Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-08-23 20:29:46    
Ghala la Kuhifadhi Maandishi Yaliyogunduliwa katika Mapango ya Dunhuang Kuzinduliwa Mjini Beijing

cri

Maktaba ya Taifa ya China   

    Mapango ya Dunhuang yako katika kitongoji cha Mji wa Dunhuang, mkoani Gansu, kaskazini magharibi mwa China. Mapango hayo yalichongwa mlimani kuanzia mwaka 366 kwenye genge lenye urefu wa kilomita mbili kutoka kusini hadi kaskazini kwa safu tano kutoka juu hadi chini, ni mapango maarufu duniani.

    Siku chache zilizopita, ghala la kuhifadhi maandishi yenye miaka elfu moja yaliyogunduliwa katika mapango ya Dunhuang lilizinduliwa mjini Beijing katika Maktaba ya Taifa ya China.

    Mwaka 1900 chumba cha kuwekea maandishi kiligunduliwa ndani ya mapango ya Dunhuang mkoani Gansu, magharibi mwa China. Ndani ya chumba hicho kulikuwa na msahafu na maandishi elfu kumi kadhaa ya tokea karne ya nne hadi ya 11 nchini China. Kusikia habari hiyo, "wapelelezi" wa Uingereza, Ufaransa, Urusi, Marekani na Japan walikimbilia huko na kupora idadi kubwa ya maandishi, vitambaa vya hariri, picha za ukutani na sanamu za kuchongwa na kuzisafirisha kisiri siri kwenda makwao. Mwaka 1910 serikali ya Enzi ya Qing iliamrisha serikali ya huko kusomba yaliyobaki hadi mjini Beijing, lakini njiani yaliibiwa tena na walinzi wa maandishi hayo. Hivi sasa mengi ya maandishi yaliyosalia yanahifadhiwa nchini China, na pia katika nchi za Uingereza, Ufaransa na Russia. Hivi sasa maandishi na vipande vya maandishi elfu 16 yanayohifadhiwa nchini China katika Maktaba ya Taifa ya China ni mengi kuliko yaliyoko kwenye nchi nyingine. Lakini jambo linalosikitisha ni kuwa maandishi hayo adimu yalirundikana katika masanduku madogo mbalimbali miaka hadi miaka, mazingira ya kuyahifadhi yalikuwa mabaya na ilikuwa ni vigumu kutumika. Mwaka 2003 serikali ya China ilitenga fedha kwa ajili ya kutengenza vikasha, makabati na kujenga ghala la kuhifadhi maandishi hayo, mazingira ya kuhifadhi maandishi hayo yamebadilika kuwa ya kisasa.

    Ghala lilijengwa kwa mtindo wa China ya kale, na lina vifaa vya kuhakikisha jotoridi na unyevunyevu maalumu kwa mwaka mzima. Vikasha na makabati yote yametengenezwa kwa mbao maalumu isiyoweza kuliwa na mchwa. Kila kabati liligawanywa vyumba vya kuwekea vikasha na kila kikasha kinawekwa makala moja, jumla viko elfu 16. Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Utamaduni wa Mapango ya Dunhuang, Proresa Hao Chunwen, alisifu sana alisema, "Maandishi ya Mapango ya Dunhuang licha ya kuwa na thamani kubwa ya maandishi yake, na thamani kubwa ya utamaduni, lakini thamani ya utamaduni haitakuwepo kama maandishi yasikuwepo. Kwa hiyo ghala la kuhifadhi maandishi hayo lina maana sana, na pia ni muhimu kwa watafiti."

    Prof. Hao Chunwen alisema kuwa baadhi ya watu wanasema kuwa maandishi mengi yameibiwa na China imebakiwa na machache tu. Huo si ukweli, yaliyobaki nchini China ni mengi zaidi na thamani ya maandishi hayo inaongezeka zaidi kufuatana na utafiti unavyoendelea. Zaidi ya hayo, baadhi ya maandishi yenye thamani kubwa zaidi yaliyokuwa mikononi mwa maofisa wa zamani baadaye yalirudishwa kwenye maktaba.

    Kutokana na uchumi unavyoendelea nchini China serikali imeongeza fedha inazotenga kwa ajili ya hifadhi ya utamaduni wa kale, naibu mkutubi mkuu Bw. Chen Li alisema, "Katika miaka ya karibuni licha ya kujenga ghala hilo pia tumerudufu nakala zaidi ya 700, na sasa kazi tunayoifanya ni kukagua maandishi ya China ya kale nchini na kufanya mpango wa kuyahifadhi."

    Kuhifadhi ni kwa ajili ya matumizi, mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Utamaduni wa Mapango ya Dunhuang Prof. Hao Chunwen alisema, serikali ya China ilianzisha kituo cha utafiti wa maandishi ya Dunhuang mwaka 1983, na mwaka 2002 tovuti ya Maktaba ya Taifa ya China ilianzishwa kwa ajili ya elimu ya utamaduni wa Dunhuang, watafiti wanaweza kusoma makala zilizohifadhiwa katika maktaba hiyo na Maktaba ya Taifa ya Uingereza. Prof. Hao Chunwen alisema, "Katika miaka ya 80 ya karne iliyopita elimu ya utamaduni wa Dunhuang nchini China ilikuwa nyuma ikilinganishwa na nchi nyingine kama Japan na Ufaransa. Lakini baada ya miaka 20 kupita kutokana na juhudi za wasomi wazee, watu wa makamo na vijana, elimu ya utamaduni huo nchini China inaongoza duniani, tunaweza kusema kuwa utamaduni wa Dunhuang sio tu upo nchini China na kwa sisi Wachina bali pia tumetoa mchango mkubwa zaidi katika utafiti wa elimu ya utamaduni wa Dunhuang.

Idhaa ya Kiswahili 2004-08-23