Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-09-01 16:38:30    
Chombo cha kuzuia utekaji nyara kwenye ndege

cri
    "Chombo kinachodhibiti kushuka kwa ndege kutoka mbali" (robolander) hapo awali kilitumika sana kwenye ndege za   upelelezi zisizo na rubani. Hivi sasa, watafiti wanajitahidi kutumia teknolojia hiyo katika ndege za abiria. Chombo hicho kinaweza kumwachia msimamizi wa udhibiti wa safari za ndege kuendesha ndege pindi inapotokea hali ya dharura na kudhibiti kushuka kwa ndege. Chombo hicho kinatumia teknolojia za aina nyingi za kisasa za kompyuta ikiwa ni pamoja na "mchakato wa kuzuia ndege kugonga kitu kingine". Kama rubani hatapokea maelekezo ya msimamizi wa safari za ndege, mchakato huo utaweza kuwasaidia wasimamizi wa safari za ndege walioko kwenye ardhi kuzuia rubani wa ndege kugonganisha ndege na majengo au milima.

    Gazeti la Sunday Times la Uingereza hivi karibuni liliripoti kuwa idara ya safari za chombo cha anga ya juu ya Marekani hivi karibuni ilifanya majaribio kwa kutumia ndege ya Boine 757 iliyowekewa chombo cha kudhibiti kutoka mbali kushuka kwa ndege, kwenye anga ya Washington, mji mkuu wa Marekani. Wakati ndege hiyo ilipojaribu kujigongesha kwenye Ikulu, software ya kampyuta iliizuia mara moja na kuilazimisha ndege kurudi mahali ilipotoka.

    Hivi sasa, wizara ya usalama wa nchi ya Marekani imetaka kampuni ya Boine kuweka lchombo hicho katika ndege zake mpya.

2004-09-01