Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-08-18 16:18:35    
China yadhibiti mchanga kwa sayansi na teknolojia

cri
    Leo tunaelekea ukanda wa mbuga wa Hunshan Dake mkoani Mongolia ya ndani Kaskazini mwa China, kuangalia mabadiliko makubwa mkoani humo baada ya kudhibiti kwa njia za kisayansi na teknolojia mchanga unaohamahama.

    Ukanda wa mbuga wa Hunshan Dake ulioko Kusini-Mashariki ya mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya ndani, ni ukanda wa mbuga ulio karibu sana na Beijing, mji mkuu wa China. Miaka 3 na minne iliyopita, ukanda huo wa mbuga ulipoteza mandhari yake ya kuvutia, mimea ya aina mbalimbali ilikuwa ikipungua siku hadi siku na upepo mkali ulivuma mara kwa mara huko. Lakini baada ya kufanya juhudi kubwa, sasa mchanga unaohamahama umedhibitiwa, na uwanja wa mbuga umeanza kurudi katika hali yake, na hasa katika sehemu fulani, misitu imeanza kutokea.

    Mzee Zhang Chengxiang ameishi katika sehemu hiyo kwa miaka mingi. Katika miaka hiyo alishuhudia mabadiliko makubwa ya ukanda wa mbuga wa Hunshan Dake. Anasema:

    "Mwaka 2000 na 2001, baada ya kufanya juhudi za miaka mitatu za kudhidibiti mchanga uliohamahama kwa njia ya kisayansi na kiteknolojia kwenye sehemu hiyo, mazingira ya mbuga wa Hunshan Dake yameanza kufufua hali yake ya mwanzo. Lakini katika miaka michache iliyopita, mchanga uliohamahama ulikuwa umeenea kila mahali milimani"

    Wakati Mzee Zhang Chengxiang alipokuwa akizungumza machozi yalikuwa yanamtoka. Alisema kuwa, miaka michache iliyopita, kama hali mbaya ya kusambaa kwa mchanga haikuweza kudhibitiwa, ilikuwa itambidi yeye na familia yake waondoke nyumbani kwenda kuishi katika sehemu nyingine.

    Mabadiliko ya ukanda wa mbuga wa Hunshan Dake yalikuwa na manufaa kwa mradi wa udhibiti wa mchanga na upepo kwa serikali ya China. Katika miaka kadhaa iliyopita, ukanda wa mbuga wa Hunshan Dake ulibadilika kuwa jangwa, na kila majira ya "spring" yalipofika, upepo mkali wa mchanga ulikuwa ukivuma na ulikuwa unaleta athari kubwa kwa mazingira ya sehemu hiyo. Na upepo huo ulikuwa unafika Beijing na Tianjin, mji mkubwa ulio karibu na mji mkuu Beijing. Ili kubadilisha hali hiyo, China ilianzisha mradi wa udhibiti wa upepo mkali wa mchanga mjini Beijing na Tianjin. Sasa mafanikio makubwa yamepatikana katika eneo kubwa lenye kilomita elfu 50 za mraba ukiwemo ukanda wa mbuga wa Hunshan Dake, ulioko Kaskazini mwa China.

    Katika kazi ya kufufua mimea ya aina mbalimbali katika ukanda wa mbuga wa Hunshan Dake, idara nyingi zikiwemo Idara ya misitu ya China, Chuo Kikuu cha Kilimo cha China, na Taasisi ya Uhandisi ya China zikishirikiana kwa pamoja, zilitumia teknolojia za hali ya juu kwa kuchunguza na kudhibiti ardhi ya mchanga. Mwanasayansi wa Taasisi ya uhandisi ya China Bw. Wang Tao alijulisha kuwa, kutumia njia ya teknolojia ya hali ya juu kufanya uchunguzi na udhidibiti kunaweza kutoa msingi wa kisayansi kwa kazi ya udhibiti wa mchanga. Anasema:

    "Kazi ya uchunguzi wa hali ya jangwa ya sehemu hiyo ilianza mwaka 1995, tulitumia teknolojia za kisasa za upimaji kutoka mbali, na kupitia mfumo wa upashanaji habari kuhus hali ya kijioglafia na teknolojia nyingine za hali ya juu. Hadi sasa tulitekeleza mara mbili kazi za ukaguzi wa hali ya jangwa katika sehemu hiyo, tumepata msingi wa kutegemeka kwa kukinga mchanga na kuzuia ardhi isipanue kuwa jangwa, teknolojia hiyo ni ya kisasa duniani kwa hivi leo."

    Njia hiyo ya kudhibiti mchanga inaenea na kufanya kazi kubwa katika udhibiti wa mchanga kwenye ubagu wa Hunshadak.

   Bw. Wangtao anasema:

   "Zamani tulichukua hatua za kibaiolojia au kupanda miti ama majani kwenye eneo la ukingoji mwa jangwa, ama kuweka vikwazo vya kuzuia mchango uliohamahama. Mbali na kutumia dawa ya kuzuia mchanga iliyotengenezwa kwa njia ya kikemikali ili kuuwezesha mchanga unaohamahama kutulia kwa muda mrefu kwenye ardhi, watu wa sehemu hiyo pia walipanda miti tofauti au majani kwenye sehemu tofauti zinazofaa.

    Ingawa mafanikio makubwa yamepatikana katika kazi ya kudhibiti mchanga kwa njia ya kisayansi na kiteknolojia, mtafiti wa Taasisi ya misitu ya Chuo Kikuu cha kilimo cha China Bw. Zhaosheng alisema kuwa, katika kazi ya udhibiti wa mchanga ya siku za mbele, China inapaswa kuimarisha zaidi matumizi ya sayansi na teknolojia katika kazi hiyo. Anasema:

    "Kwenye sehemu zenye upepo mkali na mchanga mwingi, upandaji majani kwa nguvu kazi za watu na kwa ndege unapaswa kuendelea zaidi. Mbali na hayo, serikali ingeanzisha vituo vya vielelezo vya kudhibiti mchanga kwa njia ya kisayansi na kiteknolojia, vyuo vikuu na idara husika za utafiti zinatazamiwa kufanya utafiti zaidi kuhusu udhibiti wa mchanga, na serikali ingetoa uungaji mkono kwa kazi za utafiti, ili kuzidisha matumizi ya sayansi na teknolojia katika kazi hiyo."

Idhaa ya kiswahili 2004-08-18