Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-09-10 20:55:42    
Matukio makubwa ya mashambulizi ya kigaidi duniani yaliyotokea tangu "9.11" (Sehemu A)

cri

    Tarehe 11 mwezi Septemba mwaka 2001, ndege 4 za abiria za Marekani zilitekwa nyara na magaidi. Miongoni mwa ndege hizo, ndege 2 ziligonga majengo ya kituo cha biashara duniani mjini NewYork, na minara miwili ikaporomoka, ndege moja iligonga jengo la wizara ya ulinzi ya Marekani lililoko karibu na mji wa Washington, na nyingine ilianguka karibu na mji wa Pittsburgh kwenye jimbo la Pennsylvania. Mfululizo wa matukio hayo ya mashambulizi ya kigaidi umesababisha vifo vya watu zaidi ya 3000.

Mwaka 2002

Tarehe 12 mwezi Oktoba, sehemu ya utalii nchini Indonesia kwenye kisiwa cha Benoa kulitokea mfululizo wa milipuko ya mabomu dhidi ya wageni, na kusababisha vifo vya watu 202, na wengine 330 kujeruhiwa.

Tarehe 23 mwezi Oktoba, kulitokea tukio la utekaji nyara liliofanywa na watu wenye silaha wa Chechenya kwenye jumba la maonesho ya utamaduni kwenye kiwanda cha vipuri nchini Russia, na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 120.

Mwaka 2003

Tarehe 12 na 14 mwezi Mei, kulitokea malipuko kwa nyakati mbalimbali ndani ya Jumba la serikali ya sehemu ya Nadterechnaya na sehemu ya Ossetia za Chechnya nchini Russia, na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 70 na wengine 200 kujeruhiwa.

Tarehe 16 mwezi Mei, mji mkuu wa kiuchumi wa Morocco Casablanca kulikumbwa na mfululizo wa milipuko mitano ya kigaidi, na kusababisha vifo vya watu 41.

Tarehe 1 mwezi August, hospitali moja ya jeshi mjini Mozdok nchini Jamhuri ya ya Ossetia ya Kaskazini ya Russia ilishambuliwa kwa mabomu ya magari, na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 50 na wengine 80 kujeruhiwa.

Tarehe 19 mwezi August, kulitokea malipuko dhidi ya ofisi ya Umoja wa Mataifa iliyoko nchini Iraq huko Baghdad mji mkuu wa Iraq, na kusababisha vifo vya watu 24 na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa. Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa aliyeshughulikia mambo ya Iraq Bw. Sergio Vieira de Mello alipoteza maisha katika tukio hilo.

Tarehe 25 mwezi August, mji mkubwa kabisa wa fedha na biashara wa India Bombay ulikumbwa na milipuko miwili ya mabomu, na kusababisha vifo vya watu 52 na wengine 167 kujeruhiwa.

Tarehe 29 mwezi Agosti, milipuko ya mabomu katika magari ilitokea kwenye msikiti wa Ali uliopo kwenye mji wa Najaf, kusini mwa Iraq, ambao ni mji mtakatifu wa madhehebu ya shia, na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 100 na wengine zaidi ya 200 kujeruhiwa. Ayatolla Hakimu wa madhehebu ya shia aliuawa katika milipuko hiyo.

Tarehe 27 mwezi Oktoba, makao makuu ya tawi la kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu nchini Iraq yaliyopo katikati ya mji wa Baghdad na vituo vya askari polisi vya mitaa ya mashariki, kusini, magharibi na kaskazini vimeshambuliwa kwa mabomu ya kujiua yaliyokuwa kwenye magari, na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 35 na wengine zaidi ya 200 kujeruhiwa.

Tarehe 15 mwezi Novemba, masinagogi mawili ya wayahudi mjini Istanbul, nchini Uturuki, yalishambuliwa kwa mabomu yaliyokuwa kwenye magari, watu 25 waliuawa na wengine zaidi ya 300 kujeruhiwa katika shambulio hilo.

Idhaa ya Kiswahili 2004-09-10