Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-09-22 17:59:10    
Wanasayansi watumia akili za wadudu katika kutengeneza silaha

cri

    Sisimizi kuhama, nyuki kujenga nyumba, akili za pamoja za wadudu hao zinawashangaza sana binaadamu. Hivi sasa wanasayansi wa Australia wanafanya utafiti kubuni software zinazofuatisha vitendo vya pamoja vya wadudu na kutengeneza zana mpya ndogondogo za kijeshi, zinazoweza kutumika katika maeneo makubwa na kutodhibitiwa na binadamu ili kutekeleza majukumu katika mazingira yenye hatari badala ya binadamu.

    Vyombo vya habari vya nchi za nje viliripoti kuwa wanasayansi wa Australia wamesema kuwa kubuni software za aina hiyo ni changamoto kwa wanasayansi, kwa kuwa wanatakiwa kufuatisha vitendo vya pamoja vya aina mbalimbali vya wadudu kwa kutumia kanuni za hisabati za kiwango cha juu sana, na kufikia hatua kama aliyoisema Bw. Rein mwanahisabati anayeongoza utafiti huo, "pembezoni mwa machafuko. Alifafanua, "mfumo wenye utaratibu wa kupindukia, utaonekana kuwa mgumu, lakini mfumo wa mchafuko ni kufikia pembezoni mwa kubomoka kabisa. Kitu tunachotafuta ni hali iliyo kati ya mifumo miwili, yaani kufikia pembezoni mwa mchafuko.

    Lengo la mwanzo la Bw. Rein na wenzake ni kufanya utafiti wa kutengeneza zana zinazoweza kubeba jukumu la kusimamia, hali ya hivi sasa ni kwamba zana hizo mbali baada ya kurekebishwa, zinaweza kuchukua silaha. Bw. Rein alisema kuwa mpango huo utaweza kukamilika kwa muda wa miaka 10 hadi 15. Lakini kuangalia kutoka upande wa mambo ya kijeshi, muda huo pengine bado hautoshi, kwani kuvumbua hardware moja kwa uchache kabisa kunahitaji miaka 10.

    Lengo la wanasayansi ni kufanya mitambo midogo midogo kufanya kazi kwa pamoja, kama wadudu wanavyofanya uamuzi kwa pamoja na kufanya marekebisho kuendana na mabadiliko ya mazingira mpaka kutimiza majukumu yao.

Idhaa ya Kiswahili 2004-09-22