Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-09-15 11:06:52    
Wageni wanaojifunza lugha ya Kichina

cri

    uchumi wa China umekuwa ukiendelea kuongezeka kwa kasi kubwa ambapo mawasiliano kati ya China na nchi za nje yanazidi kuongezeka. Kutokana na hali hiyo, hadhi ya lugha ya kichina pia inainuka siku hadi siku duniani. Ingawa watu wengi wanaona kuwa, lugha ya kichina ni ngumu, lakini sasa idadi ya watu wanaojifunza lugha ya kichina inaongezeka siku hadi siku.

    Bi Kerstin Storm ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Minstel cha Ujerumani. Alipokuwa anasoma katika shule ya sekondari alikuwa anapenda lugha na utamaduni wa China. Lakini katika wakati ule hakuna masomo ya lugha ya kichina katika shule za sekondari, lakini katika chuo kikuu ndoto yake ya kujifunza lugha ya kichina ilitimia.

    Baada ya miaka minne, Bi Kerstin Storm aliweza kuzungumza vizuri lugha ya kichina. Anamwambia mwandishi wa habari kuwa, kujifunza lugha ya kichina ni changu lake zuri.

    " Nchini Ujerumani watu waliojifunza lugha ya kichina ni wachache, hivyo naona kuwa, lugha ya kichina inanisaidia kupata ajira. Sasa China ina nafasi nyingi, na makampuni mengi ya Ujerumani yameanzisha mashirika nchini China, ushirikiano wa kibiashara kati ya China na Ujerumani unaendelea kwa haraka."

    Mwaka kesho, Bi Kerstin Storm atahitimu chuo kikuu. Matumaini yake makubwa ni kuwa mwandishi wa habari. Mwaka mmoja uliopita, alitumia likizo yake kufanya mazoezi katika ofisi ya gazeti moja la Ujerumani iliyoko China. Alisema kuwa, kama ndoto yake ya kuwa mwandishi wa habari haiwezi kutimia atatafuta ajira nyingine inayohusika na China, kwa mfano kuendelea kujifunza lugha ya zamani kichina au kutafiti utamaduni wa China.

    Bi Kerstin Storm alisema kuwa, sasa nchini Ujerumani kuna watu wengi wanaojifunza lugha ya kichina. Zamani alipokuwa mwanafunzi wa chuo kikuu, darasa lake lilikuwa na wanafunzi 10 tu, lakini sasa wamefikia 40. Alisema kuwa, madhumuni ya watu wa Ujerumani kujifunza lugha ya kichina ni kuzingatia shughuli za uchumi na ajira, wanaona kuwa, nchini China kuna nafasi nzuri ya kuwawezesha watu kujiendeleza; na wengine wanapenda utamaduni na historia ya China.

    Ingawa Bi Kerstin Storm anaongea kichina vizuri, lakini yeye bado anaona kuwa, lugha ya kichina ni ngumu, kutamka na kuansika siyo rahisi na hasa maneno mengi yana matamshi yanayofanana, lakini yana maana tofauti.

    Bi Kerstin Storm alitaka kuwaambia watu wanaojifunza lugha ya kichina au watakaojifunza lugha ya kichina kutumia nafasi zote kuzungumza na wachina, hii ni njia nzuri ya kupata maendeleo makubwa katika kujifunza lugha ya kichina. Anasema:

    " kama unajifunza lugha ya kichina, usiiogope, kwa sababu lugha ya kichina si ngumu kama watu wengine wanavyosema; ukizungumza na wachina mara ya kwanza na wakaonekana wanaelewa, unaweza kuzungumza nao, hivyo, utaona kuwa, lugha ya kichina si ngumu na utapata maendeleo siku hadi siku."

    Kama Bi Kerstin Storm Ndugu Ahmed Abdelazizawad Sadek mwenye umri wa miaka 22 aliipenda sana lugha ya kichina sana. Yeye ni mwanafunzi wa chuo kikuu wa Misri. Alipokuwa mtoto, alitambua kuwa, bidhaa nyingi walizonunua kutoka dukani zilitengenezwa na China". Tangu wakati huo alianza kuipenda China. alipokuwa chuo kikuu alianza kujifunza lugha ya kichina. Baada ya masomo ya miaka 3, aliweza kuzungumza lugha ya kichina. Anasema :

    " lugha ya kichina imekuwa lugha yangu ya pili. Naipenda sana lugha ya kichina, napenda kusoma magazeti, na makala za kichina."

    Hivi sasa kutokana na maendeleo makubwa ya uchumi wa China, idadi ya watu wanaojifunza lugha ya kichina inaongezeka siku hadi siku, watu hawa wanatoka Asia, Ulaya, Amerika na Afrika. Si kama tu wanajifunza lugha ya kichina, utamaduni na historia ya China, bali pia wanajifunza masomo ya uchumi, biashara, na sheria kwa lugha ya kichina.

   Kutokana na takwimu zisizokamilika, sasa idadi ya watu wanaojifunza lugha ya kichina imefikia milioni 25. ili kukagua kiwango cha lugha ya kichina cha wageni, mwaka 1991 China ilianzisha mtihani wa lugha ya kichina (HSK), mweshoni mwa mwaka uliopita, China ilianzisha vituo vya mtihani wa HSK katika miji 87 ya nchi 35, wageni laki 3.3 walishiriki kwenye mtihani huo.

    Wakati huo huo, elimu ya lugha ya kichina inaungwa mkono na nchi mbalimbali duniani. Katika nchi kadhaa, somo la lugha ya kichina si kama tu lilianzishwa katika vyuo vikuu bali pia katika shule za msingi na sekondari.

    Muda si mrefu uliopita, wizara ya elimu ya Korea ya Kusini ilitangaza kuwa, kuanzia mwaka 2005 hadi mwaka 2007, shule za msingi za nchi hiyo zitaanzisha somo la kichina. nchini Japan idadi ya watu waliojifunza lugha ya kichina ilifikia milioni moja. Nchini Uingereza, idara husika ya elimu ya Uingereza ilishirikiana na China kuanzisha kitabu kiitwacho "kujifunza lugha ya kichina kwa furaha"; nchini Ufaransa, somo la lugha ya kichina lilianzishwa katika shule 150 za sekondari, wanafunzi elfu 8 wanajifunza lugha hiyo; na nchini Marekani, ongezeko la idadi ya watu wanaojifunza lugha ya kichina ni kubwa kuliko lugha nyingine.

Idhaa ya Kiswahili 2004-09-15