Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-09-15 17:32:13    
Siku ya kuondoa ujinga duniani

cri

    Tarehe 8 mwezi Septemba ni siku ya 39 ya kuondoa ujinga duniani. Mwaka 1966, shirika la Elimu, sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa liliamua kuweka tarehe 8 mwezi Septemba kama siku ya kuondoa ujinga duniani. lengo lake ni kuhamasisha nchi mbalimbali na jumuiya husika duniani kupambana na ujinga, na kutaka kusukuma mbele kazi za kuondoa ujinga kupitia shughuli za siku ya kuondoa ujinga duniani, ili kuwasaida watoto wenye umri wa kwenda shule kote duniani waweze kwenda shuleni, wanafunzi wasikatishe masomo na watu wazima wasiojua kusoma wala kuandika wapate nafasi ya kupata elimu. Umoja wa Mataifa pia uliamua kuwa, miaka 10 kuanzia Januari mwaka 2003 ni miaka 10 ya kuondoa ujinga duniani, ili kuhimiza kazi za kuondoa ujinga kote duniani.

    Kutokana na takwimu husika, idadi ya watu wazima wasiojua kusoma wala kuandika duniani imefikia karibu milioni 860, ikiwa inachukua karibu asilimia 20 ya idadi ya watu wazima kote duniani. Watoto milioni 113 wenye umri wa kwenda shule duniani wamekosa nafasi ya kupata elimu shuleni, na theluthi mbili kati yao ni watoto wa kike. Wengi wa watu wasiojua kusoma wala kuandika wako katika nchi maskini za Afrika, Asia na Latin Amerika, pia wako watu wengi wasiojua kusoma wala kuandika katika nchi zilizoendelea, nchini Marekani watu wazima milioni 40 wanashindwa kuwasomea watoto wao vitabu na magazeti na kuwasaidia watoto wao kufanya mazoezi ya nyumbani.

    Kuna vyanzo vyingi vinavyosababisha watu wengi kutojua kusoma wala kuandika katika nchi zinazoendelea. kutokana na ongezeko la idadi ya watu, nchi zinazoendelea zina watu wengi zaidi, ongezeko la idadi ya watu ni kubwa zaidi, na uchumi wa nchi hizo uko nyuma kuliko nchi nyingine duniani, uwekezaji wa taifa katika elimu hauwezi kwenda sambamba na ongezeko la idadi ya watu. Kutokana na lugha na utamaduni, tatizo la lugha nyingi ni kubwa zaidi katika nchi hizo zinazoendelea, hasa katika nchi za Afrika. Nigeria yenye watu zaidi ya milioni 100 kwa jumla ina lugha 440, na Benin yenye watu milioni 6.6 tu ina lugha karibu 60. kutokana na uzalishaji mali wa kijamii, nchi hizo zinazoendelea zimeachwa nyuma kimaendeleo na kiteknolojia, mahitaji ya elimu na ujuzi katika nchi hizo ni ya chini na ukosefu wa elimu na ujuzi kwa wafanyakazi hauathiri sana uzalishaji mali.

    Maendeleo ya kasi ya sanyansi na teknolojia si kama tu yamefanya nchi zinazoendelea kukabililana na matatizo ya upungufu wa teknolojia, watu wenye ujuzi na fedha, bali pia yamefanya nchi hizo kutambua umuhimu wa kuendeleza elimu. Baadhi ya nchi zimeweka mbinu za kipekee zinazofaa kutokana na hali halisi ya nchini. Kwa mfano, Brazil ilitangaza kutekeleza mpango wa kuondoa ujinga nchini humo utakaoendelea kwa miaka 4 kuanzia mwaka 2003, na lengo lake ni kuondoa kikamilifu ujinga nchini humo kabla ya mwaka 2007.

    Katika miaka 50 iliyopita, idadi ya watu wazima nchini China wasiojua kusoma na kuandika imepungua kwa kiasi kikubwa, kutoka asilimia 80 ya wananchi wote wakati China mpya ilipoasisiwa hadi asilimia 8.72 katika mwaka 2002. serikali ya China ilitimiza lengo la kueneza elimu ya lazima ya miaka 9 na kuondoa kimsingi tatizo la vijana kutojua kusoma wala kuandika ilipofika mwishoni mwa mwaka 2000, na idadi ya vijana wasiojua kusoma wala kuandika imepungua na kufikia chini ya asilimia 5 katika mwaka 2003. mwaka 2003, takwimu zilizotangazwa na shirika la elimu, sanyasi na utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) kuhusu shughuli za kuondoa ujinga duniani katika miaka 10 iliyopita zimeonesha kuwa, China imepata mafanikio makubwa zaidi katika elimu na shughuli za kuondoa ujinga miongoni mwa nchi zote 40 zilizochunguzwa.

Idhaa ya Kiswahili 2004-09-15