Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-08-31 18:17:17    
Upendo wa jamii wamwezesha mfugaji wa kabila la Wayi kusoma katika chuo kikuu cha Qinghua

cri

    Tarehe 18 Agosti ni siku ya kuandikisha wanafunzi wapya katika Chuo Kikuu cha Qinghua. Kijana Lersela wa kabila la Wayi kutoka mkoa wa Sichuan ni mmoja kati ya wanafunzi hao. Katikati ya mwezi uliopita, kijana Lersela alikuwa bado ana wasiwasi kuhusu ada kubwa ya yuan 7250 ya kusoma katika chuo kikuu. Baada ya wiki mbili tu kutokana na upendo wa jamii, amepata bahati ya kuwa mwanafunzi rasmi wa chuo kikuu hicho, ambacho ni chuo kikuu maarufu kabisa nchini China.

    Lersela anatoka katika tarafa inayojiendesha ya kabila la Wayi ya mkoa wa Sichuan. Familia yake ina nusu ekari tu za shamba, ambazo zinaweza kuwatosheleza kwa chakula tu. Kutokana na umaskini, Lersela wakati wa utoto wake hakukuwa na nguo za kutosha. Wakati wa majira ya baridi, alivaa nguo zile tu kwa majira yote, na wakati wa majira ya joto alivaa shati mchana na kulifua wakati usiku kwa ajili ya kulivaa siku ya pili. Ili kupunguza mzigo mzito wa nyumbani, Lersela alianza kuchunga mbuzi alipokuwa mdogo. Ilipofika umri wake wa kuingia shule ya msingi, baba yake alimwambia asiende shule abaki nyumbani kuwasaidia wazazi kuchunga mbuzi. Lersela alilia kwa muda mrefu, akimwomba baba yake ampeleke shule, na kuahidi kusoma kwa bidii.

    Alipokuwa shule ya msingi, siku zote Lersela alikuwa anakwenda shule bila viatu. Wakati wa majira ya baridi theluji inapoanguka, miguu yake ilikuwa inauma sana na hata kufikia kupasuka kutokana na ubaridi. Japokuwa alipaswa kuchunga mbuzi baada ya shule, lakini kila akipata kitabu chochote, alikuwa anajaribu kusoma maneno yote yaliyomo, hata maneno yaliyoandikwa kwenye makasha ya vibiriti aliyopata.

    Baada ya kumaliza masomo ya shule ya msingi, kijana Lersela alifaulu mtihani wa kuingia shule ya sekondari ya tarafa ya mji wa Xichan. Kwa sababu shule ya sekondari iko mbali na nyumbani kwake, wazazi wake walimnunulia viatu, ili kutunza viatu vyake visiharibike haraka, kila mara Lersela alikuwa akijaribu kutembea kwenye nyasi, mvua iliponyesha alivua viatu na kutembea peku huku akikumbatia viatu kifuani. Lersela alisema kuwa, japokuwa nyumbani kwao ni baridi sana, lakini haikuwahi kuvaa soksi hata siku moja.

    Umaskini umemfanya Lersela athamini zaidi nafasi ya masomo. Hivyo kila mara masomo yake yalitia fora katika shule yake. Miezi miwili na zaidi iliyopita, kijana Lersela alishiriki kwa imani kubwa mtihani wa kuingia chuo kikuu, na kupata mafanikio makubwa. Alichaguliwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Qinghua kwa kushika nafasi ya kwanza katika tarafa yake.

    Majirani na jamaa wanaofahamu hali ya umaskini ya familia yake waliposikia habari ya kuchaguliwa kwake kuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Quinghua, wote walikwenda nyumbani kwake kutoa mchango kadiri wawezavyo. Yuan moja au mbili ni hela kidogo sana, haitoshi kufanya jambo lolote, lakini haba na haba hujaza kibaba. Kutokana na juhudi za pamoja, zilikusanywa Yuan 4000. Na habari yake ilipofika Chengdu, mji mkuu wa mkoa wa Sichuan, wakazi wa Chengdu pia walimchangia zaidi ya Yuan 7000.

    Bibi mzee mwenye umri wa zaidi ya miaka 80 alikuja na yuan mia moja na zaidi alizolimbikiza kwa miaka kadhaa; Bwana mmoja na mke wake waliostaafu walimpelekea Lersela nguo, viatu na soksi; marubani kadhaa wa kampuni ya usafiri wa ndege za abiria ya Sichuan walipopata habari kuwa, ni vigumu kununua tikiti za gari moshi kwenda Beijing, waliwanunulia Lersela na wazazi wake tikiti za ndege.

    Kabla ya kuondoka Chengdu, Lersela alisema kuwa, alipata upendo mkubwa kutoka kwa wakazi wa Chengdu

Idhaa ya Kiswahili 2004-08-30