Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-09-16 11:03:16    
Opera ya Beijing

cri

    Opera ya Beijing ni azizi ya utamaduni wa taifa la China, pia ni hazina ya bohari la utamaduni wa binadamu. Ina maudhui mengi, fani kamilifu na ustadi mkubwa, inamithilisha vizuri wazo la Wachina kuhusu sanaa.

    Opera ya Beijing imekuwa na historia zaidi ya 200, Mwaka 1991, ilikuwa maadhimisho ya miaka 200 kwa kuanzishwa kwa Opera ya Beijing, Wizara ya Utamaduni, Serikali ya Manispaa ya Beijing, Jumuia ya Wachezaji wa Tamthilia na Opera wa China na Chama cha Opera cha China viliandaa mjini Beijing Kongamano la Kustawisha Opera ya Beijing na Maadhimisho ya Miaka 200 tangu Opera ya Kihui Kuchezwa Beijing.

    Mwaka 1790, Kikundi cha Opera ya Kihui cha Sanqing kilifika Beijing kutoka Jimbo la Anhui kwa minajili ya kutoa pongezi kwa siku ya kuzaliwa mfalme. Matumbuizo yao yalipata shangwe kubwa. Baadaye, vikundi vingine vitatu vilifika Beijing, vilijiunga na kile cha kwanza na kutumbuiza kwa pamoja. Umaarufu wao ulivuma kote mjini na vilitawala majukwaa ya michezo. Kwa muda wa nusu karne, opera za Kihui, Jingqiang, Handiao, Qinqiang na Kunqu zilifunzana na kuchukuliana sifa. Ilipofika katikati ya karne ya 19, Opera mpya, yaani Opera ya Beijing ilitokea juu ya msingi wa opera hizo za zamani.

    Hadi leo hii, Opera ya Beijing imekua kwa miaka 150 na imeunda mfumo mkamilifu wa sanaa.

    Kongamano hilo lilihudhuriwa na vikundi zaidi ya 50, ambavyo ni pamoja na vya Taiwan na Hongkong. Maelfu ya wachezaji wlionyesha matumbuizo 166 ya Opera za Beijing, Kihui, Kihan, Qinqiang na Kunqu. Baadhi ya vikundi vilitembelea viwanda, vijiji, vyuo vikuu na maofisi kufanya matumbuizo. Idadi ya jumla ya watazamaji ilikuwa laki 1.7, ambayo ni kubwa kabisa kushinda tumbuizo lolote lililofanywa katika miaka 10 ya karibuni.

    Zaidi ya hayo, mabingwa, wataalamu na wasanii walijadili sanaa ya Opera ya Beijing na kutoa tathmini kwa matumbuizo hayo.

Idhaa ya Kiswahili 2004-09-15