Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-08-02 15:15:11    
Mkoa ujiendeshao wa Xinjiang Uygur

cri
    Nchini China watu wengi wakiutaja mkoa ujiendeshao wa Xinjiang Uygur, magharibi ya China hupata picha mkoa huo, ambao uko katika sehemu ya jangwa kubwa ambapo kuna zabibu tamu na wasichana warembo na wenye uchangamfu. Katika miaka ya hivi karibuni, sehemu ya Kanas yenye mandhari nzuri imekuwa ikisifisiwa sana na watalii wengi, wanasema kuwa, watu wakifika huko wanaweza kuburudika katika hali ya kujiunga pamoja na dunia ya kiasili.

    Kanas iko katika sehemu ya kaskazini ya mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Uygur, inapakana na nchi tatu Russia, Kazakhstan na Mongolia, tukipanda ndege kuelekea Aletai kutoka Urumuqi, mji mkuu wa mkoa wa Xinjiang, halafu tukipanda basi, baada ya saa 4 hivi tutafika Kanas.

    Basi likiingia sehemu ya milimani yenye miti mingi, watalii wataona kuwa, sehemu ya Kanas ni hifadhi moja ya kimaumbile, kivutio chake ni ziwa Kanas lililoko ndani ya misitu minene iliyozungukwa na milima mirefu, mwinuko kutoka usawa wa ziwa ni mita 1374, eneo lake ni kilomita za mraba 46. Ziwa la Kanas linazungukwa na milima yenye theluji na miti mingi mirefu, mandhari ya huko inapendekeza kweli. Sehemu hiyo ina wanyama pori na mimea pori ya aina mbalimbali. Pia sehemu hiyo ina miti mingi adimu, pamoja na wanyama adimu, ndege wa aina mbalimbali wenye thamani kubwa, na wanyama adimu wanaotambaa ambao wanaweza kuishi nchi kavu na ziwani.

    Wakati wa siku za joto, watalii wakifika Kanas hufuata mapendekezo ya wenyeji wa huko kuamka mapema asubuhi kwenda nje ya nyumba kuburudika na mandhari ya huko Kanas. Lakini asubuhi huwa na baridi kutokana na milima yenye theluji, hali ya baridi ya asubuhi ya sehemu ya Kanas huwawezesha watalii kusahau kama sehemu hiyo ya Xinjiang iko katika majira ya joto.

    Wakifika kando ya Ziwa Kanas, wataona kuwa ziwa hilo kwa kweli ni zuri na lina maajabu kama ilivyoelezwa kwa maana ya jina lake Kanas kwa lugha ya kimongolia. Mwongozaji wa watalii Bwana Li Dehua alifahamisha kuwa, sehemu nzima ya ziwa la Kanas ni kilomita 24, wastani wa upana wa ziwa ni kilomita 2. Eneo la ziwa hilo si kubwa sana, lakini ujazo wa ziwa hilo ni mkubwa sana, ambao unafikia mita za ujazo zaidi ya bilioni 5.

    Watalii wakilitizama ziwa kutoka kwenye kibanda kilichoko kwenye sehemu yenye mwinuko wa zaidi ya mita 2000 kutoka usawa wa ziwa, na mita zaidi ya 600 juu ya usawa wa ziwa, hisia zao zitaguswa kutokana na mandhari nzuri ya ziwa Kanas. Usawa wa ziwa hilo ni kama kioo kubwa sana ambacho kinaonesha mawingu mbalimbali yenye tofauti, vilele vya milima pamoja na misitu minene ya kando ya ziwa. Kwa kweli watalii huvutiwa na kujisikia burudani na furaha kubwa sana.

Idhaa ya kiswahili 2004-08-02