Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-07-27 21:45:20    
Kwanini ndege aliyelala usingizi hawezi kuanguka kutoka mtini?

cri

   

    Binadamu wanapolala wamezoea kujinyoosha kitandani, hata kama katika baadhi ya nyakati wanaweza kulala wakiwa wameketi, lakini wanashindwa kulala wakikaa vizuri. Lakini ndege wanapolala usingizi, huwa wanakaa kwenye vijiti vya mti, lakini hawawezi kuanguka chini. Je ni kwa sababu gani?

    Habari kutoka shirika la habari la Ujerumani, zinasema kuwa wanasayansi wa taasisi ya utafiti wa ndege wa Munich, Ujerumani hivi karibuni wamegundua siri hiyo. Mtaalamu wa ndege Jinter Poll alieleza kuwa yeye na wenzake wamegundua kuwa kazi za misuli ya binadamu na ndege ina tofauti kubwa sana, hususan wakati wanaposhika kiti ni kinyume kabisa.

    Bw. Poll alisema binaadamu na ndege wakilinganishwa, utakuta binadamu wanapotaka kushika kitu fulani hunyoosha mkono na kukishika, ambapo misuli inakazwa; lakini ndege hawawezi kuacha kitu wanachoshika ila tu kukaza misuli ya miguu yake, yaani maana yake ni kuwa ndege wanapotua kwenye kijiti cha mti, misuli ya miguu yao huwa inakazwa; lakini baada ya ndege kutua sawasawa kwenye kijiti, misuli huwa inalegea, hivyo miguu yake inakamata kijiti kwa uimara.

    Bw. Poll amesema kuwa kuna aina tofauti za ndege tofauti, na muda wao wa kulala pia unatofautiana, ndege aina ya thrush, wanahitaji kulala kwa saa moja hadi tatu, lakini ndege aina ya gogota pamoja na ndege wa aina nyingine wanaoatamia mayai yao ndani ya matundu mitini, wanahitaji kulala saa 6, na ni ndege wanaohitaji muda mwingi wa kulala. Aidha, wanasayansi wamesema kuwa wakilinganishwa na binadamu, ndege hawawezi kuulala fofofo, bali huwa ni kama wametulia na kupumzika tu, kwani hawana budi kuwa na tahadhari ya juu kutoka kwa maadui wanaoweza kujitokeza wakati wowote, ili wajiepushe na maafa.