Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-08-10 20:31:33    
Kabla na Baada ya Miaka Mia ya Lhasa

cri

    Baada ya mvua hewa mjini Lhasa ilikuwa safi. Tarehe 3 asubuhi mapema mwezi huu nilikwenda uwanja ulioko mbele ya Kasri la Potala, huko niliwakuta vijana wawili wakirusha vishada, wakikimbia na kucheka kwa furaha. Kwenye lango la magharibi la Kasri la Potala karibu na mnara mweupe, watalii kiasi cha mia kutoka nchi za nje walisimama kwenye foleni wakisubiri kununua tiketi za kuingia kwenye Kasri la Potala.

    Tarehe 3, Agosti miaka 100 iliyopita, wavamizi wa Uingereza walijazana uwanjani na kwa nguvu walikalia mji huo wa Lhasa. Baada ya mwezi mmoja, wavamizi hao kwa singe walilazimisha utawala wa mji huo kukubali Mkataba wa Lhasa waliouandaa.

    Mkataba huo usio wa haki uliwapatia Waingereza haki za kufanya biashara huko, kupata huduma za posta na usimamizi wa forodha. Isitoshe, serikali kuu iliyokuwa dhaifu sana ya Enzi ya Qing iliipatia Uingereza kilo elfu 37.5 za fedha nyeupe kwa ajili ya kufidia hasara walizopata Waingereza katika vita vya kuivamia Lhasa.

    Mwandishi wa habari wa gazeti la Uingereza Daily Mail, Edmond Candler, ambaye alifuatana na wavamizi wa Uingereza alieleza hivi kuhusu hali ya Lhasa: "Uchafu wa Lhasa hauelezeki, hakuna mitaro ya kuondoa maji machafu, hakuna barabara ya changarawe, na hakuna nyumba safi hata moja inayovutia. Barabarani hakuna chochote ila tu mbwa wawili watatu wanaojitafutia riziki karibu na maji machafu. Katika mazingira machafu kama hayo, Kasri la Potala linajitokeza sana."

   

 Baada ya miaka 100, mwandishi huyo alikuwa mwandishi wa BBC, na kwa mara nyingine aliutembelea mji huo wa Lhasa. Katika habari zake alizoandika, alishtushwa kwa mabadiliko makubwa ya kisasa na hata soko la biashara ya hisa limetokea huko, na reli imekuwa ikiukaribia mji huo siku hadi siku.

    Ukisimama mlimani katika Kasri la Potala ambalo liliorodheshwa katika urithi wa dunia mwaka 1994, na kuangalia mbali, utaona mtaa wa mashariki wenye majengo ya zamani na mtaa wa magharibi wenye majengo marefu ya kisasa. Kasri hilo ni shahidi wa mabadiliko hayo yaliyotokea katika muda wa miaka 100. Lhasa umekuwa mji mkubwa wa kisasa wenye kilomita za mraba zaidi ya 50 kutoka kilomita za mraba pungufu ya 3.

    Katika Mkoa Ujiendeshao wa Tibet kuna jumla ya wazee 119 wenye umri wa miaka zaidi ya mia moja. Bibi Yu Zhen mkulima mwenye umri wa miaka 105 alisema, "Siku chache zilizopita, nilisindikizwa na binti yangu kwenda kufanya sala, kama nisingetambua mahekalu ya zamani nisingeweza kufahamu mahali nilipo ni mji wa Lhasa."

    Mtawa mmoja wa dini ya Buddha mwenye umri wa miaka 69, Qu Dian, alituambia, wazazi wake walimsimulia kuwa wavamizi wa Uingereza walikuwa waovu kwa kila kitu, waliunguza nyumba, kuua watu na kunyang'anya mali. Maovu yao yaliwakasirisha sana watawa na watu wa Tibet, na "watawa wengi waliuawa."

    Mkuu wa Taasisi ya Sayansi ya Jamii mkoani Tibet alisema, Mkataba wa Tibet hauthaminiki kwa kutokuwa na saini ya mwakilishi wa serikali kuu ya Enzi ya Qing huko Tibet.

    Alisema, "Kutokana na uchunguzi wa nyaraka zote za serikali ya zamani huko Tibet neno 'uhuru wa Tibet' halikuwahi kutokea kabla ya Waingereza kuivamia Tibet." Alitueleza, "Uvamizi wa Uingereza uliwaletea watu wa Tibet janga kubwa. Maelfu ya watu waliuwawa na mali nyingi ziliibiwa. Hadi sasa vitabu vya dini ya Buddha vilivyoandikwa kwa lugha ya Kitibet zaidi ya 460 viko katika maktaba ya Uingereza."

    Barabarani tuliona bendera nyingi nyekundu zenye nyota tano za taifa zinapepea huku na huko mjini Lhasa, baada ya kuona hali hiyo meya wa mji huo alinena mwenyewe, "Janga lililotokea kabla ya miaka 100 iliyopita kamwe halitatokea tena."