Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-09-21 19:39:36    
Michezo ya ngoma na nyimbo ya China (1)

cri
    Michezo ya ngoma na nyimbo ya China iliyosimulia hadithi kamili ilianzia karne ya 13. Hivi leo kuna aina zaidi ya 300 za michezo ya sehemu mbalimbali nchini China, na Opera ya kibeijing inajulikana kama "Opera ya nchi" inayokusanya sifa nzuri za michezo ya sehemu mbalimbali . Lakini Opera ya kibeijing ni Opera ya kibeijing tu, wachina wanaona kwamba, michezo ya nyimbo na ya ngoma inatofautiana sana na Opera ya kibeijing. Ni kuanzia karne hii tu ndipo wachina walipojua opera ya nyimbo na ngoma ya zama za karibu za Italia .

    "Romiou na Juliye" ni opera moja ya Ulaya iliyovuma sana duniani, karibu watu wote wa China waliijua, uimbaji wake wa sauti kubwa uliolingana na hadithi yake ndefu yenye huzuni uliwasisimua watazamaji wa China wa vizazi kadha. Opera zilizojulikana duniani zimekuwa data za mfano kwa wachina katika kufahamishwa na kuelewa sanaa hiyo ya nchi za nje .

    Michezo ya nyimbo na ngoma ya China

    Katika miaka ya 50 ya karne hii, Mchezo wa ngoma wa "Taa ya Yungiyungi " uliotungwa kutokana na michezo ya kijadi ya China, ulieleza hekaya za kale zlizopendwa sana na watu wa China, kwamba mama mmoja aliyejichagua mume aliyempenda alifungwa chini ya mlima mkubwa, mtoto wake alipokuwa mzima, alikwenda kupasua mlima na mama yake akatoka. Mchezo huo ulionyesha matumaini ya watu, kwamba watu wema hushinda watu waovu, na nuru hufukuza giza.

    Mchezo huo ulionyesha aina nyingi za uchezaji wa ngoma asilia za kitaifa zinazopendwa na watu wa China, pia uliunganisha aina ya mwundo wa mchezo wa balet wa kiulaya na mbinu ya uchezaji wa ngoma ya kijadi ya taifa la China, na mchezo huo ukawa mkubwa wenye mtindo pekee wa China.

    Mchezo wa ngoma uitwao "Chama cha visu vidogo" uliotungwa wakati huohuo hautokani na hekaya kama michezo mingine maarufu ya ilivyo. Mchezo huo ulitungwa juu ya msingi wa ngoma za kale za China na ngoma asilia za sehemu ya kusini ya mto Changjiang, ambapo miondoko kadha wa kadha ya Gongfu ya kijadi ya China ilitumika na kuboreshwa zaidi kwenye mchezo huo pia. Watungaji wa mchezo huo walifaulu kusimulia sura za watu wenye tabia wazi , na kusifu moyo wa kutoogopa nguvu za mabavu. Mchezo huo ulijulikana kama mfano mzuri wa michezo ya ngoma iliyotungwa na wachina katika karne ya 20.

    Watungaji wa michezo hiyo miwili walifaulu kuunganisha maarifa ya utungaji wa michezo ya ngoma ya kijadi ya China na michezo ya balet ya kiulaya, wakafungua njia ya kujifunza sanaa ya nchi za nje na sanaa ya kale kwa kuboresha michezo ya China ya hivi leo. Michezo hiyo miwili ilionyesha uelewaji na uvumbuzi wa watungaji wa China juu ya utamaduni wa nchi za mashariki na magharibi.

     Watu wanaoshughulikia michezo ya ngoma ya China walitengeneza na kutafiti michezo ya ngoma ya kijadi na asilia za China kwa muda mrefu, hivyo waliweza kupata ujuzi mwingi juu ya ngoma nyingi asilia za makabila mbalimbali ya China, kazi zao ziliweka msingi kwa utungaji na ukuaji wa michezo ya ngoma ya China. Wakati huo huo, wasanii wa China pia walifanya maingiliano mbalimbali katika maeneo mengi zaidi na zaidi kati yao na wasanii wa nchi mbalimbali duniani, ambapo walipata fursa za kutazama michezo mingi maarufu ya balet duniani, na kujifunza kutoka kwa michezo hiyo ya kiulaya, wakaboresha michezo ya ngoma ya China juu ya msingi wa utamaduni wa kitaifa, na kuifanya iwe ya aina mbalimbali ya kuwapendeza watu. (itaendelea)

Idhaa ya Kiswahili 2004-09-21