Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-09-14 17:49:55    
Erlianhoate, mji unaostawi katika sehemu ya mpakani nchini China

cri

    Ukitembea katika mji Erlianhaote wenye majengo marefu na mitaa ya kisasa, na kuangalia wageni wenye ngozi za rangi mbalimbali wakipita kwenye barabara, hawezi kufikiria kuwa katika miaka zaidi ya kumi iliyopita mji huo ulikuwa tarafa moja ndogo yenye idadi ya watu ya chini ya elfu kumi. Hivi sasa mji huo umepiga hatua kubwa ya maendeleo na kuvutia watu wengi kutokana na mafanikio yake.

    Mji wa Erlianhaote iko katika sehemu ya kaskazini ya mkoa ujiendeshao wa Mongolia ya ndani nchini China, ni mji pekee nchini China wenye njia ya reli inayokwenda nchini Mongolia. Kabla miaka zaidi ya 40 iliyopita, huko kulikuwa pori lisilo na wakazi wa kudumu. Katika eneo hilo kulikuwa na wafugaji waliochukua mahema kwenda huko kuchunga mifugo yao, isipokuwa katika majira ya joto. Baadaye, mji wa Erlianhaote ulikuwa na njia ya reli, na kuendelezwa kuwa mji.

    Mwaka 1992, Erlianhaote ulikuwa ni mmoja wa miji ya China iliyotangulia kutekeleza sera za kufungua mlango kwa nchi za nje. Kwa muda mfupi, wafanyabiashara walimiminikia huko kutoka nchi za Mongolia na Russia. Wakati ule, ingawa watu walijaa sokoni, lakini hakukuwa na kelele nyingi. Wafanyabiashara kutoka nchi za Mongolia, Russia na Ulaya walipozungumza na wafanyabiashara wa China kuhusu bei za vitu kwa kutumia Kikokotoo (calculator) au kutumia ishara za vidole.

    Hivi sasa, hali hiyo imebadilika sana, wachina waliofanya biashara huko, wanaweza kuzungumza na wafanyabiashara wa kigeni bila vipingamizi. Vilevile baadhi ya wafanyabiashara wa kigeni pia wanaweza kuzungumza kichina katika shughuli zao za biashara. Mchina mmoja anayeuza nguo katika soko la huko alisema kuwa sasa ana miaka zaidi ya kumi tangu aanze kufanya biashara ya kuuza nguo pamoja na wafanyabiashara kutoka Mongolia katika soko la mji wa Erlianhaote. Sasa hana wasiwasi kuongea kwa Kimongolia na wafanyabiashara hao kutoka Mongolia.

    Biashara imestawisha mji wa Erlianhaote, ambao hapo zamani watu walisema kwa mtu anapopita katika mji huo akivuta sigara, anapofikia mwisho wa mji atakuwa amevuta nusu ya sigara. Hivi sasa mji huo umepanuliwa mara tatu, barabara za mjini ni pana na zenye kunyooka. Meya wa mji huo Bw. Chen Heping alisema, "Erlianhaote ukiwa ni mji unaofungua mlango kwa nchi za nje, serikali ya mji inafuata wazo la kustawisha mji kwa shughuli za biashara na kukukuza uchumi na maendeleo kwa kutekeleza sera za kufungua mlango. Licha ya hayo, mji huo unaendeleza ujenzi miundo mbinu na mazingira ya asili. Thamani ya uzalishaji mali kwa mji wa Erlianhaote imeongezeka na kufikia Yuan za Renminbi kiasi cha milioni 800 mwaka 2003 kutoka kiasi cha milioni 150 mwaka 1994, likiwa limeongezeka mara 5.3."

    Bw. Chen Heping alisema kuwa biashara katika sehemu ya mpakani ni hali bora ya maendeleo ya Erlianhaote, na pia ni nguvu muhimu inayoleta ongezeko la uchumi wa mji. Katika soko kubwa kabisa la bidhaa za nchini na nchi za nje la mji wa Erlianhaote, ambalo lina pilikapilika za biashara ya bidhaa zilizoletwa kutoka Mongolia na Russia. Soko hilo kila siku linatembelewa na watu zaidi ya elfu 10 wakiwemo wafanyabiashara na watalii wa nchini na kutoka nchi za nje. Mazulia pamoja na mapambo ya zulia ya kutundikwa ukutani, kamera na darubini za Russia, vyombo vya umeme, mboga na vyakula vya kichina ni vitu vinavyonunuliwa sana na watu. Katika mwaka uliopita, bidhaa zilizosafirishwa nje na kuagizwa kutoka nje kupitia forodha ya mji wa Erlianhaote zilifikia tani milioni 5, zikiwa na thamani ya dola za Kimarekani milioni 950.

    Kadiri uchumi wa Erlianhaote unavyopata ongezeko kubwa, ndivyo kiwango cha maisha ya wakazi wa mji huo kinavyoinuka kwa udhahiri. Jambo linalowafanya wakazi wa Erlianhaote kujivunia ni kuwa barabara za mjini zimekuwa pana, majengo marefu yamejengwa kwa wingi na bidhaa za aina mbalimbali zinapatikana katika maduka ya mji huo. Mbali na hayo, katika mji huo yamejengwa majengo mengine ya miundo mbinu yanayohusika na maisha ya wakazi, kama vile shule, majumba ya sinema, maduka ya vitabu, hospitali, maduka makubwa, hoteli na uwanja mkubwa mjini.

    Bwana Yang Jinrui ambaye ameishi katika mji huo kwa miaka mingi, alipozungumzia mabadiliko ya mji huo, alisema, "Zaidi ya miaka 10 iliyopita, tulikuwa na shida ya kupata mboga, ambazo zilikuwa zinaletwa hapa kutoka sehemu nyingine, tena kwa bei ghali. Lakini katika miaka ya karibuni, wakazi wa mji wetu wameweza kupata mboga kwa bei nafuu, pamoja na vitu vyote wanavyohitaji, hata wanaweza kupata samaki, kamba na kaa wa baharini wa sehemu ya kusini."

    Bwana Yang alisema kwa furaha kuwa barabara moja ya ngazi ya taifa inayoanzia katika mji wa Erlianhaote na kufikia mkoani Yunnan, sehemu ya kusini magharibi ya China itaanza kujengwa hivi karibuni. Licha ya hayo, ujenzi wa uwanja wa ndege wa mji huo pia unaandaliwa.

    Kuboreshwa kwa uhusiano wa kirafiki kati ya China na Mongolia pamoja na Russia, kumeleta nafasi mpya kwa mji huo unaoendelea wa Erlianhaote. Kutokana na uchunguzi, upungufu wa nafaka, nyama, maziwa, mboga na matunda nchini Mongolia na sehemu ya mashariki ya Russia ni kati ya 30% na 70% kwa mwaka, wakati bidhaa za vitambaa vya pamba, sufi, vyombo vya umeme vya nyumbani na zana za kazi za viwanda za usindikaji vina uhaba wa malighafi na kuhitaji kuagiza kutoka nchi za nje. Hivyo, serikali ya mji wa Erlianhaote inazipa motisha kampuni zenye nguvu kwenda kufanya ushirikiano wa kiuchumi na kiteknolojia katika nchi hizo mbili.

Idhaa ya Kiswahili 2004-09-14