Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-07-23 20:00:26    
"Wiki ya utamaduni wa China" kufanyika Mombasa

 


cri

    "Wiki ya utamaduni wa China" inafnayika kuanzia tarehe 16 hadi 23 huko Mombasa Kenya. Hii ni mara ya kwanza kwa Shughuli kama hizo kufanyika huko Mombasa, mji wa pwani wa Kenya.

    Mkurugenzi wa Idara ya mawasiliano na habari katika ubalozi wa China nchini Kenya Bwana Zhuang Yaodong alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa, kufanya shughuli za Wiki ya utamaduni wa China kunalenga kuimarisha zaidi maingiliano ya kiutamaduni kati ya wananchi wa China na Kenya, ili kuongeza maelewano na urafiki. Alisema kuwa, mwaka 2003, ubalozi wa China nchini Kenya ulifanya shughuli mbalimbali za kuadhimisha miaka 40 tangu kuanzishwa kwa uhusaino wa kibalozi kati ya China na Kenya. Kati ya shughuli hizo, "Wiki ya utamaduni wa China" iliwafurahisha zaidi wananchi wa Kenya. Ndiyo maana ubalozi wa China nchini Kenya umeamua kufanya tena shughuli za "Wiki ya utamaduni wa China" huko Mombasa, mji mkubwa wa pili wa Kenya ambao pia ni kituo cha utamaduni nchini humo.

    Kwenye ufunguzi wa "Wiki ya Utamaduni wa China" uliofanyika tarehe 16 huko Mombasa, Kenya, Balozi wa China nchini Kenya Bwana Guo Chongli aliwakaribisha watu wa hali mbalimbali wa Kenya pamoja na wajumbe wa wachina wanaoishi nchini Kenya. Balozi Guo alisema kuwa, utamaduni wa nchi mbalimbali duniani ni aina mbalimbali tofauti, China ni nchi yenye historia ya ustaarabu ya miaka 5000, siku zote inahifadhi vizuri mali zake za utamaduni, ikirithi utamaduni wa jadi na kuuenzi utamaduni kwa juhudi kubwa. Tokea yafanywe mageuzi na ufunguaji mlango nchini China, mafanikio makubwa yamepatikana katika sekta mbalimbali nchini China. Kuiwezesha dunia iifahamu China kumeisaidia China ijiunge vizuri na jumuiya ya kimataifa, na kusaidia kuongeza maelewano na mawasiliano ya kirafiki kati ya wananchi wa China na wa nchi mbalimbali duniani. Bwana Guo alisema, utamaduni wa China na wa Kenya ni wa mitindo tofauti, lakini wananchi wa nchi hizo mbili wote wanajivunia historia na utamaduni wao unaong'ara, maingiliano ya kiutamaduni yanayofanyika mara kwa mara kati ya nchi hizo mbili yataongeza maelewano na urafiki kati ya nchi hizo mbili.

    Maingiliano ya kiutamaduni kati ya China na Kenya yalianza tangu zamani sana. Mwanzoni mwa Enzi ya Ming ya China ya kale, kikundi cha meli cha China kiliwahi kufika sehemu za pwani ya Kenya, kupeleka vyombo vya kauri na kauri vilivyoonesha kiwango cha juu cha ustaarabu wa China, hatimaye kilirudi nyumbani China na bidhaa mbalimbali za huko zenye alama ya ustaarabu pamoja na wanyama teiga ambao walichukuliwa na China kuwa ni wanyama ajabu "Qiling". Hivi sasa katika sehemu ya pwani ya Lamu nchini Kenya, bado kuna watu ambao walikuwa vizazi vya wachina waliokuwepo kwenye kikundi cha meli cha China kilichowahi kufika sehemu za pwani za Kenya.

    Waziri wa nchi wa urithi wa mali za kitaifa wa Kenya Bwana Balala alihudhuria ufunguzi wa Wiki ya utamaduni wa China. Bwana Balala alikuja China siku chache zilizopita, ambapo alitembelea mji mkuu Beijing, mkoa wa Yunnan wanakoishi watu wa makabila madogomadogo wa China, na alipata picha kuhusu mafanikio yaliyopatikana katika ujenzi wa China na utamaduni wa jadi. Bwana Balala aliainisha kuwa, katika miaka ya hivi karibuni, Kenya na China zimeongeza mawasiliano na maingiliano. Katika sekta ya utamaduni, serikali za Kenya na China zilianzisha mapema mpango wa kupelekeana wanafunzi, kila mwaka wanafunzi wengi wa kila upande wanapewa nafasi na kusoma katika nchi ya upande mwingine, ambapo wanachukua kozi mbalimbali pamoja na utamaduni wa China au wa Kenya. Siku chache zilizopita, waziri wa elimu wa China alipofanya ziara nchini Kenya, alisaini mkataba wa ushirikiano na mhusika wa Chuo kikuu cha Nairobi kuhusu kuanzisha "Chuo cha Confucius" cha kufundisha lugha ya kichina. Hii itatoa fursa mpya ya kuimarisha maingiliano ya utamaduni kati ya wananchi wa China na Kenya.

    Shughuli za "Wiki ya Utamaduni wa China" ni pamoja na Maonesho ya picha za China yenye vivutio, siku ya chakula cha kichina na siku ya filamu ya China, shughuli hizo zinafahamisha historia na utamaduni wa China kwa wakenya, na kuwajulisha mafanikio mbalimbali waliyoyapata wananchi wa China tokea kutekelezwa kwa sera ya mageuzi na ufunguaji mlango. Katika maonesho ya picha za China yenye vivutio, zitaoneshwa picha 60 zilizopigwa na wapiga picha wa China ambazo zimeonesha mafanikio yaliyopatika katika sekta za utamaduni na ujenzi wa nchi ya China. Picha hizo zitawaoneshea wakenya mito na milima ya China iliyo ya kupendeza na mila na desturi za watu wa makabila mbalimbali wa China. Baada ya kutazama maonesho hayo, wakazi wawili wa Mombasa walisema:Siku zijazo, ubalozi wa China nchini Kenya utafanya shughuli za "Wiki ya utamaduni wa China" katika miji mbalimbali ya Kenya, ili kusukuma mbele maingiliano ya kiutamaduni na kuongeza maelewano na urafiki kati ya wananchi wa nchi hizo mbili.

Idhaa ya Kiswahili 2004-07-23