Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-08-05 22:05:52    
Michoro ya wanawake wa Ansai

cri
    Ansai, jimboni Shaanxi iko katika ukanda wa chimbuko la utamaduni nchini China, yapo masalia mengi ya kale na mila chache za kikale. Wanawake wanaoishi sehemu hiyo wote wana maarifa ya sanaa za kukata karatasi, kutarizi na kufinyanga. Lakini wanavyojua zaidi ni kuchora michoro.

    Yafuatayo ni maelezo ya michoro ya wanawake wanne.

    Gao Jinai mwaka huu ana umri wa miaka 70. Bikizee huyu aliwahi kualikwa kufanya maonyesho ya sanaa ya kukata karatasi katika Chuo cha Sanaa cha China. Mara ya kwanza aliposhika brashi kuchora hakuona ugeni wala uoga, hakutumia muswada, bali alichora moja kwa moja kwenye karatasi, na alionyesha mtindo tofauti. "Kurudi Nyumbani kwa Mama" ni mchoro wake mzuri. Kwenye mchoro huo alitumia rangi nyekundu na buluu kuchora majani ya miti ambayo inaruka kulia na kushoto mbinguni, alichora ndege kwa ajili ya kuonyesha moyo wa furaha, pua ya kijani inaongeza mtindo wa wakulima. Michoro yake ilionyeshwa mara nyingi na kuhifadhiwa na Jumba la Sanaa la China.

    Chang Zhenfang ni mchoraji mpya wa wakulima. Anapenda kuchora wanyama kwa maumbo ya kijometri na maua. Mchoro wake "Paa na Chui" unaonyesha amani baina ya wanayma na uhai wa majira ya chipuko.

"Mti Mkubwa" ni mchoro wa mama Xue Yuqin. Aliuchora mti huo kwa samaki wa dhahabu wakubwa wakizunguka wadogo, halafu alichora vidudu mbalimbali kwenye majani, na kuonyesha nyuki wanaorukaruka karibu na mti. Ingawa ana umri wa miaka 50 tu, lakini ameshachora kwa miaka 14 na amewahi kutunukiwa tuzo ya kwanza katika mashindano ya michoro ya wakulima wa nchi nzima.

    Zhu Guanglian amekuwa mchoraji wa kuku. Mchoro wake wa "kulinda vifaranga" unavutia watazamaji. Mamakuku alichorwa kwenye maumbo kama ulimi wa moto na anatembea kifua mbele, inaonyesha kuwa ana furaha na ukali.

    Wachoraji hawa 4 wanakaa vijijini. Sikuu za kawaida wanalima na kupika chakula, hawana nafasi za kutosha za kuchora. Lakiini majumba ya sanaa ya vijijini yanawapa nafasi ya kutumia uwezo wao wa uchoraji.

Idhaa ya Kiswahili 2004-08-05