Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-08-24 21:08:14    
Elimu ya China inayowahudumia wachina bilioni 1.3 (sehemu B)

cri

    Hivi sasa, China imeanzisha duru jipya la "Mpango wa utekelezaji wa kuendeleza elimu". Kutokana na mpango huo, ifikapo mwaka 2007, fedha zitakazotengwa kwa ajili ya elimu zitaongezeka na kuwa asilimia 4 ya pato la taifa kutoka asilimia 3.4 ya sasa, na nyongeza ya fedha hizo itatumika zaidi katika elimu kwa vijiji vya China.

    Nyumba za wakazi wa vijiji vyenye hali duni vya sehemu ya magharibi ya China zimetapakaa huku na huko, nyingi haziko karibukaribu, hivyo ni vigumu kwa sehemu hiyo kuboresha zaidi hali ya elimu. Kutokana na hali hiyo, idara za elimu za China zitachukua hatua kubwa ya kuanzisha shule za bweni ili kuwawezesha wanafunzi wa vijiji vya sehemu hiyo wapate nafasi ya kusoma katika shule za bweni zenye hali nzuri ya masomo na walimu wa kiwango cha juu. Katika shule hizo wanafunzi wataweza kusoma katika shule za bweni katika siku za wiki, na jumamosi na jumapili wataweza kurudi nyumbani. Serikali itawapatia misaada ya maisha wanafunzi wenye matatizo ya kiuchumi, ili kuhakikisha wanasoma bila matatizo.

    Serikali ya China inapojitahidi kueneza zaidi elimu katika sehemu zote nchini China, ili kulingana na hali ya sekta ya elimu inazozifungulia mlango nchi za nje, pia inaeneza masomo ya lugha za kigeni katika shule za msingi nchini China. Mwandishi wetu wa habari alipotembelea mji wa Urumuqi wa mkoa unaojiendesha wa Xinjiang ambao ni sehemu ya makabila madogo ya kaskazini magharibi ya China aliona kuwa, wanafunzi wa shule za msingi wa kabila la waurgu pia wanajifunza lugha ya kiingereza.

    Wanafunzi wa shule ya msingi waliimba wimbo wa kiingereza katika darasa la kiingereza.

    Wakati juhudi za kuimarisha elimu ya msingi zinapoendelea, serikali ya China pia inaweka mkazo katika kuendeleza elimu ya vyuo vikuu. Katika miaka kadhaa ya hivi karibuni, vyuo vikuu vya China vimekuwa vikiongeza kwa kiasi kikubwa idadi ya wanafunzi wa hali mbalimbali. Mwaka huu idadi ya wanafunzi walioandikishwa katika vyuo vikuu vya China ilikuwa ni zaidi ya milioni 4.2. Hii ni idadi kubwa kuliko miaka yote iliyopita.

    Ingawa idadi ya wanafunzi wanaosoma katika vyuo vikuu imeongezeka kwa kiasi kikubwa, lakini kutokana na idadi kubwa sana ya wanafunzi nchini China, hivi sasa idadi ya wanafunzi wanaosoma katika vyuo vikuu bado ni asilimia 17 tu ya wanafunzi. China inatazamiwa kuongeza idadi ya wanafunzi wanaosoma katika vyuo vikuu ili ifikie asilimia 32 ya idadi ya jumla ya wanafunzi ifikapo mwaka 2020.

    Wasikilizaji wapendwa, huu ndiyo mwisho wa makala yetu ya leo. Sasa tunawataka msikilize kwa makini maswali mawili tukayowasomea ili muweze kuyajibu vizuri.

Swali la kwanza: Elimu ya lazima nchini China ni miaka mingapi?

Swali la pili: Katika miaka kadhaa ijayo fedha zaidi zitakazotengwa na China kwa ajili ya elimu zitatumika kwa ajili ya elimu mijini au vijijini?

  Wasikilizaji wapendwa, mlikuwa mkisikiliza makala ya pili ya chemsha bongo kuhusu ujuzi wa Miaka 55 ya China mpya. Wiki ijayo wakati kama huu tutawaletea makala ya tatu kuhusu hali ya jumla ya maisha na maendeleo ya watu wa makabila madogomadogo zaidi ya 50 nchini China. Hadi hapa ndio kwa leo tumekamilisha kipindi hiki cha Sanduku la barua, ni watangazaji wenu Chen na Fadhili Mpunji tukiwaaga hadi jumapili wiki ijayo wakati kama huu kwaherini.