Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-09-20 21:39:19    
Vivutio vya utalii vya mji mdogo wa wilaya Kaiyang

cri

    Mkoani Guizhou kuna milima mingi, watu wanaoishi mkoani humo wanapenda sana milima. Mji mdogo Kaiyang uko karibu na mji mkuu wa mkoa Guiyang, ukifunga safari kwenda Kaiyang kutoka Guiyang, baada ya saa moja na kitu tu utafika huko. Njiani unaweza kuona nyumba nyingi za wakulima zilizotapakaa kwenye sehemu za milimani, mandhari ya huko inapendeza sana.

    Siku hiyo jioni tulifika mji wa Kaiyang tukaona, na kuona mabadiliko makubwa yaliyotokea mjini humo. Pembeni mwa mji, bado kuna nyumba za kawaida zilizojengwa kwa matofali, lakini katikati ya mji huo, barabara zimejengwa kuwa pana, kando mbili za barabara kuna majengo mengi ya kisasa. Mnamo saa 4 za usiku, maduka mengi mitaani yalikuwa bado yamefunguliwa yakiendelea na shughuli.

    Mji wa Kaiyang umekuwa na historia ya zaidi ya miaka 1300. Eneo la mji huo wa wilaya ni kilomita zaidi ya 2000, mjini humo kuna miti mingi na majani yanayositawi, hali ya hewa ni ya baridi, joto na unyevunyevu katika sehemu hiyo ni mzuri, asilimia 45 ya eneo la mji huo lina miti, na wastani wa halijoto ya hali ya hewa ni nyuzi 16 kwa mwaka.

    Mji wa Kaiyang una sura maalum ya kijiolojia ya Chokaa, milima yenye maumbo mbalimbali ya ajabu inauzunguka mji huo, mabonde yametapakaa karibu kila mahali, mito chini ya ardhi, maporomoko yanayoruka, mashimo makubwa milimani mithili ya mashimo ya mbinguni, pamoja na mashimo kwenye ardhi. Mapango ya milima na mabonde yametapakaa pote na kuonekana mandhari murua na yenye kuvutia. Ukitembea kwenye milima wa Kaiyang, utaona njia ya mzunguko inayoongoza kwenda sehemu mbalimbali zenye vivutio vingi kama ukitembea katika hali iliyoonekana katika michoro.

    Tulifika kwenye bonde kubwa la Nanjiang, tulivutiwa sana na mandhari nzuri ya bonde hilo. Bwana Zhao Weijia anayeshughulikia uendelezaji wa sehemu hiyo alituambia:

    Bonde kubwa la Nanjiang mjini Kaiyang lina urefu wa kilomita 41. Kilele cha mlima wa bonde hilo, kina urefu wa mita zaidi ya 390. Kwenye bonde hilo, kuna vivutio zaidi ya 80 vyenye mandhari ya kimaumbile. Aidha, kuna maporomoko zaidi ya 40 ya maumbo mbalimbali tofauti, na kimo cha juu kabisa cha maporomoko kinafikia mita zaidi ya 150.

    Ukitaka kuingia kwenye sehemu zenye vivutio, unapaswa kupanda jahazi na kutoka pia kwa jahazi. Milima mirefu ya ajabu, mabonde makubwa, maporomoko mbalimbali tofauti kwenye bonde pamoja na mapango mbalimbali yanaweza kukuvutia sana hata utang'ang'ania huko na kusahau kuondoka.

    Mtalii kutoka mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya ndani, kaskazini ya China Bibi Xue Yi alisema:

    Naona sehemu hiyo yenye mandhari nzuri ya kimaumbile inaweza kuwalea watu wenye hisia za kishairi, vivutio vingi vya kupendeza vya sehemu hiyo vinagusa hisia za watu wote wa sehemu hiyo. Ndiyo maana watu wengi wakiwemo wakulima, makada, na wanafunzi wanaandika mashairi ya kusifu mandhari nzuri ya sehemu hiyo. Utamaduni wa huko ni wenye mtindo maalum.

    Tulipotembelea mjini Kaiyang kweli tulivutiwa na milima, mawe ya milimani yenye maumbo ya ajabu, na wakazi wa huko wenye mila na desturi za kiasili pia walionekana kuvutia sana.

    Tulipofika Kaiyang yaani siku ya tarehe 6 Juni ya kalenda ya kilimo ya kichina, ilikuwa ni sikukuu ya kijadi ya kabila la wabuyi ambao ni wakazi wengi kabisa wa sehemu hiyo. Kila ifikapo siku hiyo wakazi wote wa vijiji vya sehemu hiyo wanavaa nguo maridadi, kuimba nyimbo, kupiga vinanda na kucheza ngoma kwa furaha. Sherehe ya sikukuu hufanyika kwa siku 3 mfululizo.

Idhaa ya Kiswahili 2004-09-20