Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-09-07 18:16:50    
Mambo ya kidiplomasia ya China inayoshikilia nia ya amani na kanuni za kujitawala na kujiamulia mambo (Sehemu A)

cri

    Leo tunawaletea makala ya nne yaani makala ya mwisho ya chemsha bongo kuhusu ujuzi wa Miaka 55 ya China mpya. Leo tunawafahamisha hali ya jumla kuhusu Mambo ya kidiplomasia ya China na mawasiliano kati ya China na nchi mbalimbali duniani.

    kuanzishwa kwa Jamhuri ya watu wa China mwaka 1949 kulikomesha historia ndefu ya uvamizi na kukandamizwa na nchi za nje kwa taifa la China. Tangu hapo China ilifuata njia ya kujitawala na kujiamulia mambo na kuanzisha uhusiano wa amani na kirafiki na nchi mbalimbali duniani.

    Tokea siku ya kuzaliwa kwa China mpya, China ilianza kushikilia sera ya kidiplomasia ya amani ya kujitawala na kujiamulia mambo katika kuendeleza uhusiano na nchi nyingine duniani. Zaidi ya miaka 50 iliyopita, sera hiyo ya kidiplomasia ya China haijabadilika hata kidogo bila kujali mabadiliko ya namna gani yaliyotokea duniani.

    Mwaka 1954, yaani kabla ya miaka 50 iliyopita China, India na Burma (yaani Myanmar ya hivi sasa) zilitetea kwa pamoja kanuni tano za kuishi pamoja kwa amani kuhusu kuheshimu mamlaka ya nchi na ukamilifu wa ardhi; kutoshambuliana; kutoingilia mambo ya ndani; kuwa na usawa na kunufaishana; na kuishi pamoja kwa amani. Kanuni hizo tano ni ufafanuzi kamili zaidi kuhusu sera ya kidiplomasia ya amani ya kujitawala na kujiamulia mambo ya China mpya.

    Kanuni hizo zimekuwa kanuni za kimsingi zinazotambuliwa duniani siku hadi siku katika kushughulikia uhusiano kati ya nchi na nchi. Kutokana na msingi wa kanuni hizo tano, China na nchi 165 duniani zimewekeana uhusiano wa kibalozi, na imeanzisha mawasiliano na ushirikiano karibu na nchi na sehemu zote duniani katika nyanja za uchumi na biashara, sayansi na teknolojia, na utamaduni.

    "Amani na maendeleo ni masuala mawili makubwa ya zama hivi", huu ni uchambuzi wa kimsingi kabisa wa China kuhusu hali ya dunia ya sasa. Ilipoingia katika karne ya 21, ingawa mabadiliko makubwa na yenye utatanishi yalitokea katika hali ya dunia, lakini uchambuzi huo wa China bado haujabadilika.

    Kuhusu mambo ya kidiplomasia, China inatetea kuuwezesha uhusiano wa kimataifa kuwa wa kidemokrasia, kupinga umwamba na siasa za kimabavu. China inatetea kuwa nchi kubwa au ndogo, yenye nguvu au dhaifu, zote ziwe sawa katika kushiriki mambo ya kimataifa. Kuhusu kutatua migogoro ya kimataifa, China siku zote inatetea kufanya mazungumzo badala ya mapambano, kupinga matumizi ya nguvu au kutishia kutumia nguvu; kuhusu ustaarabu tofauti wa aina mbalimbali wa binadamu, China inatetea kuhifadhi aina mbalimbali za ustaarabu wa binadamu, na kutetea kuwa na aina tofauti za ustaarabu na mifumo tofauti ya jamii duniani, pamoja na njia za maendeleo za nchi mbalimbali, zote zinapaswa kuheshimiwa ili kupata maendeleo kwa pamoja katika hali ya kutafuta maoni ya pamoja na kuweka kando maoni tofauti.

    Katika miaka ya hivi karibuni, shughuli za ugaidi zimekuwa zikipamba moto siku hadi siku. Suala la usalama linafuatiliwa na nchi nyingi zaidi na wananchi wake. Kuhusu suala la usalama, China siku zote inatetea kupinga ugaidi na kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya ugaidi duniani; wakati huo huo, China inatetea kuwa na wazo jipya kuhusu usalama, kuwa na mawazo ya kuaminiana ili kupata usalama, kufanya mazungumzo ili kuhimiza usalama, na kupinga kutumia vigezo viwili katika mapambano dhidi ya ugaidi; China inaona kuwa, mapambano ya kijeshi hayawezi kuleta usalama wa kudumu, China inapinga vitendo vya kushambulia mamlaka ya nchi nyingine kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi, na kupinga kuhusisha mapambano dhidi ya ugaidi na mataifa fulani au dini fulani.

    Hadhi ya Umoja wa Mataifa pia ni suala ambalo limekuwa likifuatiliwa na jumuiya ya kimataifa katika miaka ya hivi karibuni. Kuhusu suala hilo, China inatetea kulinda heshima ya Umoja wa Mataifa na kulinda hadhi ya maamuzi ya Umoja wa Mataifa katika kushughulikia masuala makubwa ya kimataifa, na pia inatetea kuheshimu sheria za kimataifa na kanuni za kimsingi za uhusiano wa kimataifa zinazotambuliwa duniani kote.

    Kwa mfano kuhusu suala la Iraq, China siku zote inashikilia kuwa lazima kutafuta ufumbuzi wa kisiasa ndani ya Umoja wa Mataifa, na kupinga kuanzisha vita dhidi ya Iraq bila idhini ya Umoja wa Mataifa. Na kuhusu suala la mageuzi ya Umoja wa Mataifa, China ikiwa ni mmoja wa wajumbe watano wa kudumu wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, inaunga mkono Umoja wa Mataifa kufanyiwa mageuzi, na kuunga mkono upanuzi wa baraza la usalama na kuongeza idadi ya wajumbe wa kudumu wa baraza hilo.

    Kuhusu masuala mengine makubwa ya kimataifa, China inatetea kuwa utandawazi wa uchumi wa dunia unapaswa kuwa wenye manufaa kwa nchi zote, na nchi zilizoendelea zinapaswa kuwajibika zaidi katika kuondoa umaskini na kuboresha mazingira.

Idhaa ya Kiswahili 2004-09-07