Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-10-08 18:24:48    
Kikundi cha wataalamu wanawake wanaoeneza elimu ya sayansi na teknolojia ya kilimo nchini China

cri

    Kwenye sehemu ya Yang Ling, mkoani Shangxi, kaskazini magharibi mwa China, ambayo ni sehemu pekee ya vielelezo ya sayansi na teknolojia ya juu ya kilimo nchini China, kuna kikundi maalum cha kueneza elimu ya sayansi na teknolojia ya kilimo kinachoundwa na wataalamu wanawake 100. Wataalamu hao wanawafundisha wakulima ufundi wa kisayansi na kuwasaidia kuacha fikra duni za uzalishaji wa kilimo. Wataalamu hao si kama tu wanaeneza elimu ya sayansi na teknolojia ya kilimo mkoani Shangxi, bali pia wameelekeza huduma zao nje ya mkoa wa Shangxi.

    Kikundi hicho kinaitwa "kikundi cha wataalamu wanawake waliojitolea cha Yang Ling", kiliundwa mwaka 2002 na shirikisho la wanawake la sehemu ya vielelezo cha Yang Ling. Wanachama wote ni wataalamu na maprofesa kutoka chuo kikuu cha sayansi na teknolojia cha kilimo na misitu cha kaskazini magharibi na chuo kikuu cha ufundi cha Yang Ling, ambao wanashughulikia mafunzo na utafiti kuhusu miti ya matunda, mboga, mifugo, miradi ya viumbe na kadhalika, wana ujuzi mwingi wa kinadharia na maarifa mengi ya mazoezi halisi. Mwenyekiti wa shirikisho la wanawake la sehemu ya vielelezo vya sayansi na teknolojia juu ya kilimo ya Yang Ling Bi. Chen Jingying alisema kuwa: jukumu la sehemu hiyo ni kuhimiza marekebisho ya miundo ya kilimo kwenye sehemu yenye mvua kidogo ili kuongeza mapato ya wakulima, kusukuma mbele maendeleo endelevu ya kilimo na mchakato wa kilimo cha kisasa. Kwenye sehemu ya Yang Ling kwa jumla kuna wataalamu na maprofesa wa kike zaidi ya 1000 wanaofanya kazi katika maeneo mbalimbali na kupata mafanikio mazuri.

    Katika miaka miwili iliyopita, wataalamu wanawake wa kikundi hicho walikuwa wameeneza ufundi wa kisayansi wa kilimo ndani na nje ya sehemu ya vielelezo ya Yang Ling. Mwishoni mwezi Julai mwaka huu, wataalamu 7 wanawake walikwenda katika wilaya ya Zhangying, mkoani Gansu wakitumia likizo yao na kusafiri kwa kilomita elfu moja hivi, kuwafundisha wakulima elimu ya kisayansi ya kupanda mmea wa dawa uitwao Thorowax. Hii ni mara yao ya pili kufika huko ambako wakulima wengi wanalima Thorowax, waliwafahamisha kwa makini wataalam wa kienyeji na wakulima jinsi ya kupanda mimea hiyo ya dawa.

    Licha ya kueneza elimu ya sayansi na teknolojia ya kilimo kwenye sehemu mbalimbali, kikundi hicho cha wataalamu wanawake pia wanajiunga na kazi ya kuwaandaa wafanyakazi wanawake wa sehemu ya vielelezo ya kilimo ya Yang Ling. Kila mmoja ana jukumu maalum la mafundisho. Hivi sasa, kikundi hicho cha wataalamu wanawake chenye usimamizi mzuri, kozi nyingi, ishara ya aina moja na moyo wa ukakamavu kinajulikana sana katika sehemu ya Yang Ling.

Idhaa ya Kiswahili 2004-10-08