Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-08-06 20:23:41    
Michoro ya kijadi ya China

cri
    Michoro ya kijadi ya mwaka mpya ya China huwa na maudhui ya mfalme wa kuku kuimarisha nyumba. Inasemekana kwamba Mfalme Yao aliposhika hatamu, dola moja ndogo ilimtunukia Ndege wa Zhongming, sura yake ilifanana na kuku, na kulia kama Phoenix. Aliweza kupigana na wanyama wakali na kuweza kuwafanya jini kutothubutu kuwaletea madhara binadamu. Ndege hao walikwenda na kurudi mara kwa mara, walipokuja walikaribishwa kwa kusafisha nyua za watu na walipoondoka, watu walichongachonga sanamu yake ya mbao na dhahabu, na kuweka mlangoni ili kuwaogofya majini. Baadaye watu walikuwa wakiweka sanamu ya kuku milangoni kila baada ya sikukuu. Katika maisha ya kawaida kuku wanamithilisha tabia tano za uadilifu. Katika mabombwe ya baraka, kuku pamoja na Maua ya undu wa KuKu huonyesha kupandishwa cheo. Kuku wa kike akizungukwa na vifaranga watano wanaonyesha kwamba watoto watano wanapandishwa vyeo, jogoo na jua vikiwa pamoja vinaonyesha jogoo kuwika.

    Kuku pia wanamithilisha maana nyingine k.v. Wataiwan na watu wa kusini mwa Jimbo la Fujian wanaona kwamba kula nyama ya kuku kunaweza kustawisha familia, kwa hivyo maarusi huwa wanapaswa kula nyama ya kuku ili waweze kuishi maisha mazuri.

    Katika eneo la kaskazini ya Shaanxi, mashariki ya Jimbo la Gansu, watu hukatakata karatasi ya mabombwe ya watoto wenye michano ya umbo la kuku, kumithilisha: 1. kuku wanawaondoshea watoto maafa na zinguo. 2. kuku ni kama mwari wanaoweza kuolewa.

Idhaa ya Kiswahili 2004-08-06