Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-09-03 12:42:42    
Dini ya kibudha nchini China

cri

    Hapa nchini China, wachumba wawili wanapoachana, watu husema kuwa Ah, hao hawakuzaliwa na heri. Wachina wanaamini kwamba watu hukutana kwa bahati walizokuwa nazo katika dunia nyingine walipotoka. Vile vile wanaamini kuwa hisani yavuta heri na uovu huleta balaa, kwa hivyo watu wakifanya wema watalipiwa baraka na wakifanya uovu watapata nuksia. Maneno hayo yalitokana na mawazo ya dini ya kibudha, lakini yamekuwa maneno ya kawaida sana katika maisha ya wachina. Tunaweza kusema kuwa dini ya kibudha imeathiri kwa kina mila na desturi za wachina.

    Imetimia miaka elfu mbili sasa tangu dini ya kibudha ilipoanza kuenezwa nchini China. Dini ya Kibudha imetoa mchango mkubwa katika kuendeleza fikra na utamaduni wa China na dini ya kibudha imeshakuwa sehemu moja muhimu isiyotengeka katika utamaduni wa China. Hata hivyo, dini ya kibudha ilizaliwa katika nchi za nje. Vitabu vya historia vinaeleza kuwa katika karne ya pili kabla ya kristo, msufii mmoja wa kibudha aitwaye Yicun alileta nchini China misahafu ya dini ya kibudha kutoka India.

    Mwanzoni kabisa, dini ya kibudha ilienezwa miongoni mwa maofisa wa serikali au watu wa hali ya juu; na kisha ikaingia katika kipindi cha kutafsiri misahafu na kuiieneza. Na baada ya hapo, dini ya kibudha ikakomaa nchini China. Toka karne ya 6 hadi karne ya 8, dini ya kibudha ilikuwa imesitawishwa na kuimarishwa sana sana. Wakati huo, China ilikuwa mojawapo ya nchi zenye nguvu na neema duniani. Japan, Korea, Vietnam na nchi jirani nyingine ziliwatuma wanafunzi waje China kujifunza. Wanafunzi hao waliporudi pia waliieneza dini ya kibudha katika nchi zao.

    Baada ya karne ya 10, madhehebu mbali mbali ya dini ya kibudha ya China yalikuwa yamechomoza na kuanzia hapo hadi karne ya 19, dini ya kibudha ikaenea nchini kote.

    Katika miaka elfu mbili iliyopita, dini ya kibudha iliathiri kwa kina kirefu fasihi, uchoraji, muziki, ujenzi na fani nyingi nyingezo. Kwa mfano, katika Enzi ya Tang, utungaji wa riwaya uliathiriwa sana na dini ya kibudha. Dini ya kibudha hasa ilichangia sana sanaa ya uchoraji ya China. Tukitembelea mapango yenye michoro ya kale ya kutani huko Xingjiang na Gansu, tutaweza kuona kwamba michoro hiyo ya kutani ina mtindo safi wa dini ya kibudha. Toka karne ya 6 hadi karne ya 10, mtindo wa uchoraji wa dini ya kibudha ulikuwa umeota mzizi kabisa nchini China. Katika fani ya ujenzi, majengo mengi ya kale ya China yana mtindo wa ujenzi wa dini ya kibudha.

    Katika miaka elfu mbili iliyopita, dini ya kibudha ilipata kutukuzwa na kusitawishwa, na baadhi ya nyakati, nayo pia ilikumbwa na mateso, maana iliwahi kutukuzwa kuwa dini ya taifa na baadhi ya nyakati iliwahi kudidimia. Katika mwendo huo wa kujieneza, dini ya kibudha iligawanyika katika madhehebu matatu, nayo ni: dini ya kibudha ya Wahan, dini ya kibudha ya Tibet na dini ya kibudha ya kabila la watai huko mkoa wa Yunan. Katika seheme zile ambako wanakaa wahan, waumini wa dini ya kibudha ni wengi sana sana. Watu wa kawaida wanaamini dini ya kibudha, lakini hawana shughuli nyingi za kidini. Kati ya watu miliyoni 2 na laki 4 wa Tibet, waumini wa dini ya kibudha wamefikia asilimia 90. Sasa dini ya kibudha pamoja na dini ya kiislam, dini ya kikatholiki, dini ya kikristo na dini ya kitao ni dini kubwa tano za China, na waumini wao wanakaa kwa amani na kwa urafiki.

    Katiba ya China inaeleza waziwazi kwamba raia wa China wana uhuru wa kuamini dini. Naibu mkurugenzi wa chama cha dini ya kibudha cha China Bw. Jing Hui alisema kuwa sera za uhuru wa kuamini dini zinatekelezwa barabara hivi sasa nchini China. Yeye mwenywe anaridhika na sera hizo. Aliongeza kuwa China inaheshimu na inafuata sheria bila kutikisika. Sheria zilizotungwa na serikali zinaweza kuwalinda waumini wa dini.

    Msufii Jin Hui aliwaomba marafiki wa nchi za nje waelewe zaidi juu ya sera za dini za China na hali ilivyo ya dini ya kibudha ya China. Kwa ufupi, dini ya kibudha inaendelea vizuri nchini China.

    Msufii Jin Hui aliongeza kuwa dini ya kibudha ni dini ya kimataifa na ina waumini wengi sana sana katika nchi za Asia ya mashariki-kusini. Chama cha dini ya kibudha cha China kinajitahidi kuimarisha maingiliano yake na nchi za nje.

    Msufii Jing Hui alisema kuwa chama cha dini ya kibudha cha China pia kinawasiliana na dini zingine za nchi mbali mbali. China imejiunga na chama cha mawasiliano ya waumini wa dini ya kibudha cha kimataifa. Kila mwaka waumini wengi wanchi nyingine wanakuja China kwa matembezi na utalii na ilhali waumini wa China pia wanazitembelea nchi nyingine au kushiriki katika mikutano mbali mbali ya kimataifa.

Idhaa ya Kiswahili 2004-09-03