Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-09-07 18:20:23    
Mambo ya kidiplomasia ya China inayoshikilia nia ya amani na kanuni za kujitawala na kujiamulia mambo
(Sehemu B)

cri
    sasa tayari tumewafahamisha sera na utetezi wa kidiplomasia wa China, sasa tunapenda kuwafahamisha kuhusu hali ya mawasiliano kati ya China na nchi mbalimbali duniani.

    China ni nchi kubwa zaidi kuliko nchi nyingine zote zinazoendelea duniani. Kuimarisha mshikamano na ushirikiano na nchi nyingi zinazoendelea ni msingi wa sera ya kidiplomasia ya China. China na nchi nyingi zinazoendelea za Asia, Afrika na Latin Amerika zilikumbwa na ajali za kihistoria zinazofanana, na pia zina lengo la pamoja la kulinda uhuru wa nchi na kutimiza maendeleo ya uchumi.

    China ikiwa nchi pekee inayoendelea iliyo mjumbe wa kudumu wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, katika miaka mingi iliyopita imefanya juhudi kubwa za mwakilishi wa nchi zinazoendelea katika Umoja wa Mataifa, na imetoa mchango kwa ajili ya kulinda haki na maslahi ya halali ya nchi zinazoendelea.

    Bara la Afrika ni bara kubwa lenye nchi nyingi zaidi zinazoendelea. China inatilia maanani sana kuendeleza uhusiano na nchi za Afrika, kushikilia kuendeleza kwa kina ushirikiano kati ya China na Afrika katika nyanja zote kwa msingi wa kanuni za kuwa na usawa na kunufaishana, kutafuta ufanisi halisi wa maendeleo ya aina mbalimbali ili kupata maendeleo ya pamoja. Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika lililoanzishwa mwaka 2000 limekuwa utaratibu muhimu wa kufanya mashauriano ya kirafiki na kusukuma mbele ushirikiano wa kunufaishana kati ya China na nchi za Afrika.

    China ni moja ya nchi yenye majirani wengi zaidi duniani. China inashikilia sera ya ujirani mwema, kujenga mazingira ya usalama na kutimiza maendeleo ya pamoja na nchi jirani. Naibu mkurugenzi wa idara ya Asia katika wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Fu Ying alisema:

    China inataka kudumisha ujirani mwema ili kushirikiana na nchi jirani zake katika kujenga mazingira ya urafiki, amani, utulivu, na kujitahidi kupata maendeleo na usitawi wa pamoja.

    China vilevile inatilia maanani sana kuendeleza uhusiano na nchi zilizoendelea, inatetea kuwa nchi na nchi zinapaswa kutojali tofauti za mifumo ya jamii na itikadi, kuheshimiana, kutafuta maoni ya pamoja wakati wa kuweka kando migongano, ili kupanua ushirikiano wa kunufaishana.

    China pia inatoa mchango mkubwa katika kutatua matatizo makubwa ya kikanda. Kwa mfano, ili kusukuma mbele utatuzi wa kiamani suala la nyuklia la peninsula ya Korea, China imehimiza mara kwa mara kufanyika kwa mazungumzo ya amani ya pande mbalimbali, na kusukuma mbele kuanzishwa kwa utaratibu wa mazungumzo ya pande 6 ya Beijing, kazi hiyo ya China ilisifiwa na pande mbalimbali zinazohusika. Waziri wa mambo ya nje wa China Bwana Li Zhaoxing alipotoa hotuba alisisitiza kuwa, China itafuata daima njia ya maendeleo ya amani, alisema:

    Umaalum mkubwa wa maendeleo ya China ni maendeleo ya amani. Njia yetu ya maendeleo ni njia ya kulinda amani ya dunia, kushiriki kwa juhudi katika ushirikiano wa usawa na kunufaishana na kusukuma mbele maendeleo ya pamoja. Maendeleo ya amani ya China yataleta fursa kwa nchi jirani na dunia nzima.

    mpaka hapo ndiyo tumekamilisha matangazo ya makala ya nne yaani makala ya mwisho ya chemsha bongo kuhusu ujuzi wa miaka 55 ya China mpya. Sasa tunatoa maswali mawili.

    Swali la kwanza: Mpaka sasa China ina uhusiano wa kibalozi na nchi ngapi duniani?

    Swali la pili: Sera ya kidiplomasia ya China inahusu nini? Katika swali hili mnaweza kueleza kutokana na jinsi mlivyosikia matangazo yetu.

    Na tutarudia matangazo ya makala 4 za chemsha bongo kuhusu ujuzi wa miaka 55 ya China mpya kuanzia tarehe 26 mwezi Septemba katika kipindi hiki cha sanduku la barua. Makala hizo nne zimekwishawekwa kwenye tovuti yetu ya kiswahili katika kipindi cha sanduku la barua, karibuni mtembelee tovuti yetu. Msisahau anuani yetu ni www.cri.cn. chagua kiswahili.

Idhaa ya Kiswahili 2004-09-07