Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-09-28 18:27:38    
Eneo la ustawishaji wa uchumi na teknolojia la Qinhuangdao

cri

    Kati ya maeneo mengi ya ustawishaji wa uchumi na teknolojia ya ngazi ya taifa nchini China, eneo la Qinhuangdao sio la kuvutia sana. Lakini eneo hilo lina vitu vingi vya kipekee vikiwa ni pamoja na ukubwa wa eneo, ubora wa uwekezaji kwa wafanyabiashara wa kigeni na kiwango cha juu cha ujenzi wa mazingira.    

    Mara tu unapoingia katika eneo la ustawishaji wa uchumi na teknolojia la Qinhuangdao, vitu vinavyovutia ni barabara pana na miti mingi iliyopandwa kwenye kando mbili za barabara na majengo ya ofisi na karakana zilizopangwa kwa utaratibu mzuri. Hivi sasa wafanyabiashara waliokwenda kuwekeza katika eneo hilo, licha ya kampuni na viwanda maarufu vya nchini, kuna kampuni nyingi za kimataifa kutoka Marekani, Japan na Singapore. Ofisa husika alisema kuwa vitu vinavyowavutia wafanyabiashara wengi kwenda kuwekeza katika eneo la Qinhuangdao ni hali bora ya kijiografia na mazingira safi ya uwekezaji.

    Kampuni ya mitambo ya kuzalisha umeme ya Harbin ni ya kwanza kwa ukubwa inayotengeneza mitambo ya kuzalisha umeme nchini China. Miaka mitatu iliyopita, kampuni hiyo ambayo makao makuu yake yako katika mji wa Harbin, sehemu ya kaskazini mashariki ya China, ilitaka kujenga kituo cha kusafirishia bidhaa zake katika sehemu ya ghuba ya bahari ya Bo iliyoko katika sehemu ya mashariki ya Beijing, hatimaye iliamua kujenga kituo hicho katika eneo la ustawishaji wa uchumi na teknolojia la Qinhuangdao, na kutarajia kusafirisha mitambo mikubwa ya kuzalisha umeme kwa gesi ya asili iliyotengenezwa kwa ushirikiano kati ya kampuni hiyo na kampuni ya GE ya Marekani. Kiongozi wa ofisi ya usimamizi ya kituo hicho, Bw. Xiao Zhenhai alipozungumzia uamuzi wao, alisema,

    "Mazingira ya kijiografia ya Qinhuangdao yanafaa sana kwa sisi kujenga kituo cha kusafirisha mitambo yetu nje. Licha ya hayo, sera nzuri za eneo la ustawishaji la Qinhuangdao katika matumizi ya ardhi, kuhamisha nyumba za wakazi na ujenzi zilituvutia."

    Eneo la ustawishaji wa uchumi na teknolojia la Qinhuwangdao liko katika sehemu ya pwani ya bahari ya Bo, ambayo iko katika sehemu ya kati ya maeneo ya ustawishaji wa uchumi ya miji ya Beijing, Tianjin, Dalian, Shenyang na Yantai. Huko kuna barabara za kasi na njia za reli zinazokwenda sehemu nyingi za bara. Licha ya hayo kuna bandari inayoweza kufikia bandari za sehemu ya pwani ya China na za nchi za nje. Ardhi ya huko pia ni imara sana, ambayo inafaa kwa ujenzi wa bandari, karakana, ofisi na barabara.

    Kampuni ya ADM ya Marekani na kampuni ya Wilmar ya Singapore zikishirikiana zimejenga viwanda vitatu vya usindikaji kwa kuvutiwa mazingira bora ya kijiografia ya huko. Hivi sasa kampuni hizo mbili zimewekeza zaidi ya dola za kimarekani milioni 500. kampuni ya usindikaji wa nafaka na mafuta ya Jinhai ni moja ya viwanda vitatu vilivyoanzishwa nazo katika sehemu hiyo, ambayo inazalisha mafuta ya maharage ya soya. Meneja wa kiwanda hicho cha usindikaji, Bw. Mu Yankui alisema,

    "Sababu ya kujenga mradi wetu huo Qinhuangdao ni kuwa malighafi inayotumika kiwandani kwetu ni maharage. Sehemu ya kaskazini mashariki ni sehemu inayozalisha maharage mengi zaidi hapa nchini ikichukua zaidi ya asilimia 60 ya maharage yanayozalishwa nchini, na zaidi ya asilimia 80 ya maharage hayo yanauzwa kwa sehemu mbalimbali za nchini. Sehemu ya Winhuangdao ni njia ya kupita ya kuingia sehemu za bara. Hivyo, kituo chetu kiko katikati ya sehemu ya kuzalisha maharage na sehemu zinazonunua bidhaa tunazozalisha.

    Bwana Mu alisema kuwa pato la viwanda hivyo vitatu vilivyojengwa na Marekani na Singapore kwa mwaka kutokana na mauzo ni zaidi ya Yuan za Renminbi bilioni 7. Mbali na hayo, viwanda hivyo vina uwanja wa kiasi wenye hekta 60, ambao unatarajiwa kujenga kiwanda kingine cha usindikaji wa nafaka. Ni dhahiri kwamba vitu vinavyovutia uwekezaji, licha ya hali bora ya kijiografia pia kuna mazingira bora ya uwekezaji na umuhimu wake wa kipekee katika ukanda wa uchumi wa sehemu za pwani ya bahari ya Bo. Kwa mfano, kampuni ya Asahi Glass Co. Ltd imewekeza nchini China baada ya kuona maendeleo makubwa ya soko la magari la China, lakini kampuni hiyo haikujenga kampuni yake katika miji ya Shanghai, Changchun na Wuhan, ambayo inazalisha magari mengi, bali imejenga kampuni yake ya kutengeneza vioo vya magari huko Qinhuangdao. Naibu mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo Bw. Sun Xiaoping alipohojiwa na mwandishi wetu wa habari, alisema,

    "Eneo la ustawishaji la Qinhuangdao linazingatia sana kampuni za wafanyabiashara wa kigeni, na limeanzisha mazingira bora sana kwa wafanyabiashara wa kigeni."

    Kampuni maarufu za China na nchi za nje zilizojenga viwanda katika eneo la ustawishaji la Qinhuangdao ni nyingi. Mkurugenzi wa eneo hilo la ustawishaji bwana Hu Yingjie alisema kuwa sababu nyingine ya kupendwa na wafanyabiashara wa kigeni kwa eneo lao ni kuwa toka mwanzoni kabisa walitekeleza usimamizi wa kisasa, toka katikati ya miaka ya 90 ya karne iliyopita, eneo la ustawishaji lilitenga fedha nyingi kwa ujenzi wa miundo mbinu na kuzingatia maendeleo endelevu ya eneo la ustawishaji.

Idhaa ya Kiswahili 2004-09-28