Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-09-28 17:55:29    
Barua za wasikilizaji 0926

cri

    Msikilizai wetu Kilulu Kulwa wa Mtoni Kijichi Bank Quarters sanduku la posta 2503 Dar es Salaam Tanzania alipokuwa jijini Dar es Salaam alituletea barua akisema kuwa, Wahariri na watangazaji wote wa idhaa ya kiswahili ya Radio China Kimataifa salaam nyingi ziwafikie kutoka hapa Tanzania mimi msikilizaji wenu ni mzima wa afya njema, aliendelea na maisha hapo jijini Dar es Salaam akiwa na mapumziko mafupi na baadaye kurejea huko Shinyanga ili kuendelea na ujenzi wa taifa la Tanzania.

    Anasema anapenda kutujulisha kuwa wakati tukiwatangazia wasikilizaji wetu makala ya kwanza ya mashindano ya ujuzi kuhusu miaka 55 ya kuasisiwa kwa Jamhuri ya Watu wa China yaani Jumapili ya tarehe 15 August,2004, alikuwa yuko jijini Dar es Salaam alisikiliza makala hiyo na pia maswali yake mawili yaliyoulizwa.

    Anasema mpango huu wa mashindano ya ujuzi yanayoendeshwa na Radio China Kimataifa karibu kila mwaka kwa kweli ni mpango mzuri sana wa kuwafahamisha walimwengu wote waifahamu vizuri China. Anasema akiwa msikilizaji wetu ataendelea kuwa mshiriki hai wa vipindi vyetu kutoa maoni na ushauri mbalimbali na pia kujiunga na mashindano ya ujuzi yanayotangazwa na Radio China Kimataifa.

    Bwana Kulwa anasema katika barua yake hii ya leo angependa kutoa ushauri kwamba kwa miaka ijayo tunapotoa shindano fulani, kama tunataka kuwafahamisha watu wengi zaidi kwa nchi zinazozungumza Kiswahili tunachagua baadhi ya magazeti yanayochapishwa katika nchi hizo maarufu tunatoa tangazo katika gazeti kuhusu shindano lenye maandishi na anwani.

    Ushauri wake huu ni mzuri, lakini labda kutokana na hali yetu halisi ni vigumu kufanya hivyo, kwa sisi hivi sasa ni rahisi zaidi kutoa tangazo la kuendesha mashindano ya chemsha bongo kwenye tovuti yetu, lakini tunajua kuwa kwa wasikilizaji wengi wa nchi za Afrika si rahisi kupata nafasi ya kutembea kwenye tovuti, lakini tuna imani kuwa kadiri utandawazi wa uchumi unavyoendelea duniani, ndivyo hali hiyo inavyoweza kubadilika, ambapo wasikilizaji wetu wengi watatembea tovuti yetu ili kupata habari mapema kuhusu

    Bwana Kulwa anasema vilevile tungetaja na zawadi zitakazotolewa kwa washindi wa shindano hilo. Kwa njia hii inaweza kuongeza washiriki wengi zaidi wa mashindano hayo kutoka nchi za Afrika mashariki. Inabidi mbinu mbalimbali zitumike ili kuongeza washiriki wa mashindano hayo kutaka Afrika mashariki.

    Vinginevyo tunaweza kufikiria kuwa kuna ubaguzi na upendeleo wa namna fulani miongoni mwa idhaa na lugha zinazotangazwa na CRI katika kutoa tuzo kubwa kama ile mialiko na kadhalika. Jambo hili mlifikiria kwa makini sana wapendwa marafiki.

    Ras Franz Manko Ngogo wa Kemogemba CRI Listener Club sanduku la posta 71 Tarime Mara Tanzania ametuletea barua akisema kuwa, kwa heshima na taadhima ya redio hii yetu pendwa ya CRI idhaa ya kiswahili, napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa juhudi na moyo mliouonyesha watangazaji wa idhaa ya kiswahili.

    Nikiwa nafuatilia matangazo yenu ya idhaa zote mbili kiingereza na kiswahili, nilibahatikia kusikia taarifa ya washindi wa nafasi maalumu wakigusiwa. Wakati ule walipokutana na spika wa Bunge la Umma la China. Kwa usongo mkubwa nilitega sikio kwa makini ili kama ningeweza kuwa miongoni mwa wale kumi tu, lakini kwa bahati sikusikika wala nchi yangu Tanzania kusikika.

   Mwanzoni kabisa, nilipokuwa najibu maswali ya Chemsha Bongo, nilikaa nikatulia ili kuyaandalia majibu maswali yote kumi, na hata kutafakari maana na hali halisi ya jinsi niliyosikiliza makala zote tano na ambavyo ningeandika. Mollah alinisaidia nikaweza kufanya nilivyofikiri na kutuma majibu yangu kwa njia niliyoiona mwafaka ingawa usumbufu ulikuwepo kwa njia ya computa. Nilipokea jibu lenye kutia imani na kunipa matumaini kuwa jibu langu kweli lilifikia walengwa.

    Nikiwa nimeijiwa na ndoto kweli ya kufika China kuijionea yote yatendekayo huko. Nilikuwa nikitabasamu mara tu barua yenye majibu yangu ilipokuwa ikisomwa hewani.

    Hivi karibuni nilisikia redioni barua iliyokuwa na majibu ya chemsha bongo ikisomwa hewani na kunitaja kuwa juhudi za kunisaidia kugombea nafasi maalumu kama mwakilishi wa idhaa ya kiswahili, baada ya kujibu vizuri zaidi , kuwa zilishindikana nami kuambulia ile nafasi ya mshindi wa kwanza.

    Mimi binafsi niliridhika na nafasi hiyo pekee ya mshindi wa kwanza kati ya washiriki 80 wa idhaa yetu ya kiswahili.

    Muda mfupi nilipokea bahasha maalumu iliyokuwa na zawadi ya kitambaa cha Batiki pamoja na cheti maalumu cha kuwa mshindi wa kwanza.

    Kwangu mimi binafsi pamoja na wana klabu chetu cha KEMOGEMBA tunayo\ninayo furaha isiyo kifani. Na kila leo tunaendelea kusikiliza kila kipindi cha CRI idhaa ya kiswahili?matangazo ambayo kwa msaada hurushwa na KBC Kenya.

    Mwisho, tunao mpango wa kuendelea kushiriki katika Chemsha Bongo ya CRI ijayo, mwezi huu wa 8,2004 mwisho kabisa napenda kuwaarifu kuwa usikivu wa matangazo yenu masafa ya "short wave" masafa mafupi yananasika na kusikika vizuri sana. Halafu huwa kunatokea mpandano wa vipindi ama upachikaji wa vipindi kwenye vipindi vingine ambavyo sio mwafaka kwa wakati huo. Je hili ni tatizo ambalo huwa linakusudiwa au hutokea kwa udhaifu wa mafundi mitambo? Naomba nipate idhini ya kuyasimamia matangazo yenu huku na niwe nawapa taarifa ya jinsi yalivyosikika na kuendesheka.

    Tunamshukuru sana Bwana Ras Falanz Manco Ngogo na wenzake, tunapenda kuwakumbusha kuwa makala zetu za chemsha bongo zimeshawekwa kwenye tovuti yetu katika kipindi cha sanduku la barua, karibuni kutembea tovuti yetu na kusoma makala hizo, ili mjibu masuala vizuri.

Idhaa ya Kiswahili 2004-09-28