na kukuza uchumi wao, uwekezaji kutoka nchi za ng'ambo ni kama chemchem iliyopo jangwani. Hivi sasa, nchi za Afrika zinachukua hatua mwafaka kuimarisha ushirikiano wa kikanda na nguvu za mageuzi, ili kujaribu kuvutia vitega uchumi vingi vya kimataifa, na kuleta maendeleo ya uchumi wa nchi za Afrika.

    Mwaka 2003, vitega uchumi vya moja kwa moja vya kimataifa vilivyowekezwa katika nchi za Afrika vilifikia dolla za kimarekani bilioni 14.4, lakini uwekezaji huo hauna uwiano. Nchi kumi zikiwemo Angola, Nigeria, Algeria, Chad na kadhalika zimechukua asilimia 75 ya vitega uchumi vyote kutoka nchi za nje.

    Kwa mujibu wa takwimu za mkutano wa biashara na maendeleo wa Umoja wa Mataifa, nchi zinazovutia zaidi wawekezaji ni zile zinazozalisha mafuta kama vile Nigeria, Angola na Algeria. Na Ghana, Kenya, Morocco, Afrika kusini na Tunisia zimevuta uwekezaji mwingi katika maeneo ya nguo, viwanda vyepesi, utalii, mawasiliano ya simu, fedha na kadhalika. Nchi kubwa zinazowekeza vitega uchumi barani Afrika ni nchi zilizoendelea kama vile Uingereza, Ufaransa, Marekani, Ujerumani na Japan. Marekani na Ufaransa zinawekeza zaidi katika maeneo ya mafuta na migodi; Ujerumani, Uholanzi na Uswisi zinapendelea maeneo ya utengenezaji mashine, ambapo Uingereza inatilia maanani zaidi eneo la utoaji huduma, na vitega uchumi kutoka nchi za Asia vingi zaidi vipo katika maeneo ya nguo, viatu na vipuri vya magari.

    Katika miaka miwili iliyopita, nchi za Afrika zimefanya juhudi kubwa katika kutunga sera nafuu za uwekezaji. Ripoti iliyotolewa na mkutano wa biashara na maendeleo ilisema kuwa, mwezi Octoba mwaka 2002, nchi kumi za Afrika zilikuwa zimefanya marekebisho 20 makubwa ili kuvutia uwekezaji wa moja kwa moja wa kimataifa.

    Kutokana na hali tofauti ya kikanda na njia tofauti ya mawasiliano ya kibiashara, nchi mbalimbali za Afrika zina umaalum tofauti katika kuvuta vitega uchumi vya moja kwa moja. Misri, Morocco na Tunisia za kaskazini mwa Afrika zina uhusiano mzuri wa kibiashara na nchi za umoja wa Ulaya, hivyo zimevuta mitaji mingi zaidi kutoka umoja wa Ulaya. Nchi zilizoko kusini mwa Sahara, nchi za Afrika zimeanzisha kwa mfululizo mashirika ya ushirikiano wa uchumi wa kikanda au sehemu ya biashara huru, kama vile umoja wa Afrika Mashariki, umoja wa uchumi wa nchi za magharibi mwa Afrika magharibi, na umoja wa uchumi na fedha wa nchi za Afrika ya kati. Kampuni za kimataifa zinapenda kuchagua soko muhimu la sehemu hizo kama vituo vya uzalishaji na uuzaji bidhaa, na kuongeza uwekezaji.

    Wataalamu wanaona kuwa, nchi za Afrika zina maliasili nyingi, zina uwezo wa kuvutia mitaji mingi zaidi ya moja kwa moja kutoka ng'ambo. Inakadiriwa kuwa, katika kipindi cha mwaka 2-003 na 2004, mazingira ya uwekezaji barani Afrika yataboreshwa kwa kiwango kikubwa.

Idhaa ya Kiswahili 2004-07-22