Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-09-09 20:33:38    
Miaka 100 ya China kufaulu kuingiza miti ya mpira asili kutoka nchi za nje

cri

    Hivi sasa, China imekuwa nchi kubwa ya kwanza duniani inayotumia na kuagiza mpira asili kutoka nchi za nje. Kutokana na maendeleo ya shughuli za mpira, kiasi cha kujitosheleza katika mpira nchini China kimefikia asilimia 32.

    Mpira asili, makaa ya mawe, chuma na chuma cha pua na mafuta zimekuwa nyenzo nne muhimu kwa viwanda, na kati ya nyenzo hizo mpira asili ni nyenzo asili pekee inayoweza kuzalishwa tena. Alasiri ya tarehe 6, wafanyakazi wa mpira wa Beijing, mkoa wa Hainan na Yunnan na wajumbe kutoka Thailand na Malaysia nchi zinazozalisha mpira walikutana mjini Kunming kuadhimisha miaka 100 ya kuanzisha juhudi za kuendeleza zao la mpira asili nchini China.

    Mwaka 1904, chifu wa kabila la Wadai wilayani Yingjiang, Yunnan Bw. Dao Anren alifaulu kuagiza miti ya mpira asili kutoka Singapore na kuipanda katika mlima wa wilaya hiyo kuanzia mwishoni mwa mwezi Agosti hadi mwanzoni mwa mwezi Septemba mwaka huo. Hivyo Yunnan imekuwa chimbuko la mpira asili nchini China.

    Mpira asili duniani umekuwa na historia ya miaka 128 tangu mwaka 1876 ulipopandwa na binadamu kwa mara ya kwanza. Miti ya mpira asili iko kwenye eneo la bonde la mto Amazon karibu na Ikweta, barani Amerika ya Kusini. Maeneo ya kaskazini mwa nyuzi 15 ya latitudo na kusini mwa nyuzi 10 ya latitudo si maeneo asili ya kupanda miti ya mpira. Lakini baada ya wafanyakazi wa vizazi kadhaa wa China kufanya jitihada kubwa na uvumbuzi wa kisayansi, walifaulu kupanda miti hiyo katika eneo kubwa la Hainan, Yunnan na Guangdong lililoko kati ya nyuzi 18 hadi nyuzi 24 ya latitudo ya kaskazini. China imekuwa na mfumo wa teknolojia wa kupanda miti ya mpira unaoambatana na mazingira ya eneo la joto nchini China na kutoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya shughuli mpira asili duniani.

    Kwa zaidi ya miaka 50 iliyopita, China imezalisha tani milioni 8 za mpira asili. Hadi mwaka 2003, eneo lililopandwa miti ya mpira nchini China lilifikia hekta laki 6 na elfu 61 na kiasi cha uzalishaji wa mpira uliokauka kimefikia tani laki 5 na elfu 65 kwa mwaka, eneo na kiasi hicho linachukua nafasi ya tano duniani. China imekuwa nchi kubwa inayozalisha mpira duniani kutoka nchi maskini ambayo ilikuwa inazalisha mpira katika kipindi cha mwanzo cha kupata ukombozi na kuwa nchi kubwa ya kwanza inayotumia na kuagiza mpira asili kutoka nje duniani.

    Mkoa wa Yunnan ulioko kusini magharibi ya China umekuwa kituo bora kabisa cha kuzalisha mpira asili duniani. Eneo lililopandwa miti ya mpira asili mkoani humo ni hekta laki 2.4, linalozalisha tani laki 2.2 za mpira uliokauka kwa mwaka, kiasi ambacho ni theluthi moja ya mpira unaozalishwa nchini China, na kiasi cha uzalishaji wa mpira asili uliokauka ni tani 1.8 kwa hekta na kufikia kiwango cha juu duniani. Katika mashamba ya Xishuangbanna mkoani humo, kiasi cha kuzalisha mpira asili uliokauka kilichukua nafasi ya kwanza duniani kwa miaka 9 mfululizo. Eneo hilo lina hekta elfu 54 za mashamba yanayozalisha mpira asili na kiasi cha uzalishaji wa mpira asili uliokauka kimefikia tani 2 na kuzidi kile cha dunia cha kilo 905 kwa kilo 1155.

Idhaa ya Kiswahili 2004-09-09