Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-09-14 16:26:06    
Mpunga mpya chotara wa China wachukua nafasi ya kwanza duniani kwa utoaji wa mavuno

cri

    Tarehe 3 mwezi Septemba, kwenye mashamba ya vielelezo katika tarafa ya Tao Yuan, wilaya ya Yong Sheng mkoani Yun nan, wataalamu husika wakivuna na kupima hapo papo, mavuno ya mpunga chotara aina mpya ya 7954B uliooteshwa na wataalamu wa kuotesha mbegu za mpunga wa China, yalifikia kilo 17928 kwa hekta.

    Mkuu wa tume ya wataalamu wa kukagua na kupima mavuno ya mazao, naibu mkurugenzi wa kudumu wa kamati ya taaluma ya kupanda mimea ya China Bw. Zhang Hong zhi alisema kuwa, kiasi cha mavuno ya aina hiyo ya mpunga kinaongoza duniani, na kuwa na sifa nyingi, zikiwa ni pamoja na kipindi mwafaka cha ukuaji, hali mwafaka ya mavuno, uwezo mkubwa wa kupambana na madhara na kujirekebisha. Hivyo, kuna mustakabali mzuri wa kueneza mpunga wa aina hiyo.

    Mpunga wa aina hiyo ulioteshwa na taasisi ya sayansi ya kilimo ya mkoa wa Zhe Jiang, na mradi huu wa mashamba ya vielelezo wa tarafa ya Tao yuan ulifanywa kwa pamoja na taasisi ya sayansi ya kilimo ya mkoa wa Zhe jiang na taasisi ya sayansi ya kilimo ya mkoa wa Yun nan. Wataalamu walipanda mbegu tarehe 5 mwezi March, kupandikiza miche ya mbegu hiyo tarehe 19 mwezi Aprili, na mpungu huo ulikuwa na mashuke yenye urefu sawasawa tarehe 22 mwezi Julai, kipindi nzima cha ukuaji ni siku 182. Asubuhi ya tarehe 3 mwezi Septemba, wataalamu tisa wa mpunga kutoka kamati ya taaluma ya upandaji wa mpunga ya China, taasisi ya mpunga wa China, chuo kikuu cha Zhe jiang na taasisi ya sayansi ya kilimo ya mkoa wa Yun nan walivuna na kupima mavuno ya mpunga wa aina hiyo hapo papo.

    Baada ya kupima kwa makini eneo la mashamba, kuchukua sampuli, kupima uzito wake na kupiga hesabu, wataalamu hao walivuna kilo 1424.7 za mpunga kwenye shamba lenye eneo la hekta 0.08. profesa Zhang Hong cheng alieleza kuwa, "tulikagua, kupima na kuthibitisha utoaji wa mpunga wa aina hiyo kwa kufuata mbinu ya kukagua na kupima inayotumika sana nchini China, baada ya kuvuna, kukoboa na kuondoa takataka, tulipima mpunga huo kwa kufuata kigezo cha kitaifa."

    Kutokana na maelezo ya profesa wa chuo kikuu cha kilimo cha mkoa wa Yun nan, ambaye pia ni naibu mkuu wa tume hiyo ya wataalamu Bw. Shi Chang jun, tarafa ya Tao Yuan iko kwenye sehemu ya bonde la mto Jin Sha jiang, ambayo iko umbali wa mita zaidi ya 1100 kutoka usawa wa bahari. Sehemu hiyo ina mwangaza wa kutosha na tofauti kubwa ya halijoto kati ya usiku na mchana. Mashamba katika sehemu hiyo yana ardhi yenye mchanga, ambayo ni mazingira mazuri kwa kilimo cha mpunga. Kwa kawaida, wakulima wa huko wanaweza kuvuna kilo 10500 hadi 12000 za mpunga kwa hekta, sehemu hiyo ni sehemu yenye utoaji mkubwa wa mpunga ambayo inajulikana nchini kote. Lakini wastani wa mavuno ya mpunga katika mkoa wa Yun nan ni kilo 6000 tu kwa hekta.

    Mtafiti wa taasisi ya mpunga ya China, ambaye pia ni naibu mkuu wa tume ya wataalamu Bw. Zhu De feng alisema kuwa, "katika miaka ya karibuni, wastani wa mavuno ya mpunga nchini China ni karibu kilo 6300 kwa hekta, na utoaji wa mpunga kwa hekta na eneo la kupanda mpunga limekuwa linapungua. Tukitaka kuongeza mavuno ya ujumla ya mpunga, lazima tueneze aina mpya ya mpunga yenye mavuno makubwa na teknolojia husika za kupanda. Mavuno ya mpunga wa aina ya 7954B unaweza kufikia kilo 8250 hadi 9750 kwa hekta kwenye sehemu zinazofaa nchini China. Wataalamu wote wanaona kuwa mpunga wa aina hiyo una mustakabali mzuri na kupendekeza kueneza mpunga wa aina hiyo kwenye sehemu zinazofaa nchini China.

Idhaa ya Kiswahili 2004-09-14