Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-08-04 14:24:53    
Sera ya elimu ya China yawanufaisha watoto wa familia maskini

cri
      Tangu miaka ya 90 ya karne iliyopita, watu wengi wa vijiji walianza kuhamia kwenye miji mikubwa. Kutokana na hali hiyo, watoto wengi waliofuatana na wazazi wao kuingia kwenye miji mikubwa walishindwa kupata nafasi za shule. Mbali na hayo, watoto wengi walikabiliwa na hatari ya kuacha masomo kutokana na umaskini. Kuhusu suala hilo, serikali za ngazi mbalimbali za China siku zote zimekuwa zikijitahidi kutatua suala hilo. Katika miaka kadhaa iliyopita, serikali pamoja na jumuiya mbalimbali za jamii zilianzisha "mradi wa matumaini" nchini China, na kuchangisha pesa kutoka serikali na vikundi vya jamii ili kuwasaidia watoto waliokosa elimu kutokana na umaskini. Sasa serikali za ngazi mbalimbali za China zimeanza kutekeleza sera mpya ya elimu, watoto wanaotoka kwenye familia maskini wanaweza kutolipa gharama za aina tatu za masomo ili kuwahakikishia watoto wanamaliza elimu zao za miaka 9.

    Kunming ni mji ulioko Kusini Magharibi mwa China, ni mji mkuu wa mkoa wa Yunnan. Serikali ya mji wa Kunming hivi karibuni ilianza kutekeleza mradi wa kuwasaidia watoto waliopoteza elimu kutokana na umaskini. Serikali ya Kunming ilitoa fedha zipatazo Yuan milioni 6 ili kuwasaidia wanafunzi 25,000 wa shule za msingi na sekondari mjini humo. Utekelezaji wa mradi huo uliondoa hali ya watoto kukosa elimu kutokana na umaskini. Ndugu Zhao Baosheng ni mkulima aliyefanya kazi mjini Kunming kwa miaka mingi. Alimwambia mwandishi wa habari kuwa, gharama za masomo kwa familia yake ni kubwa sana. Sasa utekelezaji wa mradi wa kuwasaidia watoto wa familia maskini unasaidia familia yake, alifurahi sana, akisema:

    "Tulikwenda Kunming na kufanya biashara ndogondogo mjini humo, gharama za masomo kwa mtoto wangu inafikia Yuan elfu moja kwa mwaka. Sasa sera mpya ya elimu inapunguza mzigo kwa familia yangu, ni sera nzuri sana."

    Wakati huo huo, serikali ya mji wa Kunming ilizitaka serikali za wilaya mbalimbali za Mji wa Kunming zishirikiane kutekeleza sera hiyo, ili kuongeza idadi ya watoto wanaonufaika na sera hiyo. Ofisa wa idara ya elimu ya Kunming Bw. Tian Weidong alisema kuwa, sera mpya inawasaidia watu wakiwemo watoto wyatima, watoto wa wazazi wasiokuwa na ajira na watoto kutoka familia za maskini. Aliona kuwa, sera hiyo si kama tu imepunguza mzigo kwa familia maskini bali pia imepunguza mzigo wa shule na idara husika za shina. Hivyo, sera hiyo inakaribishwa na umma. Anasema:  

    "kama sera mpya ya elimu haitatekelezwa, familia maskini haziwezi kumudu gharama za masomo kwa watoto wao, watoto hawawezi kwenda shule. Lakini hivi sasa serikali za mitaa zinawasaidia watoto kugharamia elimu, hivyo watu wanaikaribisha sana sera hiyo."

    Din Yawen na wazazi wake walifika Beijing miaka kadhaa iliyopita. Kwa kuwa Din Yawen hakuweza kuwa mkazi wa Beijing, hivyo hawezi kwenda shule mjini Beijing kama watoto wengine. Lakini hivi sasa idara husika zimeondoa vikwazo hivyo na miji mingi imeanzisha shule maalumu kwa watoto wa watu wa sehemu nyingine waliofanya kazi mijini humo. Na Ding Yawen amenufaika na sera hiyo anasema:

    "katika shule hiyo, walimu walituchukulia kama ni watoto wao. Nikiwa mgonjwa, walimu waliniambia nitumie dawa kwa wakati na kunipeleka hospitali kufanyiwa uchunguzi na daktari. Mbali na hayo, walimu hutumia wakati wa likizo kutusaidia kimasomo; kila siku baada ya masomo, shule inatupeleka nyumbani kwa basi, katika shule hiyo, si kama tu tunapata elimu, bali pia tunapata upendo."

    Takwimu zinaonesha kuwa, katika miaka 10 ijayo, watu walihamia mijini kutoka vijijini watafikia milioni 15, na watoto milioni 1 watafuatana na wazazi wao kuingia mijini. Mwenyekiti wa shirikisho kuu la wanawake la China Bibi Gu Xiulian alisema kuwa, kiwango cha elimu kwa watu wanaotoka wilayani na vijijini kinaamua kiwango cha elimu cha raia wote wa China na ustaarabu na maendeleo mazuri ya mazingira ya jamii. Hivyo, serikali za sehemu mbalimbali zinapaswa kuzingatia suala la elimu ya watu maskini na watu wanaofanya kazi mijini, anasema:

    "watoto wa wafanyakazi wanaohamahama hawana tofauti na watoto wengine, wana haki ya kuishi, kulindwa, kujiendeleza na kushiriki katika shughuli mbalimbali. Kuboresha kazi ya elimu kwa watoto hao na kulinda haki zao, ni muhimu kwa maendeleo ya uchumi wa China na utulivu wa jamii. Tunapaswa kuwazingatia zaidi watoto hawa na kuwaonesha upendo zaidi."

Idhaa ya kiswahili 2004-08-04