Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-08-12 20:56:55    
Hifadhi ya paa ya Dafeng

cri

    Jua kubwa linaangaza mbali juu ya vichaka. Ukungu unaelea kwenye mwambao wa Bahari Huanghai. Kundi la paa waitwao David's deer wananyemelea bwawa la maji. Ghafula ulisikika mshindo wa kutembea kwa watu, paa wote walishituka na kukimbilia vichakani. Hii ndiyo hifadhi ya paa ya Dafeng jimboni Jiangsu, yenye ukubwa wa hekta 1000.

    Mnyama huyu, zamani aliishi China tu katika maeneo makubwa. Kutokana na uwindaji usio mpaka katika enzi mbali mbali, mnyama huyu alitoweka kabisa mwituni katika karne ya 19. Kwa mujibu wa uchunguzi wa wataalamu, paa wa mwisho walitoweka katika mwambao wa majimbo ya Jiangsu na Zhejiang. Na paa waliofugwa katika Shamba la Uwindaji wa Nanhai mjini Beijing, walichukuliwa na jeshi la uvamizi la mwungano wa nchi nane mwaka 1900. Tangu wakati huo, paa wa aina hii hawakuonekana tena nchini China.

    Kwa ajili ya kuwarudisha paa kwao-China, marafiki wengi na bustani nyingi za Uingereza walifanya shughuli nyingi. Mwaka 1984 Shamba la Paa la Nanhai lilianzishwa upya mjini Beijing. Paa 20 waliorudishwa na Tavistock wa Uingereza waliachwa hapa. Agosti mwaka 1986 Mfuko wa Hifadhi ya Mazingira Duniani ulichagua paa 39 kutoka bustani 7 za wanyama za Uingereza na kuwapeleka Hifadhi ya Dafeng, jimboni Jiangsu. Paa hawa waliachwa ndani ya hifadhi waishi huria ili warudie tabia yao ya asili ya kuishi mwituni.

    Hali ya hewa ya hapa ni vuguvugu, mazingira ni safi na ya utulivu. Katika eneo la kilomita 80 za mraba hawaishi watu. Ni sehemu inayofaa paa waishi. Katika muda mfupi tu, paa hawa walikuwa wamezoea mazingira ya hapa. Hadi leo hii, vizazi vinne vimeshazaliwa. Na idadi ya paa pia imeongezeka na kufikia 346.

    Katika muda wa miaka 12 iliyopita, wataalamu wa hifadhi walifanya juhudi kubwa kwa ajili ya paa kuishi na kuzaliana. Baada ya uchunguzi utaratibu mzima wa maisha ya paa kuanzia kupandana, kushika mimba, kuota pembe, manyoyo na kutafuta vyakula. Leo hii, wanayma hawa adimu waliowahi kuishi nchi nyingine wanakua vizuri katika watani wao.

Idhaa ya Kiswahili 2004-08-12