Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-08-26 20:36:36    
Watoto wa mijini wafuatilia maendeleo ya watoto wa vijijini

cri

    Kwenye baraza la uchunguzi kuhusu hali ya maendeleo ya watoto nchini China lililofanyika tarehe 21 mjini Beijing, wawakilishi 32 kutoka Shanghai na Guangdong walibadilishana maoni na mapendekezo kuhusu namna ya kuboresha maisha na hali ya maendeleo ya watoto.

    Kituo cha Watoto cha China na Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa walianzisha kambi ya majira ya joto ya uchunguzi kuhusu hali ya maendeleo ya watoto nchini China ya mwaka 2004 katikati ya mwezi Julai hadi Agosti katika miji mitano ya Guangdong, Shanghai, Guizhou, Shanxi na Guangxi. Harakati hiyo imewapa nafasi watoto kushiriki moja kwa moja kwenye uchunguzi na tathmini kuhusu hali ya maendeleo ya watoto, na kuonesha vya kutosha haki ya watoto kushirikishwa iliyowekwa katika makubaliano ya haki za watoto. Watoto zaidi ya 500 kutoka miji na mikoa 12 wameshiriki kwenye harakati hiyo katika miaka mitatu iliyopita.

    Ofisa wa Kituo cha Watoto cha China Bw. Yang Jinghui alieleza kuwa, madhumuni ya harakati hiyo ni kuhimiza watoto kushiriki kwenye harakati ya uchunguzi na tathmini kuhusu hali ya maendeleo ya watoto, na kufanya watoto kujionea na kufahamu hali mbalimbali za watoto kama vile afya, elimu na hali ya mazingira ya watoto, na kulinganisha na hali zao wenyewe, na kuweka kumbukumbu na kueleza hisia zao kupitia uchoraji, picha, shajara na tasnifu.

    "Watu wanaohama kutoka kwenye Magenge Matatu walihamia huko Shanghai kutoka Sichuan, na kuishi kwenye kisiwa cha Chong Ming, watoto hao pia walisoma katika shule za kisiwa cha Chong Ming, na kupata marafiki wapya katika kisiwa hicho. Je, watoto wanazoea maisha ya huko?" Picha inayoitwa "Shauku ya maisha ugenini" iliyochorwa na mtoto mmoja ambaye alishiriki kwenye harakati hiyo unavutia sana watu: sura ya wasiwasi ya msichana mwenye mapambo ya kijadi imechorwa vizuri sana.

    Mtoto aliyeshiriki kwenye kambi hiyo Chen Yixiu alisema kwenye shajara yake kuwa,"Sasa nimefahamu maisha halisi ya kijijini na wakulima. Nisingeweza kufahamu hali ngumu ya kijijini bila kuishi pamoja na watu hao. Hali nilizojionea leo zimenishangaza sana. Tunapaswa kutumia kwa njia mwafaka mazingira ya maisha yetu, kujifunza moyo wa wanakijiji kufanya juhudi kubwa, tukikabiliwa na matatizo makubwa."

    Imefahamika kuwa, baraza la siku 4 ni hitimisho kwa harakati ya kambi ya majira ya joto, watoto walioshiriki kwenye harakati hiyo walionesha matokeo ya kambi mbalimbali kambi za majira ya watoto. Ikilinganishwa na hali ya maisha ya watoto wa mijini na vijijini, wanagundua kuwa kuna matatizo mbalimbali yanayoathiri maisha na maendeleo ya watoto, kama vile mazingira mabaya ya afya, kutozingatia afya na maadili kwa wanafunzi. Aidha, nyaya za umeme zilizowekwa karibu na barabara ni hatari sana kwa maisha ya watu. Vilevile watoto hao walioshiriki kwenye harakati hiyo walitoa mapendekezo yao, kama vile kuimarisha nguvu ya matangazo, kuongeza mawazo ya kulinda mazingira, kuhimiza wakulima kutumia gesi ya kinyesi, kubadilisha mawazo na kukamilisha mafunzo kwa uadilifu wa walimu. Pia idara zinazohusika za serikali zinapaswa kuimarisha usimamizi kwa klabu ya mtandao wa Internet.

Idhaa ya Kiswahili 2004-08-26