Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-08-16 17:44:03    
Vivutio vya mandhari ya milima na mito mkoani Zhejiang

cri

    Mkoa wa Zhejiang uko kwenye pwani ya mashariki ya China. Mkoa huo una vivutio vingi vya utalii, kama vile Ziwa Xihu mjini Hangzhou, mji mdogo unaopendeza wa wilaya wa Xitang, na mji wa Shaoxin wenye mito mingi yenye mitumbwi yenye vifuniko ya rangi nyeusi inayopita mara kwa mara. Aidha, mkoani humo kuna vivutio 11 vya ngazi ya kitaifa kama vile Ziwa Qiandao, yaani Ziwa la visiwa elfu moja kwa maana ya kichina, Mlima Yandang, Mlima Putuo, mkoa wa Zhejiang kwa kweli ni sehemu yenye vivutio vingi vya utalii.

    Eneo la Mkoa wa Zhejiang ni kilomita za mraba zaidi ya laki moja tu, mkoani humo kuna visiwa zaidi ya 2100 ambavyo ni vingi zaidi kuliko vilivyoko kwenye mikoa mingine nchini China. Idadi ya watu wa mkoa wa Zhejiang inakaribia milioni 47. Naibu mkurugenzi wa Idara ya utalii ya mkoa wa Zhejiang Bwana Yao Shenghou alipofahamisha umaalum wa vivutio vya utalii vya mkoa wa Zhejiang alisema:

    Mkoa wa Zhejiang una sehemu mbalimbali zenye vivutio vingi maalum vya utalii, kama vile Ziwa Xihu, Mlima Putuo na Mji mdogo wa Wuzhe vinavyowavutia sana wageni kutoka nchi za nje; na sehemu nyingine zenye mandhari nzuri kama vile mji wa Shaoxin, kila kivutio cha mandhari yake kina historia yake na utamaduni wake.

    Bwana Yao alisema kuwa, katika miaka 10 iliyopita, shughuli za utalii ziliendelea kwa haraka mkoani Zhejiang, kila mwaka mapato ya shughuli za utalii hufikia yuan bilioni 80, hii ni asilimia 9 ya pato la mkoa mzima. Mwaka jana mkoa huo ulipokea watalii zaidi ya milioni 1.8 kutoka nchi za nje, na watalii wa nchini milioni 84.

    Tukitaja vivutio vya utalii vya mkoani Zhejiang hatuna budi kuzungumzia sehemu yenye mandhari nzuri ya kupendeza ya Ziwa Xihu huko Hangzhou, mji mkuu wa mkoa wa Zhejiang. Wakazi wa mji huo, na watalii waliopita huko wote walivutiwa sana na mandhari nzuri ya kivutio cha mandhari ya Ziwa Xihu.

    Kwenye sehemu hiyo yenye eneo la kilomita 60 za mraba, kuna vivutio zaidi ya 40 vya mandhari nzuri na kumbukumbu zaidi ya 30 mabaki ya kale. Waongozaji wa watalii wanaweza kuwasimulia watalii hadithi nzuri kuhusu kila kivutio cha mandhari nzuri na kila kumbukumbu ya mabaki ya kale ya sehemu hiyo. Ziwa Xihu linaloonekana kama lulu linauongezea mji wa Hangzhou mvuto mkubwa, na kuwawezesha wakazi wa huko kuishi katika maisha ya hali ya utulivu na starehe.

    Mbali na vivutio vya sehemu zenye mandhari nzuri, mji wa Hangzhou una mvuto wa vyakula na vitoweo vitamu mbalimbali. Watalii wakienda Hangzhou hupenda kuonja vyakula vitamu vilivyopikwa kwa upishi wa sehemu ya kusini ya mto Changjiang, vyakula vyake vingi havitiwi chumvi nyingi, na havina ladha nzito, lakini vinapendeza kutokana na usafi na upikaji wa makini sana.

    Mpishi wa hoteli moja ya Hangzhou Bwana Liu Guomin alipofahamisha vyakula maarufu vya Hangzhou alisema:

    Samaki wa Ziwa la Xihu tuliwaopika ni chakula kitamu sana. Tulichimba dimbwi moja la kufuga samaki na kutumia maji ya Ziwa Xihu, tukiwafuga samaki hao kwa wiki moja ili wafyonze ubora wa maji ya ziwa hilo, halafu tunawapika kwa sosi, siki na sukari, wanakuwa chakula kitamu kinachowapendeza sana. Na mpishi huyo pia alifahamisha vyakula vingine vingi vya Hangzhou vinavyoonesha umaalumu wa upishi wa sehemu ya kusini ya mto Changjiang. Kweli watalii wakifahamishwa vilivyo watakuwa na hamu kubwa ya kutalii tena katika mji huo.


1  2  3