Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-09-22 20:09:43    
Michezo ya nyimbo na ngoma ya China (2)

cri
    Mageuzi na ufunguaji mlango wazi kwa nchi za nje yaliyoanzishwa mwishoni mwa miaka ya 70 nchini China, yaliifanya michezo ya ngoma ya China iendelezwe vizuri kuliko vipindi vingine vya hapo awali. Mchezo wa ngoma wa "Njia ya biashara ya hariri" uliotungwa mwaka 1979 ulifufua sanaa ya Enzi ya Tang ya Michoro ya Pangoni mwa Mogao, sura mbalimbali za wachezaji ngoma walioonekana kwenye michoro ziligeuka kuwa miondoko mfululizo ya kuelezea maana mpya ya kingoma, ambayo iliwawezesha watu waone pilikapilika za biashara zilizofanyika katika njia ya mawasiliano wakati wa Enzi ya Tang yenye usitawi. Mchezo huo ulijulikana kama mnara katika historia ya michezo ya ngoma ya China.

    Hivi sasa utungaji wa michezo ya ngoma ya China umepanuliwa zaidi, toka hekaya ya peponi na duniani, hadi hadithi za China na za ng'ambo ambazo zote zilisimuliwa katika utungaji wa michezo hiyo, ambapo watungaji wengi walijitahidi zaidi kuchagua maandishi maarufu ya kale na ya hivi sasa ili kuyatunga tena kuwa michezo mizuri ya ngoma. Michezo ya ngoma ya China kwa kwaida ni ya aina tatu yaani Michezo ya ngoma ya kichina; Michezo ya ngoma ya kisasa ya China; na Michezo ya balet ya China. Watungaji wa michezo hiyo hujifunza kutoka kwa michezo mingine mbalimbali ya kienyeji, kudadisi kwa mapana na marefu na kuonyesha uhodari wa kila aina, ambapo hali halisi ya ukuaji wa michezo ya ngoma imeonekana nchini China. Nchini China michezo ya aina mbalimbali kama vile "Mchezo wa Yangge", "Mchezo wa Mikongoji" na "Mchezo wa ngalawa ya nchi kavu" ilienea sana na kupendwa na wananchi, michezo hiyo si kama tu inabudisha watu, bali pia ina mvuto wake mkubwa wa kimaonyesho, kila ifikapo sikukuu au siku za mapumziko, watu wa familia nyingi hutumbuizwa kwa michezo mbalimbali barabarani au kwenye majumba yua tamthiliya, ambapo waburudika

    sana kutokana na sanaa ya michezo hiyo.

    Sanaa ya michezo ya nyimbo pia imeendelezwa siku hadi siku.

    Kabla ya mwaka 1945, michezo ya nyimbo ya China ilichipuka na kukua siku hadi siku, ambapo wanamuziki wengi walifanya juhudi kubwa zenye shida ili kuifanya sanaa hiyo iliyotoka nje iote mizizi na kupata matunda nchini China, mpaka siku zilizokaribia kupata ushindi wa vita vya pili vya dunia, ndipo ulipotungwa Mchezo wa nyimbo wa "Msichana mwenye nywele nyeupe", mchezo ambao ulijulikana kama mnara wa michezo ya nyimbo ya China.

    Msichana Xier wa familia ya mkulima, aliishi pamoja na baba yake mzazi katika hali duni sana. Wakati wa sikukuu ya mwaka mpya, msichana huyo alifurahia sana pambo la nywele la uzi mwekundu alionunuliwa na baba. Lakini baba yake alijiua kwa sababu hakuweza kulipa madeni aliyodaiwa na bwana shamba. Msichana Xier alilazimika kuwa mtumishi wa bwana shamba. Usiku wa mmoja wa manane, bwana shamba alimbaka, badaye kumwuza kwa mfanyabiashara wa watu. Ili kujipatia haki ya kuishi, msichana Xier alitoroka, akaenda mlimani, akaishi pangoni. Baada ya miaka kadhaa, rangi ya nywele za msichana huyo ikageuka kuwa nyeupe kutokaan na kutopata mwanga wa jua na chumvi kwa kipindi chote.

    Mchezo huo ulieleza hadithi moja ya kweli, watungaji wa mchezo huo walijitahidi kujifunza maarifa ya opera ya kiulaya juu ya msingi wa kufuata uimbaji wa nyimbo asilia za China, wakaufanya muziki wa mchezo huo uonekane mvuto wake wa kimaonyesho, na pia uambatane na desturi ya uburudishaji wa watu wa China. Mpaka hivi leo mchezo huo bado unaonyeshwa mara kwa mara, ambapo waimbaji mahodari wa vizazi kadhaa wa China Guo Laiying, Pung Linan, Wan Shanhong walijitokeza kutokana na uimbaji wao katika mchezo huo. Miaka kumi baada ya kutungwa kwa mchezo huo, michezo mipya ya nyimbo ilitungwa moja baada mwignine, na mtindo wao mpya wa kufuata desturi ya uburudishaji wa raia na mwenye umaalum wa kitaifa ulikaribishwa sana na watu, michezo hiyo iliandikwa kwenye kurasa za historia ya ukuaji. (itaendelea)