Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-09-03 12:52:17    
"Chumba Chekundu" Chashuhudia Mabadiliko Makubwa

cri
    Mjini Shanghai, wazee wengi wanaopenda chakula kitamu wanakumbuka kuwa, mkahawa wa chakula cha kimagharibi "chumba chekundu" ni mahali pa kutafuta ndoto; lakini kwa vijana wa leo, mkahawa huo ni mmoja tu kati ya mikahawa mingi iliyotapakaa mjini humo, ambayo inawawezesha watu kupata chakula kitamu.

    Nchini China, watu wa Shanghai ni watu wanaopenda na kujua zaidi kufuata wakati na kupokea mambo mapya. Mwaka 1842, China ilishindwa katika vita vya kasumba kati ya China na Uingereza. Matokeo hayo yaliulazimisha mji wa Shanghai "kufungua mlango", hivyo wakaingia wavamizi, wafanya-biashara na mikahawa ya chakula cha kimagharibi. Baadaye, mikahawa mbalimbali ya chakula cha kimagharibi ilianzishwa katika "sehemu zilizokodishwa" mjini Shanghai wakati huo. Miongoni mwake, "CHEZ ROVERE" (baadaye ulioitwa mkahawa wa chakula cha kimagharibi "chumba chekundu") ulioendeshwa na Wafaransa ulikuwa ni maarufu sana, na ulikuwa sehemu waliyokusanyika watu mashuhuri wa China na wanaotoka ng'ambo. Wakati huo, watu waliokwenda "chumba chekundu" kula chakula cha kimagharibi walikuwa watu wenye hadhi maalum na heshima kubwa, hivyo watu wachache tu walikuwa wanaweza kwenda kwenye mkahawa huo kula chakula.

    Mwaka 1978, Mmarekani Pariki kwa mara ya kwanza alifika Shanghai akiwa balozi mdogo wa Marekani mjini Shanghai. Alikumbusha kuwa, wakati huo, mjini Shanghai kulikuwa na wageni kumi kadhaa tu kutoka nchi za nje.

    Bwana Pariki alisema, "Wakati huo mjini Shanghai hakukuwa na barabara ya mwendo kasi wala uwanja wa ndege wa kimataifa ulio wa kisasa, hata hakukuwa na taa na zana za burudani kwenye sehemu ya Waitan iliyoko kando ya mto Huangpu, ambapo wageni kutoka nchi za nje walikuwa wakiwaburudisha wakazi wa Shanghai, kila walipojitokeza wapita njia wengi walisimama na kuwakodolea macho kwani kwao wageni walikuwa ni watu wa ajabu.

    Baada ya sera ya mageuzi na ufunguaji mlango kutekelezwa mjini Shanghai, hasa baada ya kuingia miaka ya 90 ya karne iliyopita, Shanghai ilianza kuwapokea wageni na kupokea utamaduni mbalimbali wa aina tofauti kutoka nchi za nje.

    Shanghai ya leo imeonekana kuwa na sura ya mji mkubwa wa kimataifa. Hivi sasa mjini Shanghai kuna kampuni zaidi ya elfu 24 zilizowekezwa na wafanyabiashara wa nchi za nje; wageni wanaoishi kwa muda mrefu mjini humo wamefikia 100,000, na watalii wa nje wanaofika mjini Shanghai ni zaidi ya milioni 3 kwa mwaka, kufanya kazi pamoja na wageni ni jambo la kawaida kwa wakazi wa Shanghai.

    Bw. Pakiri alisema, hivi sasa wageni wengi kutoka nchi za nje wanaishi kwenye mitaa mbalimbali mjini Shanghai ambapo wanaishi pamoja na wakazi wa huko katika hali ya kirafiki. Kila wakienda barabarani hawawezi kuwashangaza tena wakazi wa mji wa Shanghai, wageni kutoka nchi mbalimbali wamekuwa ni sehemu moja ya wakazi wa Shanghai.

    Bwana Pakiri alisema: "Kuanzia mwaka 1978, mabadiliko makubwa zaidi kuliko yale ya miji yo yote mingine duniani yalitokea katika ujenzi wa miundo mbinu mjini Shanghai, ambapo Washanghai na wachina wote wamebadilika kuwa na mawazo mapya na wanapenda kuwapokea wageni kutoka nchi mbalimbali duniani, ili kufundishana.

    Hivi sasa mjini Shanghai, kuna mikahawa mingi ya chakula cha mapishi tofauti ya hapa nchini na hata ya nchi mbalimbali za nje.

    Mwuzaji chakula wa Marekani Bw. Robester alisema, kabla ya kuja China hakutegemea mikahawa mingi ya aina mbalimbali mjini Shanghai. Na mikahawa maarufu ya chakula cha kimagharibi mjini humo hujaa wateja wengi wachina. Mkahawa wa chakula cha kimagharibi "Chumba chekundu" umekuwa mmoja tu miongoni mwa mikahawa mingi, hayo yameonesha mabadiliko makubwa yaliyotokea katika usitawi wa shughuli za mikahawa mjini Shanghai.

Idhaa ya Kiswahili 2004-09-03