Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-09-14 15:52:27    
Barua za wasikilizaji 0914

cri
    Katika wiki zilizopita, kutokana na kusoma makala maalum za chemsha bongo kuhusu ujuzi wa miaka 55 ya China mpya, hatukuweza kuwasomea barua tulizopokea kutoka kwa wasikilizaji wetu, tunadhani wasikilizaji wetu wanaweza kutuelewa.

    Kweli katika wiki zilizopita, kulikuwa na mashindano ya michezo ya Athens yaliyofanyika katika hali ya motomoto, na pia China ilikuwa ikiladhimisha miaka 100 ya kuzaliwa kwa kiongozi wa China marehemu Deng Xiaoping. Tulikuwa katika pilikapilika za kutafsiri na kutangaza, tunapenda kubadilishana maoni na wasikilizaji wetu kuhusu mikasa hiyo mikubwa. Sasa tunawaletea barua tulizopokewa kutoka kwa wasikilizaji wetu.

    Msikilizaji wetu Mbarouk Msabah wa sanduku la posta 52483 Dubai, Emirates ametuletea barua akisema kuwa, anapenda kutoa shukrani zake za dhati kwa Redio China Kimataifa kwa kunitumia post cards mbali mbali ambazo zina picha nzuri za wanyama mbali mbali ambao wapo hatarini kutoweka nchini China.

    Anasema kwa kweli post cards hizo za kuvutia zinaonesha jinsi ya Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China inavyothamini umuhimu wa kuhifadhi na kulinda wanyama "adimu" nchini humo ambao wanahitaji kuenziwa na kukingwa kwa uangalifu mkubwa, kabla hawajatoweka kabisa na kubakia historia tu ndani ya vitabu.

    Anasema amevutiwa sana na wanyama hao kama vile "Chui wa Siberian" au "Chui wa Manchurian"ambao inaaminika idadi yake haizidi zaidi ya 12 hadi 16 tu!!! Katika mbuga kote nchini China na kuwafanya wanyama hao kua ni adimu kabisa nchini China hata kuliko Panda wakubwa wa China, jambo ambalo limewaorodhesha "chui wa Manchurian" kuwa ni miongoni mwa wanyama 10 muhimu kabisa waliomo hatarini kutoweka hapa duniani.

    Anasema "Chui wa Manchurian" ambae kwa wenyeji wa maeneo wanakoishi nchini China huitwa "Mfalme wa milimani" ni moja kati ya wanyama wenye kusisimua sana ulimwenguni kwa vile ni wanyama wa aina yake wenye uhimu wa kipekee.

    Anasema hata kwake barani Afrika ambako kumekuwepo na maeneo makubwa kabisa ulimwenguni yenye mbuga za wanyama kama vile, Mbuga ya Taifa ya Wanyama ya Serengeti yenye ukubwa wa zaidi ya kilomita za mraba 14,000 nchini Tanzania hadi nchini Kenya na kuhesabika kua ni yenye aina mbali mbali za wanyama wa mbuga kuliko eneo jingine lolote duniani, kumekuwepo na kitisho kikubwa cha kupotea kwa buadhi ya wanyama ambao ni adimu kupatikana sehemu nyingine duniani.

    Pia Mbuga za wanyama za Selous, Ruaha na Tarangire nchini Tanzania, Tsavo na Amboseli nchini Kenya, kote huko ambako wanyama mbali mbali kama vile Tembo wakubwa wa kiafrika au vifaru wa mekua katika tishio kubwa la kutoweka kutokana na vitendo haramu vinavyofunywa na "majangiri" ambao huwauwa wanyama hao kiholela ili kuyipatia pembe ambazo huuzwa katika maeneo ya Mashariki ya Mbali na Mashariki ya kati barani Asia kwa thamani kubwa.

    Anasema ni wazi kabisa Serikali za Mataifa yetu hazina budi kuchukua hatua mwafaka katika kulinda tajiri wetu huo mkubwa usitoweke na kubakia kama ni historia tu kwa vizazi vijavyo.

Idhaa ya Kiswahili 2004-09-14