Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-07-27 22:20:03    
Mawasiliano ya simu barani Afrika yana nafasi kubwa ya kibiashara

cri
    Katika mchakato wa mapinduzi ya teknolojia ya mawasiliano ulimwengini, bara la Afrika lilikuwa nyuma katika eneo hilo. Lakini katika miaka ya hivi karibuni, kwa kuambatana na mchakato wa uchumi huria unavyoendelea kwa kasi kubwa zaidi, mafanikio yanapatikana katika mawasiliano ya simu katika nchi mbalimbali za Afrika, na wakati huo huo, nafasi kubwa za kibiashara ziko katika kazi hiyo.

    Karika Afrika ya Kaskazini, mawasiliano ya simu nchini Misri yaliendelea kwa haraka sana. Katika miaka ya hivi karibuni, serikali ya Misri ilihimiza na kuziunga mkono nchi za kigeni kuwekeza vitega uchumi kuanzisha vituo vya utafiti na kufanya ushirikiano na makampuni ya Misri. Kutokana na sera nzuri ya serikali ya Misri, mafanikio makubwa yalipatikana katika biashara ya mawasiliano ya simu katika nchi hiyo. Mwaka 2000, mapato kutokana na mawasiliano ya Misri yalifikia Dola za kimarekani bilioni 1, na watu waliotumia simu za mikononi waliongezeka 110% na kufikia milioni 2.5, inatazamiwa kuwa, watu watakaotumia simu za mkononi nchini Misri mwaka 2007 watafikia milioni 7, familia zenye simu za waya zitafikia milioni 9.36.

    Nigeria ni mfano mwingine wa maendeleo ya mawasiliano ya simu katika Afrika ya Magharibi. Tangu mwaka 1999, serikali ya Nigeria iliuza haki ya biashara ya mawasiliano ya simu, na kitendo hicho kilihimiza sana maendeleo ya mawasiliano ya simu katika nchi hiyo. Kutokana na takwimu zilizotolewa na serikali ya Nigeria, mwaka 1999 uwekezaji katika sekta ya mawasiliano ya simu ulikuwa dola za kimarekani milioni 50, mwaka 2002 ulifikia dola bilioni 2.1, hadi mwishoni mwa mwaka jana, uwekezaji ulifikia dola za kimarekani bilioni 4. kiasi cha kuenea kwa simu nchini humo kilifikia 3.92% kutoka 0.4% mwaka 1999.

    Afrika Kusini ni nchi yenye soko nzuri la mawasiliano ya simu barani Afrika. Hasa katika miaka ya hivi karibuni, maendeleo makubwa yalipatikana katika kazi ya mawasiliano ya simu katika Afrika ya Kusini. Mwaka 2003, kasi ya ongezeko la simu za mkononi nchini Afrika Kusini ulichukua nafasi ya nne duniani, hadi mwezi Okatuba mwaka 2003, miongoni mwa watu milioni 450, watu wenye simu za mkononi walifikia milioni 150, mwaka 2006 idadi hiyo inatazamiwa kufikia milioni 21.

    Mbali na hayo, mafanikio ya kazi ya mawasiliano ya simu yalipatikana katika nchi za Cameroon, Togo, Cote Divoire za Afrika ya Magharibi, Kenya, Uganda za Afrika ya Mashariki na Botswana ya Afrika ya Kusini. Kampuni moja ilitoa takwimu kuwa, mwaka uliopita, watu waliotumia simu za mkononi katika sehemu ya kusini ya Sahara ya bara la Afrika waliongezeka kwa 37%.

    Jumuia ya benki ya dunia ilikadiria kuwa, katika miaka 5 ijayo, uwekezaji barani Afrika katika miradi ya ujenzi wa vyombo vya kimsingi vya mawasiliano ya simu utafikia dola za kimarekani bilioni 3.2. sasa, makampuni makubwa ya mawasiliano ya simu ya nchi mbalimbali yakiwemo Ericsson, Motorola, na Alcatel yanataka kumiliki soko la Afrika. Na makampuni ya mawasiliano kama Vodaphone na France Telecom yameanza kufanya biashara barani Afrika. Bila shaka, maendeleo ya mawasiliano ya simu ya Afrika pia yanaleta nafasi kwa makampuni ya China, kwa mfano, kampuni ya Huwei ya Shenzhen, Kampuni ya Zhongxing yameingia solo la Afrika.

    Lakini soko la mawasiliano ya simu ya Afrika bado lina hatari. Mtaalamu alisema kuwa, makampuni ya biashara za simu za mkononi ya Afrika kwa wastani yanapata faida ya dola za kimarekani 20-25 kwa kila simu, faida hiyo ni kubwa zaidi kuliko kiwango cha nchi zinazoendelea, sababu kubwa ni kuwa, watu wenye simu za mkononi wengi ni watajiri. Lakini hadi mwaka 2006, faida kwa kila simu ya mkononi itapungua na kufikia dola za kimarekani 10 kwa mwezi, makampuni madogo ya mawasiliano ya simu hayataweza kuendelea na biashara zao.

2004-07-27