Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-09-29 18:55:42    
Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari mjini Beijing kupatiwa chakula chenye virutubisho

cri

    Katika miaka ya karibuni, chakula bora kimepikwa katika shule za msingi na sekondari za mji wa Beijing , hivyo ubora wa chakula cha wanafunzi shuleni umeongezeka sana. Hivi sasa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wapatao laki 3.5 wanakula chakula bora.

    Kiongozi husika wa idara ya elimu ya Beijing tarehe 21 alieleza kuwa mji wa Beijing unaimarisha usimamiaji ili kuhakikisha mazingira ya usafi katika upikaji wa chakula bora cha wanafunzi. Mji huo umethibitisha idara 50 maalmu za kutoa chakula chenye virutubisho cha wanafunzi kwa kutumia zabuni ya hadharani na kukagua usafi wa chakula. Kila siku idara hizo zinawapatia wanafunzi laki 2.3 chakula bora. Idara hizo ziko sehemu zote mjini Beijing. Aidha mji wa Beijing umejenga mikahawa ya wanafunzi yenye kiwango cha juu na kuiwezesha mikahawa ya shule 200 za msingi na sekondari kuwapatia wanafunzi laki 1.2 chakula bora na safi cha mchana kinawasaidia, Hivyo kuwa na mfumo wa kutoa chakula bora unaosimamiwa na idara za elimu na afya za ngazi mbili za mji na wilaya na uunganishaji wa kupika chakula hicho katika shule na kupika chakula na kuwapatia wanafunzi baadaye.

    Kutokana na matakwa ya mradi wa kupika chakula bora wa Beijing, idara ya elimu ya Beijing imeimarisha usimamiaji wa kuagiza vitu vya asili vinavyotumika kutengeneza chakula bora cha wanafunzi na kuboresha zaidi mfumo wa kutoa vitu vya kutengenezea chakula cha wanafunzi na kutoa zabuni ya kununua vitu hivyo kutoka idara zilizopitishwa kwa makini, ili kuhakikisha ubora wa mchele, unga wa ngano, nyama na mayai vinavyotolewa na idara hizo kwa mikahawa inayopika chakula bora. Hivi sasa kituo cha kutoa huduma kwa chakula bora kwa wanafunzi kinaweza kutoa aina 120 za vitu vya asili vinavyotumika katika upikaji wa chakula. Kila mwaka kinaipatia mikahawa inayopika chakula bora tani elfu 4 za mchele, tani mia nne za unga wa ngano, tani mia tano za nyama ya nguruwe na tani mia tano za nyama ya kuku na viboksi milioni 8 vya chakula vinavyotumika mara moja tu.

    Mji wa Beijing pia imeagiza usimamiaji wa kuchambua na kudhibiti vitu vinavyoathiri usafi wa chakula HACCP katika mikahawa inayopika chakula cha wanafunzi. Hivi sasa mikahawa hiyo yote imepitishwa HACCP ya idara za afya na baadhi yao zimepitishwa HACCP ya kimataifa na kuwezesha usafi wa chakula cha wanafunzi kufikia kiwango cha juu mjini Beijing.

    Zaidi ya hayo, mji wa Beijing umezipa idara husika zana za kupima na kusafisha dawa za mbolea zinazobaki katika mboga za majini. Hatua hizo zimehakikisha usalama wa chakula bora kwa wanafunzi.

Idhaa ya Kiswahili 2004-09-29