Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-09-08 20:30:24    
Mlima Wutai

cri

    Mlima Wutai uliopo katika Jimbo la Shanxi ni mmojawapo kati ya milima minne inayojulikana kwa utamaduni wa dini ya Buda. Miaka 5 iliyopita, mahekalu ya Mlima Wutai yaliteuliwa kuwa maudhui ya kusanifu stempu. Kuanzia hapo, msanifu Yan Bingwu alipania kuyaonyesha mahekalu ya Mlima Wutai kwenye stempu.

    Ili kutimiza lengo lake, Yan alitembelea Mlima Wutai zaidi ya mara 10, na kufanya uchunguzi kwa bidii kutoka kwa wataalamu wahusika. Mwishowe, kutokana na msaada wa mwalimu wake, Yan alifanikiwa kusanifu stempu 6 za mandhari ya mahekalu yote ya Mlima Wutai.

    Mlima Wutai pia unaitwa Mlima Baridi. Msanifu anaona kuwa neno la baridi linadhihirisha hali ya maumbile ya Mlima Wutai, vilevile linahusiana na nia ya dini ya Buda ya kutuliza moyo na kuwaokoa binadamu.

    Wakati aliposanifu rangi ya msingi, aliunganisha ufundi wa jadi wa China na wa kisasa wa Kizungu. Katika kuchora mahekalu, ameonyesha vizuri uzuri wa mandhari ya maumbile, lakini juu ya msingi wa kuonyesha ukweli alipiga chuku, aliongeza au kufuta mandahri fulani ili kila stempu iwe na ujumbe wake maalumu. Kwa mfano, katika stempu ya "Kundi la Mahekalu huko Tarafa ya Taihuai", mnara mweupe ni mdogo katika mandhari halisi, lakini msanifu aliugeuza kuwa mkubwa katika stempu, pia aliipeleka mandhari ya nyuma mbali zaidi. Mfano mwingine ni "Kilele cha Bodhisattva", mandhari yanaonekana wakati kunapoanza kutanduka baada ya kuanguka theluji, wakati huu msanifu aliongeza mawingu na ukungu mbinguni, kwa hivyo kilele hicho kinaonekana kama kiko katika pepo ya dola la Buda.

    Baada ya kutolewa, stempu hizo zilipewa hongera na wahakiki. Walisema kuwa stempu hizo zimemithilisha vizuri sifa za ujenzi wa mahekalu; utumiaji wa rangi ni uvumbuzi mpya; stempu hizo zinastahiki kupewa pongezi.