Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-09-29 17:48:47    
Moshi wa sigara una madhara zaidi kuliko hewa inayotoka kwenye injini za magari

cri

    Je, hewa chafu na yenye moshi wa sigara ndani ya baa ikilinganishwa na barabarani ambako kuna hewa nyingi zinazotoka kwenye injini za magari, kipi kina madhara zaidi? Utafiti mmoja uliofanywa na wataalamu husika wa Marekani umedhihirisha kuwa hewa ya ndani ya baa ni yenye madhara zaidi, na uchafuzi kwa hewa ya ndani ya baa au majumba ya burudani hautaweza kuondolewa bila kuzuia watu wasivute sigara ndani ya majengo hayo.

    Matokeo ya utafiti huo uliofanywa na wataalamu wa Marekani, ambayo yamechapishwa katika jarida la mwezi Septemba linalojulikana kwa "Kazi na utibabu wa mazingira" nchini Marekani yameonesha kuwa ikilinganishwa na ubora wa hewa iliyoko katika barabara za kasi au barabara za mijini, wakati ambao kuna msongamano wa magari, hewa iliyoko katika baa au majumba ya burudani ni yenye chembechembe nyingi zinazoweza kusababisha ugonjwa wa saratani kwa zaidi ya mara 50.

    Bw. Jeams Rapaz ambaye ni kiongozi aliyeongoza utafiti huo, aligundua kwa mara ya kwanza kuwa moshi unaotoka kwenye sigara unasababisha maelfu ya wamarekani kufariki dunia kila mwaka. Katika utafiti huo, Bw. Jeams Rapaz aliona kuwa kiwango cha chembechembe ndogo zenye uchafuzi katika mazingira wanakofanya kazi wafanyakazi wa majumba ya starehe na migahawa 6 ya jimbo la Delaware, Marekani ni cha juu sana kuliko kiwango uchafuzi kinachoruhusiwa katika hewa ya nje ya majengo.

    Kati ya mwezi Novemba mwaka 2002 na mwezi Januari mwaka 2003, Bw. Delaware alifanya uchunguzi kuhusu hali ya hewa katika majumba ya starehe na migahawa 6 ya mkoani Delaware na kupima chembe za aina mbili zilizoko katika moshi wa sigara.

    Matokeo yake yalionesha kuwa kuna microgram 231za chembechembe katika kila mita za ujazo, kiasi ambacho ni mara 15 kuliko kikomo cha chembe kinachoruhusiwa na mamlaka ya mazingira nchini Marekani, na ni mara 49 kuliko chembe zilizoko katika barabara ya kasi ya No. 95 Wilmington, Marekani katika wakati wenye msongamano wa magari. Chembe za uchafuzi za aina mbili zenye madhara kwa afya za watu zilizoko katika moshi wa sigara ndani ya majengo 8 ya burudani wakati wa usiku zilikuwa microgram 134, kiasi ambacho ni mara 5 kuliko kikomo kinachoruhusiwa katika hewa ya nje ya majengo. Ingawa barabara ya kasi ya No. 95 ya Wilmington, ambako kuna uchafuzi mwingi ndani ya hewa zinazotoka kwenye injini za magari wakati wenye msongamano wa magari, lakini chembe za aina hizo ndani ya hewa ya huko ni microgram 7 tu.

    Kupiga marufuku kuvuta sigara ndani ya majengo, hususan katika majengo ya burudani na migahawa ni njia nzuri. Utafiti uliofanywa umeonesha kuwa baada ya kutolewa amri ya kupiga marufuku kuvuta sigara ndani ya majengo, chembechembe za aina hizo zenye uchafuzi katika hewa ya majengo ya burudani yaliyotajwa hapo juu, zimepungua kwa 90%. Habari zinasema kuwa miji 727 ya Marekani imepiga marufuku kuvuta sigara ndani ya majengo, na miji 312 kati ya miji hiyo imetekeleza hatua ya kupiga marufuku ya kuvuta sigara katika baa na migahawa.

Idhaa ya Kiswahili 2004-09-29