Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-08-09 20:20:22    
Tusafiri kuelekea Kanas

cri
    Katika Sehemu ya Kanas yenye miti mingi mirefu na wanyama adimu, ndege wa aina mbalimbali wenye thamani kubwa, na wanyama adimu wanaotambaa ambao wanaweza kuishi nchi kavu na ziwani, Ziwa la Kanas linalozungukwa na milima yenye theluji linawavutia zaidi watalii.

    Watalii wakifika kando ya Ziwa Kanas, wataona kuwa ziwa hilo linapendeza kweli na lina maajabu kama ilivyoelezwa kwa maana ya jina lake Kanas kwa lugha ya kimongolia.

    Watalii wakipanda kibanda cha kuangalia samaki kilichoko kwenye sehemu yenye mita zaidi ya 600 juu ya usawa wa ziwa, hisia zao zitaguswa kutokana na mandhari nzuri ya ziwa Kanas. Usawa wa ziwa hilo ni kama kioo kubwa sana ambacho kinaonesha mawingu mbalimbali yenye tofauti, vilele vya milima pamoja na misitu minene ya kando ya ziwa. Kwa kweli watalii huvutiwa na kujisikia burudani na furaha kubwa sana.

    Kibanda cha kuangalia samaki kinaegemea ziwa kwa upande wake kaskazini, na pande za mashariki na magharibi zinaegemea miamba mirefu na mikali. Watalii wengi waliowahi kupanda kibanda hicho walisimuliwa na wenyeji wa huko hali kuhusu kibanda hicho, baadhi yao waliambiwa kuwa kibanda hicho kilijengwa kwa ajili ya kutazama jitu ajabu lililoko kwenye Ziwa kanas, wengine waliambiwa kuwa kutoka kibanda hicho wanaweza kuangalia samaki wenye sura tofauti na wengine. Mwongozaji wa utalii alisema kujenga kibanda hicho ni kwa ajili ya kuwasaidia watalii kuangalia samaki wa Zeluogui yaani samaki wekundu wa ziwa Kanas. Mwongozaji huyo alisema kuwa, samaki wa aina hiyo ana kichwa kikubwa chenye urefu wa mita moja hadi mbili, mwili mwake una urefu wa mita 4 hadi 5. Zamani watu walifuga ng'ombe na kondoo kwenye eneo la ziwa Kanas, na kuwaacha mifugo kunywa maji ya ziwa. Ilisemekana kuwa asubuhi ya siku moja, mtu mmoja aliona kuwa, wakati ng'ombe na kondoo walipokunywa maji ya ziwa, samaki mwekundu aliruka juu na kuburura ng'ombe hadi ziwani. Samaki wa aina hiyo ni nadra kuonekana, nao hujificha ndani sana ziwani.

   Kusimama kwenye kibanda cha kuangalia samaki, pia kunaweza kutazama maskani ya wafugaji wa makabila ya wamongolia na wakazakstan, ambapo mamia na maefu ya ng'ombe na kondoo wanaofugwa kwenye sehemu kubwa ya mbuga wanaonekana kama vito vyenye kung'ara vya aina mbalimbali vinavyotapakaa kwenye zuria ya kijani.

    Mlichosikiliza ni muziki uliopigwa kwa kinanda cha Chuwur, kinanda pekee cha watuwa, kupiga muziki kwa kinanda hicho pia ni njia ya watuwa ya kuwajulisha wageni hali ya Kanas. Kinanda hicho kilitengenezwa kwa mmeya adimu sana. Muziki murua uliopigwa na watuwa umewafanya watalii kujisikia kama kukaa nyumbani kwao, na kujisikia matumaini ya watuwa kwa maisha mazuri.

    Mpigaji kinanda cha Chuwur mzee Yedeerxi mwenye umri wa miaka 67 ni mpigaji pekee wa kinanda hicho nchini China. Aliwaambia watalii kuwa hivi sasa mtoto wake wa pili anajifunza kupiga kinanda hicho, amejifunza kwa miaka minne, baada ya miaka miwili au mitatu atashika ustadi na ataweza kupiga muzi pamoja na babu yake.

Sehemu ya Kanas yenye ziwa ya kuvutia, milima mirefu na muziki mwororo inawavutia watalii kweli.

Idhaa ya Kiswahili 2004-08-09