Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-08-05 21:53:46    
Masuali na majibu kuhusu ugonjwa wa ukimwi

cri
    Ni akina nani ambao wako kwenye hatari zaidi ya kukumbwa na MAHABUSI?

    Watu wafuatao ni maarufu kwa MAHABUSI, yaani wana hatari zaidi kuliko wenzao ya kupatikana na ugonjwa huu:

    1. Waasherati?yaani wenye kuruka mahali pengi hapa na pale badala ya kutulizana kwa uaminifu mahali pamoja.

    2.Makahaba.

    3 .Wanaume wenye tabia ya kujuana kimwili na wanaume wenzao kwa njia ya tupu ya nyuma. Hawa ni mashuhuri kipindukia.

    4 .Wanaume au wanawake wenye kujuana kimwili na yeyote katika makundi matatu yaliyotajwa juu?iwe ni ndani au nje ya ndoa.

    5 .Wakazi katika eneo ambalo ugonjwa huu umetapakaa kwa wingi sana na ambao wamekuwa wakidumisha uhusiano wa karibu sana na watu walio kwenye makundi hayo manne yaliyotajwa.

    6 .Wenye kupewa (kusaidiwa) damu za watu wengine mara kwa mara.

    7 .Wenye mazoea ya kushirikiana kujidunga wenyewe sindano za madawa ya kulevya.

    8 .Watoto ambao mama zao wana MAHABUSI, au mama zao ni maarufu kwa ugonjwa huu kama ilivyoorodheshwa.

    Kwa nini waasherati, makahaba, n.k. wako kwenye hatari zaidi kuliko wenzao ya kupatikana na MAHABUSI?

    Kwa sababu ya kukaribiana kimwili na watu wengi tofauti kundi hili lina nafasi kubwa zaidi ya kubahatisha kuokota MAHABUSI na magonjwa mengine ya zinaa kutoka kwa watu hao mbalimbali.

    Pia kwa sababu ya kufanya zinaa mara kwa mara zaidi kuliko wenzao (au kufanya zinaa kwa mtindo iliyo tofauti na wenzao) kuna uwezekano mkubwa zaidi kwa watu wa kundi hili kuchubuka katika via vyao vya uzazi pamoja na kuwa na vijeraha kutokana na magonjwa mengine ya zinaa. Vitu hivi (kuchubuka, vijeraha na utoko katika via vya uzazi) hufanya viiini vya MAHABUSI vipate mteremko wa kupenya mwilini.

Idhaa ya kiswahili 2004-0