Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-08-25 18:10:09    
AIDS (UKIMWI) 17

cri
    Katika kupambana na magonjwa yatakayojaribu kukunyemelea silaha yako kubwa ni kuwahi mapema kutibiwa kila upatapo ugonjwa wa aina yoyote. Usipuuze ugonjwa hata uwe mdogo kiasi gani.

    Katika kujitahidi kuepuka kueneza viini vya ugonjwa wako kwa wengine yafaa uzingatie yafuatayo:

1. epukana na uasherati. Kufanya matembezi na watu wengine huku ukijua kwamba una MAHABUSI ni sawa na kufanya kitendo cha uuaji.

2. kama itawezekana jizuie usioe au usiolewe; lakini kama hiwezekani basi yafaa umweleze yule utakayeoana naye kuhusu ugonjwa wako, na ikiwa mtaridhiana itabidi kila mara mtakapofanya kitendo cha ndoa mchukue tahadhari za kuvaa mpira na tahadhari nyingine za uzazi wa majira ili kuzuia kuambukizaan ugonjwa pamoja na kuzuia kubeba mimba.

3. usitoe damu yako kuwapa wengine; na kama wewe ni mwanaume usitoe maji yako ya kiume ya uzazi yapewe kina mama wanaohitaji kupata watoto.

4. usiruhusu sindano zilizotumika kukudunga zitumike kwa watu wengine. Mweleze daktari wako jambo hili kila mara anapoagiza upigwe sindano.

5. usishirikiane na watu wengine wembe, au mswaki, au kitu kingine chochote kitakachokuwa kimeguswa na damu yako au na majimaji mengine yatakayokuwa yanakutoka.

    Mipira ya kuvaa uumeni husaidiaje kuzuia MAHABUSI isienee?

    Mpira unaovaliwa uumeni unaweza kufananishwa na mfuko uliofunika "kidole" cha mkono. Mfuko huu hukusanya maji yale yanayotoka ambayo yana viini vya MAHABUSI. Ijapokuwa mfuko wenyewe ni mwembamba sana lakini imethibitika kwamba viini vya ugonjwa haviwezi kuupenya na kutoka nje. Hata hvyo mfuko huo unaweza usisaidie kitu endapo uangalifu mkubwa hautachukuliwa wakati wa kuutumia. Mambo yafuatayo ni muhimu yazingatiwe wakati mfuko huo unapotumika.

1. mfuko uvaliwe kila mara kitendo hicho kinapofanyika.

2. mfuko huo uvalishwe "kidoleni" kabla ya kwanda-wakati "kidole" kimekuwa imara.

3. mfuko usivutwe sana mpaka ubane ncha ya "kidole". Yafaa kuacha nafasi kidogo (kiasi cha cm. 2 hivi) mwishoni mwa mfuko huo kwa madhumuni ya kupokea maji yatakayotoka-mifuko mingine inayo kijimfuko kidogo nchani kwa kusudi hilo.

4. ikiwa kwa bahati mbaya mfuko utapasuka kabla kitendo hakijamalizika yafaa kuacha kila kitu na mfuko mwingine mpya uvaliwe.

5. mara tu baada ya maji ya kiume kutoka na kabla "kidole" hakijalegea "kidole" na mfuko wake vitolewe nje huku kingo za mfuko huo zikiwa zimeshikiliwa kwa mkono ili kuzuia hata tone moja la maji lisiweze kutoka nje ya mfuko huo.

6. mfuko mpya utumike kila mara kitendo hicho kinapofanyika. Mfuko uliokwishatumika lakima utupwe hata japo uonekane kwamba bado ungali mzima na hauna dosari.

7. kama kutakuwepo na haja ya kulainisha mfuko huo kabla ya kuanza, mafuta ya chakula yanaweza kutumika kwa kusudi hilo, lakini si vizuri kutumia vaseline au mafuta mengine yatokanayo na petroli kwa vile mafuta ya aina hiyo huweza kuudhuru mfuko. Mate yasitumike kulainisha mfuko-kwa vile yanaweza yakawa yana viini vya MAHABUSI.

8. mifuko mipya ambayo haijatumika ihifadhiwe mahali pakavu na pasipokuwa na joto kali.

9. mifuko iliyotoboka; au iliyopoteza ulaini wake; au iliyoanza kunatanata isitumike hata iwe ni mipya kabisa.

Idhaa ya Kiswahili 2004-08-25