|

Nchini China, riwaya ya "Jumba Jekundu la Ndoto" iliyoandikwa na Cao Xueqin, mwandishi maarufu wa riwaya wa Enzi ya Qing, inajulikana na watu wote. Katika miaka 200 iliyopita, hadithi ya mapenzi ya Jia Baoyu na Lin Daiyu, wahusika wakuu wawili katika riwaya hiyo, iliwavuta watu wasiohesabika na ilionyeshwa na wasanii wengi katika michoro, michezo ya kuigiza na filamu.
Miaka ya karibuni, katika soko la vitu vya utamaduni la mji wa Chengdu, Jimbo la Sichuan, kumetokea homa ya kukusanya vyombo vya kauri ya rangi vilivyochorwa hadithi ya "Jumba jekundu la Ndoto". Mkusanyaji anayejulikana kuliko wengine ni Long Jiesheng.
Long mwenye umri wa zaidi ya miaka 40 amekua katika mazingira ya utamaduni tangu utotoni. Baba yake alipenda vyombo vya kauri na michoro na majirani zake wengi pia ni watu wa mambo ya utamaduni. Wakati alipokuwa wa kijana, alipenda kukusanya stempu. Mwaka 1982, mzee mmoja aliyekuwa jirani yake alipohama, alimpa Long vyombo kadhaa vya kauri kama zawadi wakati wa kuagana. Kutokana na vyombo hivi, alianza ushabiki wake wa kukusanya vyombo yva kauri. Long amezama kabisa katika ushabiki wa vyombo vya kauri, kiasi cha kwamba, wazazi wake walipomwuliza anahitaji kitu gani kabla ya kufunga ndoa, bila ya kujifahamu alisema: "ninataka kurithi vyombo vyenu vya kauri."
Miaka 8 iliyopita, vyombo vya kauri alivyokusanya vilikwisha kuwa vingi. Siku moja alipoviangalia, aligundua kwamba vingi kati yake vina michoro mizuri inayohusu hadithi ya "Jumba Jekundu la Ndoto". Basi, kuanzia siku hiyo, kwa kusudi maalum, alianza kukusanya vyombo vya kauri vyenye michoro ya hadithi hiyo. Sasa, vyombo vya kauri ya rangi vya hadithi hiyo alivyokusanya ni vingi sana na vya namna mbalimbali kama vile vifaa vya kulia, vyombo vya kunywea chai na pombe, vifaa vya chooni, vifaa vya pombe, vifaa vya chooni, vifaa vya pombe, vifaa vya ofisini, vifaa vya kurembea, vifaa vya ofisini, vifaa vya kuvutia sigara, vipuzi, vyombo vya kuwekea vitu na mapambo.
Idhaa ya Kiswahili 2004-08-13
|