Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-09-07 19:07:23    
Mazungumzo ya nane ya uwekezaji na biashara kuwa ya kimataifa na kuhimizana

cri

     Mazungumzo ya nane ya kimataifa ya uwekezaji na biashara yatafanyika tarehe 8 mwezi Septemba mwaka huu katika mji wa Xiamen kutokana na mpango uliowekwa hapo awali. Mazungumzo hayo, ambayo ni mkutano mkubwa wa kimataifa wa kuhimiza uwekezaji ulioandaliwa na wizara ya biashara ya China, yamefanyika mara saba, na kila mara mashirika mengi ya hapa nchini na ya nchi za nje yalishiriki.

    Mazungumzo ya uwekezaji na biashara wa China yalianzishwa mwaka 1997. Mpaka mazungumzo yaliyopita yalipofanyika, jumla ya mikataba ya miradi zaidi ya elfu 14 ya mitaji ya nchi za kigeni yenye thamani ya dola za kimarekani karibu bilioni 70 imesainiwa. kuhusu mazungumzo ya nane, kiongozi wa ofisi ya uratibu aliye naibu meya wa mji wa Xiamen bibi Huang Ling hivi karibuni alipohojiwa na mwandishi wetu alisema kuwa mazungumzo ya safari hii yatakuwa ya kimataifa zaidi na ya kuhimizana, na watatoa uwanja kwa ajili ya mazungumzo ya uwekezaji na biashara kati ya wafanyabiashara wa China na wa nchi za kigeni. Alisema,

    "Shughuli muhimu za mazungumzo ya uwekezaji na biashara ya mwaka huu, licha ya mazungumzo, kutakuwa na mihadhara kuhusu uwekezaji na sherehe ya ufunguaji wa mkutano. Safari hii kampuni ya Hitachi ya Japan itapeleka wajumbe zaidi ya 100, ambayo inakadiriwa kuwa ni ya kwanza kwa wingi wa idadi ya wajumbe watakaoshiriki. Hivi sasa, kampuni ya Hitachi imeagiza sehemu 55 za maonesho zenye eneo la karibu mita za mraba 500. Wafanyabiashara wa kampuni ya Japan nchini China wamesema kuwa hii ni mara ya kwanza kwa kampuni ya Hitachi kushiriki kwenye mazungumzo ya uwekezaji na biashara, ikitarajia kuwafahamisha zaidi washiriki wa mazungumzo bidhaa za kampuni hiyo na nguvu ya teknolojia yao ya hivi sasa. Habari zinasema kuwa hivi sasa kampuni maarufu za kimataifa zilizooneshwa nia ya kutaka kwenye mazungumzo ya uwekezaji na biashara ya China ni pamoja na kampuni za Kodak ya Marekani na Volvo ya Sweden.

    Tangu kuanzishwa mazungumzo ya uwekezaji na biashara ya China, wizara ya biashara ya China ambayo ni mwenyeji, ilitathmini uzoefu wake katika mazungumzo yaliyopita, ili kufanya mazungumzo hayo kuwa mazuri zaidi mwaka hadi mwaka. Habari zinasema kuwa mazungumzo ya mwaka huu yamepiga hatua kubwa kuliko yale ya zamani, na kuelekea kuwa ya kimataifa zaidi na yenye kiwango cha juu cha utaalamu. Kiongozi wa ofisi ya mkutano, bibi Huang Ling alisema,

    "Mazungumzo ya 8 ya kimataifa ya uwekezaji na biashara yatakuwa ya kimataifa zaidi, ambayo idadi ya nchi na sehemu zitakazoshiriki itakuwa kubwa zaidi, na maonesho ya kampuni za nchi za nje yatakuwa ya kiwango cha juu zaidi."

    Wizara ya biashara ya China imesema kuwa licha ya mkutano wa maendeleo ya biashara wa Umoja wa Mataifa na mashirika ya kuhimiza uwekezaji duniani kushiriki na kutoa msaada katika maandalizi ya mazungumzo, safari hii kuna jumuiya za kiuchumi duniani zikiwemo jumuiya ya maendeleo ya viwanda ya umoja wa mataifa na shirika la mambo ya fedha duniani, ambazo zimetoa msaada katika maandalizi ya mazungumzo hayo. Aidha, nchi nyingi zimeeleza kutarajia kuwa na siku ya maonesho ya nchi yake katika kipindi cha mazungumzo ya safari hii ili kuonesha sura ya nchi yake kwa wajumbe, mazingira na miradi ya uwekezaji.

    Hali maalumu nyingine ya mazungumzo hayo ni ya kuhimizana. Licha ya kufuata desturi ya zamani ya kuvutia kampuni za kimataifa zije kushiriki kwenye mazungumzo ya biashara na kuwekeza nchini China, itahimiza kampuni za China kuwekeza katika nchi za nje. Mkurugenzi wa kituo cha kuhimiza uwekezaji wa kimataifa, Bw. Huang Heming alisema,

    "Katika mazungumzo hayo, tutazihimiza kampuni za China kujenga miradi katika nchi za nje ili kuhimiza ushirikiano wa kimataifa duniani na kuhimiza kampuni za China kushiriki kwenye ushindani wa kimataifa. Katika siku za baadaye, licha ya kuvutia kampuni za kigeni kuwekeza nchini China, vilevile tutahimiza kampuni za China kuwekeza katika nchi za nje."

     Habari zinasema kuwa katika muda wa mazungumzo ya uwekezaji ya safari hii, wizara ya biashara ya China itafanya semina zaidi ya 10 kuhusu masuala makubwa mawili ya kuvutia kampuni za nchi za nje kuwekeza nchini China na kuzihamasisha kampuni za China kuwekeza katika nchi za nje. Hivi sasa kuna nchi za Marekani, Japan, Uingereza, Ufaransa, Italia na Singapore, ambazo zimejiandikisha kushiriki kwenye mazungumzo ya kuwekeza nchini China. Mazungumzo kuhusu kampuni za China kuwekeza katika nchi za nje, yanafuatiliwa na serikali na miundo ya kuhimiza uwekezaji ya nchi za nje na sehemu zaidi ya 60 duniani.

     Ili kuongeza ufanisi wa kuhimizana katika mazungumzo ya uwekezaji ya safari hii, wizara ya biashara ya China imejitahidi kuinua kiwango cha upashanaji habari na usimamizi. Kiongozi wa ofisi ya mazungumzo ya uwekezaji, bibi Huang Ling alisema, "Mwaka huu tutainua kiwango cha usimamizi na huduma ya upashanaji habari. Lengo la mazungumzo hayo ni kufanya usimamizi na shughuli za uratibu kufikia kiwango cha kisasa na kulingana na kiwango cha kimataifa.

     Habari zinasema kuwa wizara ya biashara ya China, hivi sasa imeboresha mfumo wa kujiandikisha wafanyabiashara wa nchi za nje na kutafuta kampuni za kushirikiana. Mbali na hayo, mji wa Xiamen ambako mazungumzo ya safari yatafanyika, umezindua harakati za mazungumzo zikiwa ni pamoja na mawasiliano, huduma na usalama ili kufanikisha mazungumzo ya nane ya kimataifa ya uwekezaji na biashara ya China.

Idhaa ya Kiswahili 2004-09-07