Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-08-03 15:30:46    
Barua za wasikilizaji 3/8/2004

cri
    Wasikilizaji wapendwa ni watangazaji wenu Chen na Fadhili Mpunji tunawakaribisha katika kipindi hiki cha sanduku la barua. Leo tunawasomea barua tulizopokea kutoka kwa wasikilizaji wetu, na kuwaletea maelezo kuhusu

    Msikilizaji wetu Mbarouk Msabah wa sanduku la posta 52483 Dubai Emirates ametuletea barua akisema kuwa, angependa kutoa pongezi zake za dhati kutokana na maelezo ya kuvutia kabisa yaliotangazwa katika kipindi cha sanduku la barua cha terehe 20 mwezi Juni mwaka huu, ambayo yalihusu kutimia kwa miaka 50 tangu China ilipotoa kanuni 5 za kuishi pamoja kwa amani

    Anasema kanuni hizo za kimsingi zilitolewa mwaka 1953 ambazo Waziri mkuu wa wakati huo wa China Bw. Zhou Enlai aliziwasilisha kwa viongozi wa nchi jirani za India na Burma ambayo sasa inaitwa Myanmar, zikiwa na malengo halisi ya kujenga mahusiano mazuri kati ya mataifa yote katika eneo la Asia ya Mashariki na kati. Kwani tukizingatia kwa makini kanuni 5 ambazo ni

    a. kuheshimu mamlaka ya nchi na ukamilifu wa umilikaji wa ardhi.

    b. Kutoshambuliana

    c. Kutoingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine

    d. Kuishi kwa usawa na kunufaishana.

    e. Kuishi kwa pamoja kwa amani

    Anasema, chini ya kivuli cha kanuni hizo 5 tutagundua kuwa Jamhuri ya watu wa China tangu kuasisiwa kwake, imekuwa na shabaha kubwa ya kujenga jamii yenye kuishi kwa amani, upendo, masikilizano na maendeleo ya pamoja na majirani zake.

    Anasema ulimwengu una kila sababu ya kuisifu Jamhuri ya watu wa China, kwa vile imekuwa ni taifa pekee lenye nguvu hapa duniani, ambalo kamwe halikuwa na sera za uingiliaji kati maswala ya ndani ya nchi nyingine, kutishia mataifa mengine, kuvamia kijeshi au kutawala mataifa mengine pamoja na kukiuka sheria za umoja wa mataifa kama tunavyoshuhudia leo yanayofanya mataifa mengine makubwa hapa duniani.

    Badala yake China imekua ni moja kati ya mataifa machache kabisa hapa duniani ambayo sera zake ni kuheshimu uhuru wa mataifa mengine, kujenga urafiki na maelewano miongoni mwa jamii za mataifa mbalimbali pamoja na kutoa ushirikiano kikamilifu katika kutafuta maendeleo ya pamoja kwa wanadamu wote, katika hali ya kuishi kwa amani na upendo miongoni mwetu.

    Bwana Msabah anasema, kwa mara nyingine angependa kuishukuru sana Redio China kimataifa kwa kuandaa maelezo kama hayo ambayo yalimpa imani kubwa juu ya sera za nje za China.

    Msikilizaji wetu Xavier Telly-Wambwa wa S.L.P 2287 Bungoma, Kenya ametuletea barua akianza kwa salamu kwa Mama Chen, Fadhili na wengine. Ansema kuwa HUKO Bungo ma Kenya yeye ni hajambo. Anasema anapenda kutumia fursa hii kushukuru kwa gazeti la China today toleo la Mei 2004 pamoja na picha tatu za wanyama adimu China walio katika hatari ya kutoweka ambapo serikali ya Jamhuri ya watu wa China inachukua hatua mbalimbali kuwahifadhi wanyama hao adimu.

    Licha ya matatizo ya aina mablimbali anayokumbana nayo huku na huko na kule, anasema anachukua fursa hii kumshukuru Mungu kumwezesha kila siku kusikiliza makala nzuri kutoka Radio China Kimataifa kila siku saa kumi na moja kamili hadi saa kumi na moja na nusu kupitia KBC-Kenya. Pia apenda kutumia fursa hii kutoa shukrani kwa salamu kutoka kwa wasikilizaji kama Bw Geoffrey P. Njereka, Bw Kaziro Dutwa, Bw Kilulu Kulwa, Bw Mogire Machuki, Bw Martin Nyatundo, Bw Bramuel Sirali, Bw Mbarouk Msabaha, Bw Franz Manko Ngogo wa Kemogemba pamoja na wasikilizaji wengine wengi.

    Anasema leo ana furaha tele hasa kwa kutuandikia nyaraka hii na kutoa maoni kuhusu vipindi mbalimbali vya Radio China Kimataifa.

Idhaa ya Kiswahili 2004-08-03