Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-09-29 15:20:34    
China yachukua hatua mbalimbali ili kuongeza kiwango cha elimu ya sayansi kwa umma

cri
Katika miaka ya hivi karibuni, China inafanya uchunguzi kuhusu kiwango cha umati wa watu kuhusu elimu ya sayansi kila baada ya miaka miwili nchini kote. Matokeo ya uchunguzi yalionesha kuwa, kiwango cha umma kuhusu elimu ya sayansi nchini China kinaongezeka mwaka hadi mwaka. Lakini ndugu Li Daguang ambaye alishughulikia uchunguzi huo alisema kuwa, kiwango cha umma kuhusu elimu ya sayansi bado hakijainua kwa haraka nchini China. Anasema:

" baada ya kufanya uchunguzi kadhaa tumeona kuwa, kiwango cha umma kuhusu elimu ya sayansi nchini China kinainuka polepole, mwaka 2003, watu waliofikia kiwango kinachofaa elimu ya sayansi walifikia 1.98% tu, likiwa ni ongezeko la 0.6% kuliko kile cha miaka miwili iliyopita. Takwimu zinaonesha kuwa, hivi sasa nchini China, watu wenye shahada za elimu ya juu, kiwango chao cha elimu ya sayansi kilikuwa juu sana, kiasi hiki ni sawa sawa na kile cha nchi zilizoendelea; habari zinasema kuwa, mwaka 2000, kiwango cha watu wa Japani kuhusu elimu ya sayansi kilikuwa 5.3% na Marekani 17%.

Ili kuongeza kiwango cha umma kuhusu elimu ya sayansi nchini China, katika miaka ya hivi karibuni, China imechukua hatua mbalimbali, kama vile, kujenga jumba la makumbusho la sayansi na teknolojia, na kuongeza vitabu vya elimu ya sayansi; Mtaalamu wa kueneza elimu ya sayansi ambaye pia ni Mkuu wa jumba la makumbusho la sayansi na teknolojia la China Bw. Wang Yusheng alisema kuwa, mafanikio yamepatikana kutokana hatua hizo. Anasema:

" katika miaka ya hivi karibuni, mafanikio yamepatikana katika kazi ya kueneza elimu ya sayansi nchini China. Idara husika za serikali zimechukua hatua mbalimbali zilizosaidia maendeleo ya kueneza wa elimu ya sayansi; watu wengi zaidi wanashiriki kwenye kazi ya kueneza elimu ya sayansi; majumba mengi ya makumbusho ya sayansi na teknolojia na mazingira yamejengwa tayari; vyombo vya habari vimeanza kufuatilia zaidi kazi ya kueneza elimu ya sayansi siku hadi siku. Na mwamko wa umma kuhusu elimu ya sayansi umeongezeka sana."

Mbali na serikali, jumuiya nyingi za kiraia pia zinashiriki kwenye kazi ya kueneza elimu ya sayansi, kamati ya sayansi na teknolojia ya China ni moja kati ya jumuiya hizo. Mkurugenzi wa Kamati ya sayansi na teknolojia ya China Bw. Zhang Yutai alifahamisha kuwa, miaka mingi iliyopita, wanasayansi wa kamati hiyo walikwenda sehemu mbalimbali ili kueneza elimu ya kisayansi. Anasema:

" Shirika la sayansi na teknolojia la China linawahamasisha wanasayansi kwenda sehemu mbalimbali hasa vijijini kueneza elimu ya sayansi na teknolojia kwa vijana. Na kuchukua hatua mbalimbali za kutoa mafunzo , kutumia televisheni, radio, mtandao wa internet, na magezeti kwa kueneza elimu ya sayansi kwa umma."

Serikali na jumuia mbalimbali zilifanya juhudi kubwa, lakini kutokana na idadi kubwa ya watu, msingi dhaifu wa kiwango cha umma kuhusu elimu ya sayansi, ukosefu wa miundo mbinu wa kueneza elimu ya sayansi, kiwango cha umma kuhusu elimu ya sayansi hakiwezi kukidhi mahitaji ya maendeleo ya sasa, na bado kuna pengo kubwa kikilinganishwa na nchi zinazoendelea.

Ili kuongeza zaidi kiwango cha elimu ya sayansi kwa umma wa China, serikali ya China inaandaa mpango wa maendeleo ya sayansi na teknolojia, ambapo itawekeza zaidi katika shughuli hizo, hadi kufikia mwaka 2020, kiwango cha umma kuhusu elimu ya sayansi nchini China kitafikia kile cha nchi zilizoendelea mwanzoni mwa karne 21. Kuhusu hali hiyo, mkurugenzi wa jumba la makumbusho la sayansi na teknolojia la China Bw. Wang Yusheng alijulisha:

" matarajio yetu ni kuwawezesha watu wengi kufaidika na shughuli za kueneza elimu ya sayansi. kuanzisha utaratibu wa kueneza elimu ya sayansi kwa umma. Mbali na hayo tunataka kuimarisha zaidi uwezo wa mashirika , vyombo vya habari na shule katika shughuli za kueneza elimu ya sayansi kwa umma."

Habari zinasema kuwa, katika siku za baadaye, kazi muhimu ya kueneza elimu ya sayansi itawalenga wakulima, vijana na maofisa wa serikali mbalimbali nchini China. China itaenea teknolojia ya kilimo katika vijiji, kuwapatia wakulima ufundi maalumu wa kilimo; kuzidisha mwamko wa watoto na vijana kufanya mashughuli mbalimbali za sayansi na teknolojia; mbali na hayo, China itachukua hatua husika ili kuwawezesha maofisa wa serikali nchini China kuongeza uwezo wao katika sayansi na teknolojia.

Idhaa ya kiswahili 2004-09-29