Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-09-30 18:59:26    
Chaguo kubwa la usafiri lasaidia kupanua upeo wa macho wa wachina

cri

    Watalii wengi wakitaka kwenda Lhasa, mkoani Tibet, hawana chaguo lingine ila tu kupanda ndege, lakini kutokana na ujenzi wa reli ya Qinghai-Tibet, muda si mrefu baadaye, watu wataweza kufika Lhasa kwa kupanda gari moshi. Wakati huo, watu wataweza kuutembelea mji wa Lhasa, ambao huitwa mji wa mwangaza wa jua kwa kuendesha magari binafsi, kupanda ndege na gari moshi. Kutokana na kuongezeka kwa chaguo la usafiri, upeo wa wachina utapanuka siku hadi siku.

    Reli siku zote ni uti wa mgongo wa mawasiliano na uchukuzi nchini China, kiasi cha abiria na shehena zinazosafirishwa kwa njia ya reli nchini China ni kati ya 35% na 55% na kuchukua nafasi ya kwanza duniani. Urefu wa reli nchini China umeongekeza kufika kilomita 73,002 ya mwaka jana kutoka kilomita 21,810 ya mwaka 1949. Hata kwenye sehemu ya magharibi ambayo zamani haikuwa na hata kilomita moja ya reli, sasa imejengwa reli yenye urefu wa kilomita elfu kumi hivi. Sasa mfumo wa usafiri wenye njia 8 zinazoelekea mashariki na magharibi na njia 8 zinazoelekea kaskazini na kusini umeshaundwa nchini China kwa hatua ya mwanzo.

    Kuanzia mwaka 1997, kasi ya gari moshi nchini Chinaimeongezeka mara tano, baadhi ya magari moshi yanaweza kwenda kwa kasi ya zaidi ya kilomita 160 kwa saa. Sasa muda wa kwenda Shanghai kutoka Beijing kwa gari moshi ni saa 11 dakika 58 kutoka ile wa saa 17 dakika 26 ya mwaka 1996.

    Wakati huo huo, uchukuzi wa mizigo kwa njia ya reli nchini China pia umepata maendeleo makubwa. Baada ya kasi kuongezeka mara ya tano, magari moshi yanayopita kwenye reli ya Datong-Qianhuangdao, ambayo ni reli muhimu ya kusafirisha makaa ya mawe nchini China, yameongezeka kufikia 190, kati ya hayo 18 yanaweza kuchukua tani elfu kumi mara moja.

    Licha ya ndege na gari moshi, wakazi wengi wa China wanasafiri kwa basi, wengine wanasafiri kwa kuendesha magari yao binafsi. Mwaka 2003, pato la wastani kwa kila mchina lilikuwa ni zaidi ya dola za kimarekani elfu moja, na kuziwezesha familia nyingi kumudu kununua magari.

    Ripoti iitwayo uchambuzi wa hali ya bei za magari nchini China iliyotolewa na kituo cha utafiti cha teknolojia ya magari cha China ilidhihirisha kuwa, tofauti na karne iliyopita, hivi sasa, magari mengi nchini China yananunuliwa na watu binafsi. Mwaka jana, katika mji wa Beijing. 90% ya magari yalinunuliwa na watu binafsi.

    Kutokana na kuwepo kwa mahitaji ya magari kwa miaka mingi na kushuka kwa bei, magari milioni 2 hivi yaliuzwa mwaka jana, likiwa ni ongezeko la asilimia 75 kuliko mwaka uliopita. Mwaka 2004, aina mpya za magari zinaongezeka, ushindani kwenye soko la magari ni mkali sana, matokeo yake ni bei za magari zinashuka zaidi, hii ni sababu moja ya kuwahamasisha wachina kununua magari. Kusafiri mpaka Lhasa kwa kuendesha magari ilikuwa ni ndoto kabisa miaka kumi iliyopita, lakini sasa watu wengi wameshatimiza ndoto hiyo.

Idhaa ya Kiswahili 2004-09-30