Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-10-13 18:11:25    
Maendeleo ya teknolojia ya kamera za kitarakimu nchini China

cri

    Kamera za aina ya "Dalai"na "Bendera Nyekundu 20" zilizalishwa nchini China katika mwaka 1957, zikifuatiwa na kamera zilizojulikana kwa "Phoenix 205" na "Sea Gull A4"zilizotengenezwa baadaye, ambazo hivi sasa zimehifadhiwa na mashabiki wa kamera katika kabati zao kama kumbukumbu.

    Lakini, kamera za aina hizo zinaonesha historia ya maendeleo ya kamera nchini China. Kamera ya kwanza iliyotumia teknolojia ya tarakimu nchini China ilianza kuuzwa madukani mwezi Agosti mwaka 1999, ilijulikana kwa "Sea Gull DC-33. mwishoni mwa mwaka 2003, kamera iliyojulikana kwa jina la"Legen T40"?na ilithibitishwa na wataalamu kuwa na teknolojia ya tarakimu ya kiwango cha juu. Hali isiyopendeza iliyotokea miaka michache iliyopita, ambayo watu baada ya kupiga picha kwa kamera za tarakimu walishindwa kupata sehemu za kusafisha picha zilizopigwa kwa kamera za tarakimu, hivi sasa maduka yanayoweza kusafisha picha zilizopigwa kwa kamera za tarakimu yako kila sehemu za mijini. Watu wakiona maduka mengi yanayosafisha picha zilizopigwa kwa kamera za tarakimu, wanashangaa na kusema, "Kumbe enzi ya tarakimu imewadia."

    Ni kweli kuwa kamera za tarakimu zimekuwa chombo kinachopendwa sana watu wakati wanapotembelea sehemu za vivutio katika siku za mapumziko. Hivi sasa soko la kamera za tarakimu limepata maendeleo makubwa, na kila mwaka zinauzwa kamera za tarakimu laki 2 na elfu 47 hivi kwa mwaka, na kamera za tarakimu zilizouzwa katika nusu ya kwanza ya mwaka huu zilikuwa milioni 1.2.

    Wakati wa kukaribia sikukuu, kamera za kampuni maarufu za nchi za nje zinashusha bei za kamera zao ili kuwavutia wateja wengi. Hivi sasa kamera za tarakimu zinauzwa kwa wingi sana, hatua ambayo imefanya kamera za kawaida kupoteza soko lake. Katika jengo linalojulikana kwa jina la Hailong, sehemu ya Zhongguancun, muuza duka mmoja alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa. Mpiga picha anaweza kuona mara moja picha alizopiga, hivyo anaweza kuchagua picha zile nzuri mara moja, tena ni rahisi kwake kuzituma na kuzitunza. Hivyo siku hizi kamera za tarakimu zinauzwa kwa wingi siku hadi siku.

    Kampuni ya Legen imeanza kuuza bidhaa za aina nyingi mpya, ambazo ni pamoja na ile inayojulikana kwa S50, ambayo inatoa picha safi yenye chembe milioni 5 katika picha, licha ya hayo kamera za aina hiyo ina uwezo wa kurekodi muziki wa MP3, kutumika kama radio na lenzi ya Video. Kampuni ya Patriot imetengeneza lenzi inayoweza kuvutwa nje kuwa ndefu mara 8.8, ambayo inajitahidi kuwa na kiwango cha zile za kiwango cha juu za kampuni nyingine za kimataifa. Kuinuka kwa kiwango cha teknolojia kumefanya kamera za tarakimu kuuzwa kwa wingi na kwa muda mrefu.

    Lakini katika soko la kamera nchini China, kamera za kampuni maarufu za nchi za nje, zikiwa ni pamoja na Cannon, Sony na Olimpas, toka muda mrefu uliopita zilikuwa zinachukua nafasi kubwa katika soko la China. Mwaka uliopita, China iliondoa kiwango cha uagizaji wa kamera za nchi za nje, hali ya soko la kamera nchini ilibadilika kwa haraka, ambapo miji ya Beijing na Shanghai iliagiza kwa wingi kamera za nchi za nje. Aidha kampuni za kamera za nchi za nje zimebadilisha sera zao za kulenga soko la kamera za kiwango cha juu, badala yake zinajiingiza kwa nguvu hata katika soko la kamera za kiwango cha chini.

    Kutokana na kukabiliwa na shinikizo kutoka viwanda vya nchi za nje ya kulenga shabaha yao hata katika bidhaa za kiwango cha chini, maofisa wa idara ya upashanaji habari wamesema kuwa shinikizo linalotoka sokoni pia linaweza kubadilika kuwa nguvu inayovihamasisha viwanda vya nchini kuzalisha kamera za teknolojia ya tarakimu. Kwani viwanda vya nchini vina hali bora ya kujirekebisha kwa haraka kufuatana na mahitaji ya soko na utoaji huduma, katika usambazaji wa bidhaa na kupunguza gharama ya uzalishaji bidhaa, hivyo vitajihimiza kuchukua hatua mwafaka ili kujiimarisha katika kukabiliana na kampuni za kamera za nchi za nje.

Idhaa ya Kiswahili 2004-10-13