Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-07-26 19:06:27    
Safari katika mji mdogo wa Wuzhen

cri
    Mji mdogo wa Wuzhen uko mashariki ya China, muundo wa mji huo unaonekana kama msalaba. Kama ilivyo ya miji mingi ya kusini mwa Mto Changjiang, mto unapita kufuata mji huo na matawi yake makubwa na madogo yanafika kila mahali. Barabara zote zinazotanda kuelekea pande zote nne si ndefu. Kutoka mashariki hadi magharibi ni kilomita 3.75 na kutoka kusini hadi kaskazini ni fupi zaidi. Madaraja yenye maumbo mbalimbali yaliyojengwa juu ya mto huo yameongeza mandhari nzuri. Madaraja makubwa yanaonekana kama upinde wa mvua na madogo yamejengwa kwa kutumia pande la jiwe la jabali moja tu. Mapana yanaweza kupitisha gari na membamba yanawaruhusu watu wawili tu wapishane. Mbele ya milango ya baadhi ya nyumba kuna madaraja ya mawe na mbele ya nyumba za watu wengi zaidi kuna magati. Mji huo mdogo wenye historia ya zaidi ya miaka 1300 unaonekana kama picha ya kupendeza iliyochorwa kwa kufuata hali ilivyo.

    Ili kuwawezesha watalii kuhisi hali ya mji mdogo wa Wuzhen ilivyo, idara husika ya huko iligawa eneo la hekta 6 kuwa sehemu ya vivutio vya utalii. Bwana Ni Amao ni mfanyakazi anayeshughulikia huduma za utalii katika mji wa Wuzhen, alifahamisha:

 

    Sehemu yenye vivutio vya utalii ni pamoja na makazi ya jadi ya wakazi wa Wuzhen, hata pamoja na makazi makukuu ya mwanzoni; karakana za jadi, na kivutio cha utamaduni wa jadi. Kwenye mitaa yenye mikahawa jadi, watalii wanaweza kuonja chakula na vitoweo vingi vya jadi vyenye mitindo maalum ya sehemu hiyo.

    Katika sehemu kadhaa, yamebaki makazi yenye ua mkubwa wa zamani. Kwenye mtaa wa mashariki wenye mtindo dhahiri wa jadi, wakazi wa familia zaidi ya 350 wanakaa huko. Watalii wakifika huko wanaweza kuona sura pekee ya sehemu za kusini mwa mto Changjiang, madaraja madogo mbalimbali yalijengwa mahali pote ambapo nyumba za familia mbalimbali zikiegemea kando ya mto, na kusikia harufu nzito ya maisha ya huko.

    Katika makazi ya wakazi wa Wuzhen, roshani za maji zilizojengwa kwenye upande mmoja wa makazi unaokabiria na mto zinaonekana umaalum pekee na sehemu nyingine za kusini mwa mto Changjiang. Roshani hizo zilijengwa juu ya mto, zikihimiliwa na nguzo za miti au mawe, ndani wanaweza kukaa watu au kuwekwa vitu. Nyumba za familia moja moja zinazoegemea mto, zina madirisha pande tatu, wakazi wanaweza kuangalia mandhari ya nje kutokana na madirisha ya pande tatu.

    Kila kitu cha Mji mdogo wa Wuzhen kinahusiana na maji, kwa mfano nyumba za wakazi zilijengwa kando ya mto, madaraja mengi yalijengwa juu ya mto, wakazi wa Wuzhen wanafanya shughuli kwenye mto, na mji huo unategemea njia ya mto kuwasiliana na nje. Madaraja mbalimbali kwenye mto yamepunguza umbali wa kando mbili za mto, na madaraja hayo yanaonekana pia desturi na mila za mji huo.

    Madaraja ya Mji mdogo wa Wuzhen yenye maumbo mbalimbali tofauti yanahusika na desturi na mila za maisha ya wakazi wa mji huo. Kwa mfano, kila ifikapo sikukuu ya tarehe 15 Januari wakati wa mwaka mpya kwa kalenda ya kichina, wakazi wa huko hujipanga njiani kabla ya kuanzisha shughuli za kusherehekea sikukuu, wakazi walioshika taa mbalimbali za maua hutembea huku na huko wakipaswa kupita madaraja 10 tofauti. Hawapaswi kuzungukazunguka au kurudia njia waliyowahi kupita, walisema kuwa wakipita madaraja 10 tofauti katika siku hiyo, watakuwa na amani na utulivu katika mwaka mmoja.

    Mji mdogo wa Wuzhen wenye mandhari nzuri jinsi ilivyo na picha ya kupendeza, wakazi wa huko wanaishi maisha utulivu, na hawana matatizo ya kiuchumi. Kila mahali unaweza kuona kuwa wakazi wa huko wanapiga soga na kujiburudisha kwa starehe.

Idhaa ya kiswahili 2004-07-26