Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-08-12 20:55:25    
Uwanja Mpya wa Ndege "Baiyun" Mjini Guangzhou

cri

   

    Siku chache zilizopita uwanja mpya wa ndege mjini Guangzhou ulifunguliwa. Uwanja huo umejengwa kwa vigezo vya juu vya viwanja vikubwa vitatu vya ndege nchini China kutokana na zana zake za kisasa, mazingira bora ya sehemu ya wasafiri kusubiri ndege, na mfumo wa kuhakikisha usalama. Sifa za uwanja huo ni zifuatazo:

    Jumba katika uwanja huo limejengwa kwa ukuta wa vioo, eneo la ukuta huo ni mita za mraba 140,000 ambao ni ukuta mkubwa wa kioo duniani.

    Mnara wa mawasiliano una urefu wa mita 112, ambao ni wa kwanza kwa urefu nchini China na ni wa pili katika bara la Asia.

    Uwanja huo unaweza kushughulikia wasafiri milioni 25 kwa mwaka na wasafiri 93,000 kwa saa katika kipindi cha wasafiri wengi.

    Mfumo wa kuhakikisha usalama ni wa kisasa. Mfumo huo umetumia sayansi na teknolojia ya kisasa na mtandao wa kompyuta katika ukaguzi wa usalama.

    Sehemu ya ndege kuruka na kutua ina mita za mraba milioni 7.2, hii ni sehemu kubwa iliyojengwa kwa fedha nyingi na kwa kigezo cha juu sana nchini China.

    Uwanjani kuna taa 56,726 na ukali wa mwanga wa taa katika sehemu ya ndege kuruka na kutua unajirekebisha wenyewe kwa mfumo wa kompyuta katika ngazi tano kutokana na mahitaji tofauti.

    Karakana ya ndege ni kubwa kabisa nchini China, ambayo iligharimu yuan milioni 930, eneo lake ni mita za mraba 103413. Karakana hii ina nafasi ya kuwekea ndege 4 kubwa za abiria kwa wakati mmoja, na ina uwezo wa kukarabati ndege 257 kwa mwaka.

    Uwanja huo wa ndege una uwezo mkubwa wa uchukuzi wa mizigo. Kituo cha kushughulikia uchukuzi wa mizigo katika uwanja huo ni kikubwa kabisa, eneo lake ni mita za mraba 101,303. Kina uwezo wa kushughulikia mizigo tani 80 kwa mwaka, ni kituo kikubwa cha pili katika Asia na ni cha tatu duniani.

    Uwezo wa kujaza mafuta kwa ndege pia ni mkubwa, ambao unaweza kujaza mafuta yenye ujazo wa mita 1000 kwa saa.

Idhaa ya Kiswahili 2004-08-12